Nimwombe Rais Samia awaondoe haraka wanajeshi wetu kule DRC Congo. Mnapigana na nchi ya EAC

Nimwombe Rais Samia awaondoe haraka wanajeshi wetu kule DRC Congo. Mnapigana na nchi ya EAC

‘Kuiba japo madini kidogo’😁😁😁😁😁!!!
Hata mimi nakuunga mkono katika hilo,

Lakini ukweli mchungu ni kwamba , hiyo nchi ya kuiba madini iko wapi, Tanzania? Hii hii nchi yetu ambayo tunajiibia madini yetu wenyewe,!! Hivi ni kiongozi gani mwenye akili hiyo aende kuiba madini Congo?

Ili ayapeleke wapi? Kuna kiongozi mwenye akili hiyo ya kwenda kuiba madini Congo kwenye vita wakati anaweza kuiba hapahapa bila kutumia hata manati,

Acha Kagame aibe mwenye uchungu na maendeleo ya nchi yake , lakini sio hawa tuliowapa dhamana ya kutuongoza ,

Wanakula kulaini hapahapa bila kuhangaika na mambo ya vita.

Hebu kaa kwa utulivu uitafakari nchi yako kwanza na uililie hasa,

Hayo angeweza kuyafanya Magufuli tu,

Mtu ambaye alikuwa na vision na target ya kuipeleka Tanzania sehemu fulani
Lakini nae inasemwa kuwa aliibiwa madini sana na PK kwenye ukuta aliojenga Mererani
 
..amani ktk nchi jirani ni neema kwa nchi yetu.

..kuna biashara kubwa kati ya Kenya na Tanzania kutokana na amani iliyoko ktk nchi zetu majirani.

..sasa fikiria tukiwa na majirani wengine zaidi ya Kenya wenye amani na mafanikio ya kiuchumi nchi yetu itafaidika kwa kiwango gani.
Biashara yetu na Kenya ni kubwa kwa sababu Kenya ni tajiri wa kipato kuliko sisi na ina uchumi mkubwa, suala la amani ni nyongeza tu, unaweza kuwa na amani na ukawa masikini.
 
..Mhhh!!

..kuliwahi kutokea massi huko nyuma, lakini kulikuwa na utulivu wa kiwango fulani wakati wa Mobutu.

..Laurent Kabila alitawala kwa amani kwa kipindi kifupi sana, kabla hajavamiwa na waasi waliofadhiliwa na Rwanda, na Uganda.

..Ni ukweli usio na mashaka kwamba waasi wanaofadhiliwa na Rwanda na Uganda wamesababisha vifo na maafa makubwa kuliko wakati wowote ule baada ya uhuru wa Congo.
Mabadiliko ya tawala kutoka kiimla mpaka kidemokrasia huko Kampala na Kigali ndio mwanzo wa kurejea kwa amani na utulivu huko Drc mashariki
 
Kuuawa askari imetokea tu kama Bahati mbaya,unajua vita vya DRC ni kama mradi?
Inasemekana baadhi ya askari wetu wanaotoa hadi hongo,waende huko, kwasababu pesa wanazolipwa ni nyingi sana,ndo ambazo wakitoka huko wakifika huku wanaanza kujenga majumba na starehe mbalimbali.
Imetokea tu.
 
Biashara yetu na Kenya ni kubwa kwa sababu Kenya ni tajiri wa kipato kuliko sisi na ina uchumi mkubwa, suala la amani ni nyongeza tu, unaweza kuwa na amani na ukawa masikini.

..mahali penye vita ni vigumu wananchi wake kufanya shughuli za uzalishaji mali na matokeo yake ni umasikini.
 
Mabadiliko ya tawala kutoka kiimla mpaka kidemokrasia huko Kampala na Kigali ndio mwanzo wa kurejea kwa amani na utulivu huko Drc mashariki

..ni vigumu sana watawala wa Rwanda na Uganda kuruhusu demokrasia.

..Si umeona Museveni amemteua mwanae kuwa Mkuu wa majeshi?

..kuna kipindi huko nyuma Museveni alimteua mdogo wake kuwa Mkuu wa majeshi.
 
Hizo tawala Zina mwisho mkuu
 
Na Kagame siyo wa mchezo mchezo. Ni Putin wa Afrika huyu, akiamua kumung'oa mama jua halizami.

PK aliwahi kumwambia JK, I will hit you!. JK hakutia neno.
Awachezee hao hao kongo lakini sio TZ.
Amuulize Iddi Amin Dada alifanywa nini na TZ
 
..Mhhh!!

..kuliwahi kutokea massi huko nyuma, lakini kulikuwa na utulivu wa kiwango fulani wakati wa Mobutu.

..Laurent Kabila alitawala kwa amani kwa kipindi kifupi sana, kabla hajavamiwa na waasi waliofadhiliwa na Rwanda, na Uganda.

