Nimeyakumbuka maisha yangu ya uyatima; Uyatima ni noma sana ndugu zangu

Nimeyakumbuka maisha yangu ya uyatima; Uyatima ni noma sana ndugu zangu

Mkuu hakika Mungu akupiganie
Uko sahihi Kaka, kuna muda inabidi tu tukubaliane na hali,ila mimi suala la ndungu hapana aisee!

I swear to God katika kukua kwangu kwote mpaka sasa sijawahi kuishi kwa ndugu wa aina yoyote yule.

Kitu kinachoniuma mpaka leo ni kuniacha niishi nikiwa kama mtoto wa mtaani katika mji na mkoa ule ambao wamejazana na ndio chimbuko letu.
Kwamba hakuna hata mmoja aliekua na huruma na mimi?
Daaaaah wakuu kuna yime naishiwa mpaka nguvu ya kutyp...[emoji22][emoji22][emoji22][emoji22
 
Jana (Ijumaa) nikiwa kazini Kuna saa nilikosa Kazi (zilikua zimeisha). Nikawazaa, ghafla mawazo ya maisha ya UYATIMA niliyopitia yalinijia.

Ni ndefu sanaa we somaa.!

Japo siwezi kuyaandika yotee, maana UYATIMA wangu ulinipitisha kwenye makubwa sanaa..!!

Nilizaliwa kwenye familia ya watoto 3 tukiwa na baba na mama.
Baba alifariki kwa ku palaryze nikiwa mdogo sanaa.

Baba alikuwa ni mfanyabiashara mwenye mali nyingi ila mama alikua ni mama wa nyumbani.

Kwasababu ya kumkosa mumewe, baada ya baba kufariki mama alikuwa anaumwa umwa Sana.

Hii ilisababisha Mali nyingi kuuzwa na bila kusahau nyengine zilidhulumiwa na ndugu.

Ndugu na marafiki wa baba waligawana mali nyingi sanaa tukaachwa na nyumba tu ya kuishi.

Mama alikua anateseka Sana na mawazo ya kumpoteza mpendwa wake, hii ilisababisha kudhoofisha Kinga ya mwili na hatimae malaria kali ilimjia na kumchukua.

Ilikua ni siku ya jumapili nilipoletewa habari kuwa "Mama yako amefariki".
Aisee Ile siku ilikua nomaa, Mimi na mama tulikua na kijiwe chetu..!! Pale nyumbani (Kona ya barazani kwenye ua alilokuwa analipenda).

Aisee nilikaa pale na kulia sanaa, nilikumbuka ule usia wake, vicheko vyake, sura yake, harufu yake, kifupi niliona dunia imefika mwisho.

Wakati huo nikiwa mdogo sanaa (darasa la 4) ila huwezi amini NAKUMBUKA KILA KITU MPAKA LEO.

Nakuonya mwana JF "Usimfanyie mtoto ubaya" kwamaana "Hawezi sahau".
Mimi japo nilifanyiwa ubaya na ndugu tena nikiwa mdogo ila nakumbuka majina, siku, location yaani kila kitu kwa jambo nililyofanyiwa na ndugu.


Siku ya msiba wa baba watu walijaa wengi na waliiba Mali za pale nyumbani na wezi wote nawakumbuka ""wakina Wajomba zangu""

Baba alikua Tajiri hivyo nyumbani kwetu kulijaa ndugu waliokuja kuomba Msaada.

Ila baada ya baba kufa walipungua sana na baada ya mama kufa ndio kabisaa sikuwaona.

Tulianza kulelewa na dada.

Maisha ya ushua yalipotea na kama upepo, tukaanza shida.

Dada majukumu yalimzidi tuka hamishwa kila mtu kwake.

Mimi nikabaki Dar, mdogo angu mkoani na dada angu akabaki nyumbani.

Huko nilikoenda nilienda kwa mshua mmoja hivi taita Dar pale (rafiki wa baba).

