Zee Korofi
JF-Expert Member
- Oct 5, 2021
- 1,604
- 1,430
Wazima? Mimi ni kijana tu wamiaka 24 nasoma bado, nipo chuo mwaka wa 3. Mwaka wa 1 niliingia kwenye mahusiano na mwanamke mmoja tu, ni binti wa rikalangu. Sikujua kumbe mumewe ni mtu mzito tu mpaka nilipoona picha wakiwa wawili.
Alikuwa analalamika haridhishwi na pia mumewe alikuwa na kisirani, ukizingatia maisha ya chuo magumu basi nilikubali kuendelea naye ili nipate chochote kitu.
Baadaye akaja kupata mimba ambayo kwa mara ya kwanza nilijua ni ya mume wake, mpaka baadaye aliponitonya kuwa ni yangu na kunipiga biti nikae kimya atanilelea mtoto,.
Yeye na mumewe wana watoto wawili, mwanangu sasa ana miaka karibu miwili na kafanana na mamaye. Roho inaniuma kwani huyu bosi analea mtoto asie wake. Nataka sana kuishi na damu yangu.
Kikubwa kilichonileta hapa ana ujauzito mwingine kwani tuliahiriki mapenzi siku za hatari. Na mumewe hajajua kwani kamdanganya mimba ni yake. Naogopa mno kwa kweli kwani sijazoea mikiki ya hivi.
Jamani naombeni uahauri life la chuo ni gumu mno na nashindwa kumuacha huyu dada, na siku zinavyokwenda najikuta nampenda na mimi. Na vipi kuhusu mwanangu na ujauzito wangu?
Nimuache? Je vipi mwanangu nitampataje? Yeye anasema atasomeshwa, atakula na atalala nisiwe na shaka.