..Ni ukweli usio na mashaka kwamba waasi wanaofadhiliwa na Rwanda na Uganda wamesababisha vifo na maafa makubwa kuliko wakati wowote ule baada ya uhuru wa Congo.
Utulivu uliokuwepo wakati wa Mobotu ilikuwa ni kwa sababu ya msaada wa USA kwa sababu Mobotu alikuwa adui wa Ukomunisti, baada ya Ukomunisti kuanguka na vita baridi kuisha Mobutu alikosa umuhimu kwa US akapoteza uungwaji mkono, maovu yake waliyokuwa wanayafumbia macho muda mrefu yakaanza kupewa uzito ndipo hapo na waasi na wapinzani wakarejea ulingoni Congo kwa nguvu kubwa sana. Mojawapo ya hao waasi ni Laurent Kabila ambaye alipata msaada na ushirikiano mkubwa kutoka kwa Kagame, Museveni na hata Tanzania.

Tangu wakati huo vurugu na maasi zimekuwa na muendelezo DRC kwa sababu Laurent Kabila hakuweza kutawala au kuidhibiti DRC vizuri na zaidi sana aligombana na kutofautiana na warlords wenzake, Kagame na Museveni walioshiriki kumuweka madarakani.
 
Haina mashiko kwa mtu aliyevaa mawani ya mbao, na kusahau mikakati ya kupambana na China juu ya mali hizo hizo katika eneo hili. Tunaangalia maswala ya kidunia kirahisi rahisi kwa kutumia 'one dimensional view' na kusahau mikakati pana zinazotumiwa na hawa watu.
Hivi kwani ushiriki wa hao mabeberu katika eneo hilo umeanza leo na mgogoro huo wa Kagame na M23?
Huo wimbo wa mabeberu umepitwa na wakati, China ndio mvunaji mkubwa wa madini na mbao huko DRC kwa sasa kwa njia halali na haramu.
 
Mabadiliko ya tawala kutoka kiimla mpaka kidemokrasia huko Kampala na Kigali ndio mwanzo wa kurejea kwa amani na utulivu huko Drc mashariki
Hakuna dalili demokrasia itapata nafasi Kampala au Kigali kwa miaka mingi ijayo, lakini pia DRC imekuwa ikitawaliwa kiimla tena na madikteta wajinga kwa muda mrefu sana, hata Tshisekedi aliporewa ushindi na Kabila kutoka kwa Fayulu ili awe kibara wake na amlinde.
 
Sijajua wanajeshi wetu wanafia nini kule DR congo wakati sasa imejulikana bila shaka kwamba wanapigana na wanajeshi wa Rwanda ambayo ni nchi mwanachama wa EAC.

SOLUHISHO ya vita ile ni kuiwekea vikwazo RWANDA na kuifukuza EAC haraka iwezekanavyo.

Mama yetu mpendwa nakuomba uwaondoe haraka watoto wa taifa letu wanaopigana na M23 kule DRC.damu yao inamwagika kwa sababu gani?

View: https://www.youtube.com/watch?v=HHtxvhSPgAQ&t=124s&pp=ygUWdGhlIHBlb3BsZSAgd2hvIGFzayBtZQ%3D%3D

Mwombe kagame aondoe majeshi yake Congo anapigana na nchi za EAC.
 
Na Kagame siyo wa mchezo mchezo. Ni Putin wa Afrika huyu, akiamua kumung'oa mama jua halizami.

PK aliwahi kumwambia JK, I will hit you!. JK hakutia neno.
Story za vijiweni hizi na ovyo kabisa! Mheshimu Amiri Jeshi Mkuu wetu na nchi. Hao M23 ulisahau walivyochapwa enzi za Mwakibola? Muhimu tuiombee DRC amani, wahuni waondoke na askari wetu waendelee kuwa salama. 🙏🙏🙏
 
Na Kagame siyo wa mchezo mchezo. Ni Putin wa Afrika huyu, akiamua kumung'oa mama jua halizami.

PK aliwahi kumwambia JK, I will hit you!. JK hakutia neno.
Alisikika mlevi mmoja akiwa mitaa ya Manzese Mtaa wa Fisi 😂😂😂
 
EeeenHeeee, jamaa wanavyo pamba, kwa mtu asiyejuwa haya atadhani Kagame kweli ni Putin wa hapa!
Hapana, labda ingefaa kumfananisha na Netanyahu wa hapa, kwa sababu hiyo ndiyo 'model' muhimu anayo ifuata yeye.
Ulinganisho pekee na Putin, labda ni huko kutaka maeneo ya jirani ya nchi zinazomzunguka ambako watu wa asili ya Rwanda wamejipenyeza kwa wingi.
Kagame ni Putin wa Africa. Usiwe mbishi dogo. Kagame akikutaka wewe hakukosi
 
Hiyo vita sio ya kuisha leo wala kesho provided M23 wana support ya nchi jirani. Adui (makundi yote ya waasi) wakizidiwa wanauwezo wa kupotea haraka kama walivyo na uwezo ku-mobilise jeshi haraka hali ikitulia na kulianzisha tena.