Ila huyu "Mkewe hakunipenda kabisa" sababu mpaka leo huwa siijui.
Nilikua sili Sana, nilifanya Sana Kazi na mengine ila sijui kwanini hakunipenda.

Nilikaa pale miaka miwili, mama akaanda staili moja ili niondoke kwake.

Lile zegwe hausi geli alilijua.
Akanitahadharisha.

Nikamuhadithia shangazi
Shangazi alikuja kunichukua fasta.

Shangazi yangu hakua na maisha mazuri ila nilikomaa hivyohivyo.

Nilikomaa sanaa, chakula hakitoshi, Shule kwenda na miguu tena Dar es salaam, halafu mbali sanaa.
Mwaka mzima hununuliwi nguo mpya..!! Unavaa nguo za kushindia hizohizo mpaka mtaa una kukariri.

Ila nilikomaa.

Shangazi yangu hakuwa na room kwa watoto wa kiume, kwahiyo sometimes nilikua nalala kwenye korido na sometimes nje ya nyumba.

Yaani nje kabisa, milango inafungwa mi nafunga net kibarazani nalala.

Hakua ananitesa na nilikua nina amani.

Kwakuwa chakula kilikuwa hakitoshi nilianza kufanya Kazi kwenye nyumba za watu.

Maisha ya zamani ilikua mwenye hela ndio anabomba la maji la Dawasco.

Hivyo mi nilikua nachotea watu maji wananilipa ndoo moja 50.

Hapo nikawa napata nauli ya kwenda Shule (kipindi hicho mwanafunzi nauli 50).

Na nyengine kabla sijala nyumbani nilikua natanguliza kwanza sambusa, hivyo na kile kidogo cha nyumba nakua nashibaa.

Maisha yalienda mara la 7 nikafaulu.

Miaka ile kufaulu la Saba ilikua dili hasaaa.

Shuleni kwetu tulienda secondary Wa3 tu, yaani tulifaulu Wa3 tu..!!!

Mtaa mzima hongera...!!!

Kufika Shule nikaanza kucheza kamali ili nipate pesa ya kujikimu..!!

Nilikua nawala hasa.

200 inazalisha 3000 mpaka 5000.

Bwana eeeh Kuna siku ikapitishwa karatasi waandikwe majina ya wacheza kamali, na Mimi ndani...!!!

Tulipigwa sanaa siku ile, fimbo kama 100 hivi.
Enzi zile tulikua tunapigwa hasaaa.
Unashika chini huku umebongoa, walimu wanapita na fimbo, ukiishika Tako umefutaa.!!!

Tulipigwa sanaa.

Ila Sasa hata nikiacha kucheza nitapata wapi hela ya kujikimu shule..!!
Shangazi ya kunipa hana, hana uwezo wa kunipa nauli, je madaftari na vitabu atanunua?

Dah maisha yaliendelea, tukawa tunacheza nje ya Shule.

Kufika form 2 nikaongoza wastani kwa Shule nzima.

Ikabidi mwalimu wa darasa aniite "wewe una akili sanaa, kwanini unakua mtundu?"

Nikamuhadithia nayopitia nyumbani, huyu mwalimu niliona kabisa machozi yana mlenga.

Tokea siku hiyo alianza kunichukulia tofauti sanaa.

Form 4 nikaongoza kwa kupata Division 1 Kali sanaaa.

Taarifa zikaenea kwa ndugu na jamaaa + mtaani.

Hongera na masifa kama yoteee.

Ila nyumbani hali ilikua tofauti..!!

Binadamu yangu ye alipata 4 Mimi 1.

Mama ake ikawa kila jambo ananipendelea Mimi..!!

Binamu yangu alini mind sanaaa.

Akawa anatanitaka nitoke kwao, hii "Toka kwetu" mwanzo niliiona ya kawaida sanaa ili kufika form 5 ilikolea sanaa.

