Nimwombe Rais Samia awaondoe haraka wanajeshi wetu kule DRC Congo. Mnapigana na nchi ya EAC

Na waifu hua anatamba kitaa na anamkubali mume wake...🤣
Alafu mume mwenyewe ndo wewe hapo...
Physical unaweza kusema ni mtu mwenye akili timamu...
Ila sasa 😁😁😁😁😁😁😁
 
Na Kagame siyo wa mchezo mchezo. Ni Putin wa Afrika huyu, akiamua kumung'oa mama jua halizami.

PK aliwahi kumwambia JK, I will hit you!. JK hakutia neno.
Una uhakika na unayosema? Baada ya hapo kamuulize Sultan Makenga wa M23 kilichomkuta.Si walikuwa wapo supported na huyo PK.
 
Well said DRC Tanzania haiwezi kuicha ikadondoke kizembe najua soon hao M23 watafurushwa tuu,CDF alikwenda kule last month kustudy situation najua watakuwa wanajua uimara na weekness zao.
 
Hawapo serious wa-Congo wanataka wengine wanunue ugomvi wao.
Ndivyo walivyo hata kwenye maisha ya kawaida. Wale wenyeji wa asili wa MATAIFA YA RWANDA, BURUNDI na KONGO yaani PUISSANTS [BSC] - wao migogoro huwa ni sehemu ya maisha yao na wakati mwingine huwa wanaingilia migogoro isiyo wahusu. Huwa wana tabia ya kununua UGOMVI 🇨🇩
 

Vita ya Congo itakoma pale Madini yatakokwisha kule kongo na M7 na Kagame kufa
 
Well said DRC Tanzania haiwezi kuicha ikadondoke kizembe najua soon hao M23 watafurushwa tuu,CDF alikwenda kule last month kustudy situation najua watakuwa wanajua uimara na weekness zao.
Mwenzangu unaonekana una taarifa kidogo sana za kuhusu vita ya Drc.Au unapotosha kwa makusudi.Umewahi kusikia kwamba gari la UN lilipata ajali likiwa likiwa ndani ya Drc likakutwa lina shehena yq silaha za moto.Ukiwaona wakongo wanawafukuza monisco unaweza dhani ni wehu.Ila kiukweli vita ile inachochewa na mataifa makubwa kwa sababu ya maslahi yao binafsi.inasikitisha kuona nchi mojawapo ya africa inasambaratika.hakuna raisi ataingia congo aweze kuleta amani.na utaona vita iko kwenye maeneo yenye rasmali tuu.ukienda bukavu au kinchasa ni kama uko nchi nyingine.Hii pia imehamia hadi kule central republic.

kinachoumiza zaidi kuwa watoto na wanawake ndiyo wahanga wakubwa sana.
 
Na Kagame siyo wa mchezo mchezo. Ni Putin wa Afrika huyu, akiamua kumung'oa mama jua halizami.

PK aliwahi kumwambia JK, I will hit you!. JK hakutia neno.
Wewe usiniambie?!
 
Yes naelewa kinacoendelea ndugu ni kweli Manusco wanahusika pakubwa na ndio maana Serikali ya DRC imewaambia waondoke mwisho ni December 2024 na baadhi ya kambi wameshakabidhi kwa serikali ya DRC kwenye hilo jimbo chini ya Gavana Cirimwani.Pamoja na yote serikali ya Felix Tshekedi inajitahidi sana kupambna ila baadhi ya makamanda wake ni wasaliti sababu ya rushwa ndio maana baadhi wameondolewa na kupelekwa Kinshasa.Pia vikwazo vya silaha waliyokuwa wamewekwa kununua ilichangia jeshi lao week.Lakini kwa sasa wana mpka Drone.
 
Acha wapambane wapate uzoefu wa vita mkuu. wamejibweteka sana, wamekalia kuchukua mikopo na kula bata tu. Tena mama angewapeleka wote
 
CDF alikwenda kule last month kustudy situation najua watakuwa wanajua uimara na weekness zao.
Hiv najiuliza, what if cdf kaenda huko (kama ulivyodai), halaf m23 wakamlamba bomu akafa, sijui nini kingetokea
 
Wapiganaji wetu pambaneni kwa heshima ya umoja wa EAC na Afrika..

Wapiganaji wetu pambaneni kwa ajili ya ukombozi wa Afrika..Tuliweza na tunaweza

Wapiganaji wetu piganeni zaidi ya kipindi cha Mwakibolwa..Mnaweza💪🏿

Bunge letu liongeze bajeti mahsusi kwa ajili yw Jeshi..
 

Ni kweli,Ila mfumo wa usalama wa nchi ya DRC umeshakufa siku nyingi sana,yaani ni nchi inayoenda kama bendera.Tshekedi ni robot remote yake iko Ulaya na marekani.

Jumuiya za africa (mfano Sadec na Au) zimemezwa kabisa. Nusu ya Jeshi la Drc limesheheni mamuluki waliopandikizwa kwa kisingizio cha malidhiano.Tena hapa tunazungumzia nafasi zote za juu kabisa za jeshi zimeshikwa na mamuluki, wamelidhoofisha kabisa.Yaani taarifa zote za kiinteligencia zinawafikia waasi kabla yautekelezaji.Halafu wakawekewa zuio la kutouziwa silaha.ukipeleka suma Jkt inaweza simamia usalama wa nchi ile kuliko jeshi la Drc.

Tuendelee kuiombea ile nchi.Mungu awasaidie .ni nchi nzuri yenye utajiri mkubwa ardhi nzuri kabisa.
 
Hiv najiuliza, what if cdf kaenda huko (kama ulivyodai), halaf m23 wakamlamba bomu akafa, sijui nini kingetokea
Aaaagh!!
Kitapigwa kisago kuanzia hapo Goma mpaka Kigali.
CDF kiongozi mkubwa bro.
 
Na Kagame siyo wa mchezo mchezo. Ni Putin wa Afrika huyu, akiamua kumung'oa mama jua halizami.

PK aliwahi kumwambia JK, I will hit you!. JK hakutia neno.
Mwambie ajaribu kuigusa TZ huyo putin wa mchongo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…