Nimpeleke mtoto shule ya milioni 1.5 au hela nimuwekezee UTT au hisa?

100% Fact
 
Bado unajitafuta wewe, ad upewe maoni Tena mwanaume mzima khooo*!
 
Hard time create strong men.

Strong men create good time.

Good time create weak men.

Moral of the story👇👇👇👇👇

Kayumba Schools Create Strong men.
 
mkuu utaishia kizidi kuwa maskini na majuto mbeleni na tatizo ni hapo uliposema eti "mama wa mtoto yaani mkeo ndio anakung'ang'aniza ww mumpeleke mtoto huko english medium kisa kaona mashoga zake na marafiki na anaowajua wamepeleka watoto wao huko basi ndio analazimisha na nyinyi mfate mkumbo je,kiuchumi mnalingana na hao mnaojilingisha nao.? kwenye matumizi ya pesa wanawake hawanaga huruma na mkeo ni aina ya wale wanaotamani maisha ya wengine na kama ilivyo hulka za wanawake wao wanapenda kushindana na kuonyeshana ufahari nakutaka sifa tu na kujlinganisha au kutamani maisha ya walio wazidi na ww mume usipokuwa mkali mwenye misimamo utaumia..acha huo ujinga wa kulinganishwa kipato chako kiuchumi na wengine eti flani kafanya vile nasi tufanye au flani kampeleka mtoto wake english medium na sie tumpeleke ni umaskini wa kujitakia huo ishi mwisho uwezo wako na si kumfurahisha mke kwa gharama ya maumivu yako..kama ww huna uwezo wa hizo shule private una hela za mawazo sijui unabangaiza basi acha ujinga akiforce alipe ada yeye au mchangie nusu kw nusu
 
Mpeleke shule boss. Elimu ndio urithi usioweza kuharibiwa na yeyote. Hela ni makaratasi.
Duh so to u " Education is better than money?"

Kama ni hivyo then kwanini shule za EMs hawawapokei watoto wenu hadi mlipe hela?

Because to them money is better than education.

As a matter of fact kwani Kayumba watoto hawasomi?
 
Kama urithi wa pesa utakushinda kumuachi mtoto basi acha urithi wa elimu nzuri au jina kama ww ni mtu maarufu
 
Hakuna mbadala wa elimu nzuri, period, kayumba ni upuuzi, tu, taja waziri anayesomesha mtoto kayumba! Hata, waziri wa elimu, hapeleki mtoto kayumba,
 
Fact ni ujinga kulipia mamilioni English Medium mtaala wa Necta wakati shule za serikali wanafundisha bure
 
Do so to u " Education is better than money?"

Kama ni hivyo then kwanini shule za EMs hawawapokei watoto wenu hadi mlipe hela?

Because to them money is better than education.

As a matter of fact kwani Kayumba watoto hawasomi?
Sijazungumzia money. Nmezungumzia urithi. Huyo ni mzazi akimwachia mtoto elimu bora hata asipo mpa pesa huyo mtoto ata survive.
Hiyo ya kuchagua pesa anatakiwa kuchagua mtoto mwenyewe akiwa na uwezo wa kufanya choice lakini sio mzazi.
 
Hakuna mbadala wa elimu nzuri, period, kayumba ni upuuzi, tu, taja waziri anayesomesha mtoto kayumba! Hata, waziri wa elimu, hapeleki mtoto kayumba,
Elimu nzuri ni Nini?

Sasa mkuu unataka ujifananishe na mawaziri wenzako wanasomesha Kwa hela za wizi.

Usiige kunya kwa Tembo utapasuka msamba
 
Sijazungumzia money. Nmezungumzia urithi. Huyo ni mzazi akimwachia mtoto elimu bora hata asipo mpa pesa huyo mtoto ata survive.
Hiyo ya kuchagua pesa anatakiwa kuchagua mtoto mwenyewe akiwa na uwezo wa kufanya choice lakini sio mzazi.
Elimu bora ni nini?
 
Mungu alivyo wa ajabu. Unamtoa mtoto Ems ili kuokoa ada iende UTT unaanza kupata pesa zinazotoshea kununua uniform na daftari za Kayumba. Zile ulizodhani zitakuwa za saving zinapotea kabisa. Acha mtoto shule mengine yatajipa mbele. Huenda mzazi wako asingekupeleka usingepata nguvu ya kupambana mtaani kila siku ungekuwa unamlaumu amechangia kufeli kwa maisha yako. Lakini kwa sasa huna cha kumlaumu umebaki na maisha yako.
 
Ila nakupa ushauri mmoja,mtoto akianza english medium chekechea hakikisha primary anaenda shule hizo hizo la sivyo atakuwa kilaza kwakuwa hataweza kuelewa vizuri kufundishwa kwa kiswahili primary

Unaweza kuona utani lkn nina ushahidi tosha,yani mwanzo lazima atapata sana shida kuswitch kutoka kiingereza mpaka kiswahili
 
Kupanga ni kuchagua kama lengo ni kuwa na msingi mzuri hasa WA Kiingereza mpeleke...Kama unaona Kayumba kuzuri Sawa pia... Yaani nachojaribu kukuonyesha hapa Jenga picha ya faida na hasara za Kila upande ..

Mfano umesema Una malengo umtunzie Hela uwe mtaji WA baadae ,jiulize huyo mtoto atapenda kufanya biashara,Hali ya maisha ya baadae unaifahamu n.k .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…