Kuna siku nilirudi nyumbani nikafungasha nguo na kusepa gheto la masela wapiga misuli.

Shangazi alimind sanaa.

Akaniita tukaongea na kuahidi kila jumapili nikachukue elfu 5 ya matumizi ya wiki.

Yaani kwa wiki utumie elfu 5..!!
Kula mchana, asubuhi, usiku na hela ya pindi mchikichini..!!

Nilikonda hasaa, maana kila siku nashindia miogo ya Shule.
Maana kila siku natakiwa kutumia buku..!!

Maisha yaliendelea taarifa zikamfikia baba mdogo.

Akaniomba niwe naenda kwake kuchukua misaada.

Nilienda kama wiki 4 mfululizo (kila jumamosi).

Nakumbuka Kuna jumamosi nilienda nikamkuta mkewe na baba mdogo hayupo.

Sasa bana Mimi Nina aibu ya kuomba Msaada kwahiyo muda wa kuondoka nikaaga ili niondoke kimya kimya.

Mama mdogo aliniita akanipa maneno makali "Unasababisha sisi tuishi maisha magumu kisa wewe....." aliongea mengi ila mwisho wa siku alinikataza kwenda kwake kuchukua misaada.

Na kama baba mdogo alijua maana hakuwahi kuniuliza lolote juu ya lile jambo.

Nilifika nyumbani siku hiyo nililia sanaa, nilikumbuka maisha ya baba yupo na mama.
Nililia balaaa.

Ghafla mama mdogo (ndugu wa mama) akaniambia niwe naenda kwake.

Huyu nae alinisaidia mara sijui 6 ya 7 nae akanipa dongo "Kwani wengine hawapo" nilibaki mdomo wazi.

Nikarudi gheto nikajisemea "Sitaki tena msaada nitakomaa mpaka nafia humu"

Ile elfu 20 ya mwisho niliyopewa Msaada nikafanya mtaji wa kuuza vitu vidogo vidogo Shule na mitaani.

Nikaacha kwenda mchikichini (tution) NECTA form 6 sikufaulu vizuriiiiii, ila nilipata credit za Degree.

Nilisoma PCB ila nilipenda sanaa mambo ya biashara.
Afya sikuiwaza kabisaa na Wala sikuipenda.

Sasa bana kuomba mkopo na post, post zinatoka chuo UDSM halafu bodi ya mkopo "NO LOAN".

Nani atanisomesha sasa??..!!!!!

Dah nikawazaa, kumbe shangazi yangu anahangaika.

Akanitafutia ufadhili mmoja wa ada.
Chuoni nikawa nalipa 240,000/= ya mambo mengine ya chuo ila ni Diploma.

Nikajisemea "yaani hizi C zangu za PCB naenda kusoma diploma, huku wenye E na D wanaenda degree"
Maisha gani haya...!!!

Nikabeba begi kwenda chuo.

Chuoni sikua na raha Wala amani, nilipenda masomo ya biashara ila nikawa nasomo visivyojulikana na moyo wangu..!!

Nikiwa Diploma 2 mdogo angu akamaliza form 4, akapata ufaulu wa kawaida ila sio wa kwenda advance..!!

Wakumsomesha HAKUNA..!!

UYATIMA nyie, Achana nao kabisaa...!!

Ikabidi nimpe ahadi ya kwamba anisubiri mi mwaka mmoja nimalize Diploma halafu yeye ataingia kwa ada yangu mi nitaishia hapo..!!

Ila kabla ya hapo nikiwa form 4 na 6 nasubiri matokea na post zakuendelea kusoma nilishawahi fanya sehemu tempo.

Kwahiyo lengo langu lilikua ni kumaliza Diploma halafu niende pale kujishikiza, then mdogo angu aingie chuo.

Nikamaliza diploma kufika ile ofisi kuongea na bosi akakubali. Kunipa Kazi.

