Nimrudishie nini Bwana?

Nimrudishie nini Bwana?

Mulama

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2011
Posts
3,036
Reaction score
1,808
Nimrudishie nini Bwana kwa ukarimu wake wote alionitendea? Nitakipokea kikombe cha wokovu na kuitangaza amani ya Bwana kwa neno lake, Zaburi 116:12.

Mungu wangu u mwaminifu sana kwangu hata sasa umenipa makumi mawili matatu hapa kwenye ardhi yako nikiwa timamu na afya tele, ahsante Mungu kwa upendeleo huu mkubwa kwangu nisioweza kuulipa.

Lakini sasa niruhusu nikutumikie nikawe chombo cha amani nikahubiri usalama na amani kwa watu wako ili wakusifu wewe Mungu wetu.

Na kwa kazi yako utaniweka na utimamu na uzima hata makumi mawili matatu mengine nikutumikie Mungu wangu. Ni katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristu naomba na kushukuru, Amiina.[emoji120][emoji120][emoji120]
 
Nilipoona kichwa cha bandiko nikajua ni miongoni mwa waliokula teuzi za Hangaya.

Hongera mkuu kwa ukuu aliokufanyia muumba.
 
Kalambe asali usisahau kuchomeka ndugu zako na rafiki kwenye vitengo kuna kutenguliwa pia
 
Back
Top Bottom