Nikawa mpiga Kazi pale.

Nilikomaa kuishi maisha magumu hasaa ili tu mdogo angu aingie chuo.

Aisee ni mengi aiseee.

Ile dogo kumaliza Certificate nikamshikiza pale job na kikazi fulani hivi.
Huku Mimi nika apply Kazi serikalini nikapata Mkoani.
Dah hapo ndio ikawa kama nafuu imeanza kuja.

Maisha yalienda, serikalini kazini nikaomba ruhusa ya kwenda Shule kupiga Bachelor nikaunga Masters.

Sikuacha ndoto zangu zife, nilienda kusoma masomo ya biashara.
Ghafla zile ndoto zilizozimwa kisa yatima kakosa ada zikatimia.

Na mwaka huu naingia darasani kusoma PhD yangu..!!!

Na mdogo wangu aliendelea mpaka akapata CPA..!! Na mwaka huu anaingia darasani kusoma Masters.

Mama yetu alikua anatuambia "baba yenu alitaka na kutamani sanaa msome".

Angalau sasa hata tukifa tunaenda kuwaambia wazazi wetu "Tumemaliza yale mlioyatamani kutupa"

Dada yetu yupo na ameolewa na yeye ndio mama yetu.

Huwa tunamlea vizuri ""Japo tunampaga pesa kimya kimya ili shemeji asijue..!!!""

Aisee ni mengi aisee na siwezi kuyaandika yoteee.

Maana pia nilishawahi fukuzwa na shemeji (mke wa kaka - kaka mtoto wa baba mkubwa) bila kujua sababu..!!
Nilikua naendaga kuwasalimia, mkewe sijui akanichoka na kunifukuza ..!!!

Kifupi ndugu walikua wanadhani na hasa wake wa ndugu zangu walikua wanadhani sijui naenda kumaliza hela za waume zao.

Kifupi hakuna aliyenisaidia bila kulalamika, na kunisimanga.
Na wotee waliona Bora kunitimua ili nisiwaletee shida makwao.

Kifupi mpaka leo ndugu huwa siwaelewi.
Huwa wanapiga simu na kiukweli si "save" namba zao.
Na kesho wakipiga Tena na nikiwauliza "nani mwenzangu" huwa wanakata simu na kusema "huyu siku hizi yupo serikalini na kasoma basi anajidai sanaaa"

Na huwa hawaniambii direct ila Wana mwambia dada au shangazi.

Cha ajabu WAMESAHAU YOTEE WALIYOTENDA..!!!

Kifupi sina swaga yoyotee na ndugu YOYOTE.

Siwachukii ila SINA MPANGO NAO KABISAAA.

Ila mdogo angu anamsemo wake "Atavuna aliyepanda kwenye maisha yangu tu, kwani wakati hatuna wazazi na tunateseka walikua wapi"

Kifupi hatuna connection na ndugu wa upande wa mama woteeeeee yaani hata mmoja sijui yuko wapi.

Ila Kwa baba ni shangazi yangu ndio aliyepambana tukafika hapa..!!!
Tupo nae karibu na tunampenda sanaaa.

Baba yangu kwao walizaliwa Wa2 tu.
Yeye na dada ake ambae alitulea.

Nampenda sanaa shangazi yangu na namuheshimu sanaa.

Siwezi kufika Dar bila kumuona Wala kumletea Zawadi ni Mungu wangu aisee hapa duniani.

Ila ndugu wa mama HAPANA KWA KWELI.

Siwachukii ila HATA SIJUI WAKO WAPI NA SINA MPANGO NAO KABISAAA.
Waliamua kunitupa na Mimi nimejitupa mazima.

Dah tuishie hapo.....

YANAYONITAWALA KICHWANI.

1. Natamani kumuuliza yule mama wa mshua, kwanini alipanga kunifanyia lile tukio ili mumewe anifukuze?

2. Natamani kuwauliza wajomba zangu, kwanini mliamua kutudhulumu mali zetu?

3. Natamani kuwauliza mama wadogo, kwanini mliamua kumuacha dada yao (mama yetu) atulee kwa shida wakati wao walikua wanakuja kwake kulia shida?

Kifupi natamani tu nikae na walionifukuza halafu niwahojii kwanini walinifanyia vile.
Yaani tuhojianee weee mpaka moyo ukaridhika.

Natamani nikae na walionipitisha kwenye shida niwahojiiii mpaka niridhike.

KITU NILICHOSHINDWA NI KUWATAFUTA NA KUONGEA NAO.
Najua watakua wanamiliki simu ila hata kutafuta namba zao NIMESHINDWA ..

Na nimepitia mengi siwezi kuyaandika yoteee mengine yanauma na kuumiza.

Tuishie hapa.

Miss you Daddy and Mammy.

UYATIMA ni nyokooooo sanaaaa.
Uzi huu Kuna vipande vinanihusu, ni kama tumepita njia Moja. Mimi sikuwa yatima ila umaskini WA familia na ukubwa wake.
 
Heri yako umeshakiepuka hicho kikombe japo uliteseka sana, sie wengine bado tupo kwenye mchakato wa mateso sijui mpaka lini. Ndugu wa kweli ni Baba, Mama na kaka/dada mliozaliwa kwenye familia moja tu.
 
Heri yako umeshakiepuka hicho kikombe japo uliteseka sana, sie wengine bado tupo kwenye mchakato wa mateso sijui mpaka lini. Ndugu wa kweli ni Baba, Mama na kaka/dada mliozaliwa kwenye familia moja tu.
Soon, nakuhakikishia bado kidogo tu. Usiache kumuomba Mwenyezi Mungu Mwenye rehema
 
Jamani jamani 😭😭😭😭 mnatuumiza sasa
Mara nyingi sana ndg. upande wa mama huwa bega kwa bega na watoto wa dada/wadogo zao.

Katika maisha tunapitia changamoto nyingi sana, lakini siku zote tusiwasahau waliotushika mkono katika mafanikio yetu ya sasa.

Kwa upande wangu nitamshika mkono aliyenishika mkono, kuna ndugu unaona kabisa ana nia ya kukusaidia lakini hali hairuhusu (Una uhitaji wa laki 1 anakupatia 5000, na hapo kajikamua sana).
 
Huyu mtoa mada ni dizaini ya wale ndugu lawama. Hawa huwa hanawaga shukrani zaidi ya lawama kwa waliowasaidia kufika hapo walipo. Analaumu ndugu hawajamsaidia lakini ukifatilia stori yake unakuta kuna maeneo meng tu kasaidiwa na hao anaowaponda.

Ndomaana kuna jamaa yangu alisema hataki kusikia mambo ya kukaa na watoto wa ndugu nyumbani kwake. shukrani zao ndo zinakuwaga kama hizi. eti nimejisaidia mwenyewe nyooo...mtoto toka lini akajisaidia mwenyewe na akainuka?
Mmmh roho yako ya fisi kabisa mkuu. Yaani wewe ni mulemule kwenye wanyanyasaji.
 
Natamani kuishi ndani ya mioyo ya watoto waishio katika mazingira magumu,yatima na wengineo.

Hii ni ndoto yangu kubwa mno katika maisha yangu na ninaamini nitakuja kuitimiza tu.

Maisha ya upweke Kwa mtoto ni magumu sana 🥺🥺🥺


Nakumbuka mwaka fulani nilikwenda kutembelea kituo cha watoto yatima(hii ni kawaida katika maisha yangu kufanya hivi)nikakutana na katoto kakiume kama miaka minne hivi kamekaa pekeyake pembeni ya mlango chini..jamani nililia mnooo (Nina huruma iliyopitiliza Kwa watoto)

Nakumbuka niliishia kutoa mizigo niliyopeleka..nikaongea kidogo nikaondoka..nilishindwa kuendelea kumwangalia zaidi yule mtoto..

Kilio kikaanza kwenye gari sasa🥺🥺🥺ilibidi dereva apark pembeni aanze kunibembeleza upya.

Picha ya huyu mtoto bado ipo kichwani haijawahi kunitoka kabisa na ndio picha inayonipa msukumo zaidi kutaka kuwa mama wa watoto wengi sana.

Natamani kuwa mbegu iliyo hai mioyoni mwa watoto walioamini kuwa wamekosa tumaini.
Aisee Mungu akupiganie utimize dhamira yako.
Wale watoto wanatia imani unapofika pale na kuanza kusema Baaba huyooo...asee una tambua kuwa wanakosa upendo wa wazazi wote ingawa ni wadogo sana ila wana tambua kuwa wale sio wazazi wao bali ni walezi.
 
Pole sana Mkuu [mention]Liverpool VPN [/mention]

Ila pia kulea mtoto asiye wako ni changamoto

Mwanao unaweza kumkaripia na kumwambia neno lolote, hata la kashfa na kipondo juu na pasiwe na tatizo lolote. Ila ukifanya jambo hilo hilo kwa yatima au mwana asiye wako, inatafsiriwa tofauti kabisa. Na yule mtoto anaichukulia tofauti kabisa, anahisi kafanyiwa vile kwa sababu ya hali yake...

Kuna familia naijua waliishi na yatima, ambaye wazazi wake walifariki na kwa bahati nzuri, ile familia walikuwa na mtoto mdogo ana kama miezi mitatu hivi, so ikawa rahisi tu, mama akamchukua yatima wakashare ziwa moja na mwanae. Akawalea vizuri bila hata shida. Na baadaye mama akapata watoto wengine wengi tu. Familia ikawa kubwaa.

So kwenye kukua wale watoto wawili wakaambia kuwa wao ni mapacha. Na jina la ubini wanatumia moja, shuleni wanapangwa darasa moja. Kila kitu swafi.

Kafika umri fulani ndugu wakaja kumwambia ukweli yule yatima, kuwa wewe hapo unapoishi huyo sio baba yako wala Mama yako. Mama yako amefariki na baba yako amefariki.

Nadhani yule binti alipata msongo wa mawazo, Yule binti aliharibikiwa mazima.

Na bahati mbaya sasa yule mzee naye alikuwa ni mkali sana by nature tu, alikuwaga watoto wake wakizingua zinapita bakora za maana.

Sasa yule binti alichezea bakora sana ila wapii.. akawa anauweka uyatima mbele, kila kitu akiambiwa anakimbilia kwenye kivuli cha uyatima.

Ilikuwa tafrani.

Binti Alitanga tanga sana na dunia.

Kumlea ikashindikanika.

Kaja kujitafuta na kujitambua tena baada ya kama miaka 15 au 20 hivi.

Hapo watoto aliowacha kwenye ile familia wameshasoma wengine wapo makazini.

Akarudi tena kwa wale wazee, kawaomba msamaha. Wakamsamehe. Ndo kuanza tena shule pale alipoishia. Akakomaa komaa na shule kwa miaka kadhaa mpaka akapata degree.

Kasoma zile elimu za watu wazima.

Na akaja kupata na ajira mahali.
 
Huu uzi ni mchungu sana kwa sis wazaz vijana ambao bado ni wapambanaji.
NB
sihofii kifo ila naogopa kufa sasa hiv kwasababu ya watoto wangu na mama yao
 
[emoji3][emoji3][emoji3]muone

Aise Nina huruma sana Kwa watoto ningekuwa hili swala ninauwezo nalo..hakika nisingeruhusu mtoto apitie changamoto kabisa.

Wiki kama mbili nilikutana na mtoto wa kiume(rika la kijana wangu kabisa)usiku Ana fanya biashara ya kuuuza nini Sijui huko aise nilimwaga machozi sana ujasiri sikuwa nao tena Kwa Yule mtoto.

Nikamwambia funga unachokifanya nifuate.nikampeleka sehemu ya kula ale akitakacho..aise mtoto alikuwa na njaa yule [emoji3064][emoji3064][emoji3064]..nilikahoji kanandoto ni katoto ambako kapo kwenye plans zangu.haijalishi ndoto zangu zitawahi ama kuchelewa lakini lazima nikawe mbegu njema moyoni mwake.

Itoshe kusema ninahisia za karibu mno
Hizi ndio sadaka zile tunazozisema.

Na Mimi ngoja mambo Fulani yakae njema nitatake responsibility kwa mtoto mmoja wapo.
 
Hii Stori imenikumbusha mbali.
Pumzikeni kwa Amani Wazazi wangu huko mlipo.
 
Magumu uliyopitia wewe umeamua kumpitisha pia mwanao huyu wa kike kwa kumfanya akose upendo wa MAMA! Hivi unajua umemfanya mwanao naye awe 1/2 yatima??

Nakubali umepitia magumu japo kuna wengine wamepitia magumu zaidi, nasikitika kwamba badala ya kuwa mnyenyekevu shauri ya maisha uliyopitia umekuwa na kiburi na kujiona!
Itakuwa ngumu kumuelewesha jamaa kuwa anatengeneza season ya kilichomtokea kikatokee kwa huyo binti au mjukuu.

Ni muda sasa a estblish strong family, aoe. Asije akaamini kuwa mdogo wake aliesta nae, atasimamia majukumu yeye ikitokea hayupo duniani ohoo.
 
Kumbuka Maisha ni FUMBO gumu sana. Mafanikio ni MITIHANI migumu sana. Ulikopita usipaangalie kwa uchungu bali kwa furaha, kwasababu umesha vuka huko.

Mafanikio ni mazuri ukiweza kuwasaidia wengi kadri uwezavyo bila kujali walifanya nini wakati ulipokuwa ukihitaji, na bila kujali watakulipa nini au kukukumbuka ulivyo wasaidia. Kwa kifupi tenda wema nenda zako. Usiweke kinyongo kwenye haya maisha, mafanikio ni FUMBO, ulichokipata kwa jasho kinaweza kuondoka kirahisi sana,bila kujali ulivipata kwa jasho la damu au kwa ugumu vipi.

Usikumbuke saana mapito kwa maana ya maumivu, kumbuka mapita kwa maana ya uongeze juhudi kutafuta.
Wasaidie wote bila kubagua, na watafute ndugu ,jamaa na marafiki popote walipo, furahi nao hata kama huwasaidii chochote.

Kuna rafiki yangu tumekuwa pamoja, alikuwa na uwezo mkubwa sana kielimu, lakini hakufanikiwa kusoma sana kwasababu zingine ulizozieleza, hawakuwa na kipato kizuri kuweza kusoma.

Alifanikiwa kwa biashara, alitumbua sana. Ila bahati mbaya alipata ajali akavunjika mikono yote miwili, Mkono mmoja ulikatwa kwa jinsi ulivyokuwa umesagika, mkono wa kushoto waliweza kuuunga unga, upo lakini hauna nguvu sana.

Maisha yalipiga U-Turn, aliishiwa, akakimbiwa na mke, hadi ndugu. Alirudi nyumbani kwao anaishi na mama yake ni mzee sana, lakini ndiye umuhudumia muda mwingi.

Huwa anakumbuka, alivyo kuwa anakula bata, na aliokuwa akila nao, leo hawamkumbuki tena.

Usilipize ubaya kwa ubaya, lipa wema kwa kila baya unalotendewa, na Mungu atakubariki sana.

Ubinadamu mgumu sana, ni hayo tu.
 
Back
Top Bottom