Tanzania na wasaidizi wengine waipe Congo ultimatum msaada wa kijeshi uende sambamba na serikali ya Congo kuwekeza heavily kwenye jeshi lao kulinda mipaka yao na kuli-control hilo eneo. Awawezi kuli-control hilo eneo ifike wakati tuache fate ichukue mkondo wake kama ni annexation ya eneo let it be aitokuwa nchi ya kwanza kumegwa kwa sababu ya serikali kushindwa ku-control eneo.

Bila ya Congo kutoa road map ya adhma yao ya kuli-control hilo eneo miaka 20 baadae bado tutakuwa tunapeleka askari wakati wenyewe huko Kinshasa wako busy kuboresha mikorogo na kukata mauno.

Ifike hatua lazima Tanzania ione seriousness ya Congo kutaka kulinda himaya zake yenyewe kabla ya kuji-commit kuwasaidia miaka zaidi ya 20 ya kuwasaidia inatosha kama wenyewe hawana mpango wa kuweka strong military presence huko. Kwani sisi nani alitusaidia Amini alipoitaka Kagera si wenyewe tulilinda eneo letu.

Let them annex it kama wa-Congo wameshindwa kulilinda eneo lao inatosha, watasaidiwa mpaka lini.

Iła M23 lazima nae atiwe adabu kipindi hiki kwa kuuwa askari wa Tanzania, lazima ajue sumu aionjwi.
The thing is, tukiwaacha Congo, siku M23 wakishinda vita next stop ni kwetu..
Kuliko kupigana vita kwenye ardhi yetu ni bora tutume vikosi nje hata miaka 100 kama vitasaidia vita isije kwetu.

Hio ndio sababu tunaendelea kutuma vikosi, bila kutuma watu Congo mpaka leo ile vita ingekua imehamia Kigoma, na tusingekua tunaingelea wanajeshi watatu kufa, tungekua tunaongelea wananchi 70 na wanajeshi 10+ kufa..
 
Tofauti yetu na east Congo ni kwamba Nyerere alitumia jitihada nyingi sana kwenye nationalism.

Tanzania sijui sehemu nyingine zaidi ya Ngara (I’m open for education) na tena kabilla la wahangaza tu wanaongea Kinyarwanda tena as a second language, lakini Kiswahili ndio lugha kuu.

Na wahangaza ninao wajua mimi walio kulia Dar ni waswahili pengine wazaramo na wandengereko kunishinda (mind you upande wa mams yangu ni wandengereko huo uswahili kwetu ni wakunitisha).

Isitoshe asilimia kubwa ya hayo makabila ya mpakani wanajitambua kama watanzania kuliko hizo lebel za uasi mnazotaka kuwapa. Hata huko vijijini ambapo wapo watu wa makabila ya mpakani wanaokaribisha raia wa nchi jirani. Ni watu wanaoishi huko huko wenye kuongea lugha moja na hao wageni ndio wanao report uingiaji wa waamiaji haramu (ndio tuelewe umuhimu wa natiolism propaganda na kazi kubwa aliyofanya JKN) sio rahisi kama tunsvyodhani wengi wetu.

Hiyo inakwambia muhimu ni nationalism efforts ya mipaka yetu kuliko kutaka kuwapa watu wa mipakani labels za hovyo and mistrust kisa wanaongea lugha moja na watu wa nchi jirani.

Sisi wenyewe ndio tunaotaka kuchochea huo mgawanyiko kwetu ambao aupo; be careful na wachangiaji wa JF kuna mijitu ina agenda zao. Unakuta jitu kila siku yeye ni mada za ugomvi wa kidini tu we vipi.
 
Hiyo vita sio ya kuisha leo wala kesho provided M23 wana support ya nchi jirani. Adui (makundi yote ya waasi) wakizidiwa wanauwezo wa kupotea haraka kama walivyo na uwezo ku-mobilise jeshi haraka hali ikitulia na kulianzisha tena.

Tanzania na wasaidizi wengine waipe Congo ultimatum msaada wa kijeshi uende sambamba na serikali ya Congo kuwekeza heavily kwenye jeshi lao kulinda mipaka yao na kuli-control hilo eneo. Awawezi kuli-control hilo eneo ifike wakati tuache fate ichukue mkondo wake kama ni annexation ya eneo let it be aitokuwa nchi ya kwanza kumegwa kwa sababu ya serikali kushindwa ku-control eneo.

Bila ya Congo kutoa road map ya adhma yao ya kuli-control hilo eneo miaka 20 baadae bado tutakuwa tunapeleka askari wakati wenyewe huko Kinshasa wako busy kuboresha mikorogo na kukata mauno.

Ifike hatua lazima Tanzania ione seriousness ya Congo kutaka kulinda himaya zake yenyewe kabla ya kuji-commit kuwasaidia miaka zaidi ya 20 ya kuwasaidia inatosha kama wenyewe hawana mpango wa kuweka strong military presence huko. Kwani sisi nani alitusaidia Amini alipoitaka Kagera si wenyewe tulilinda eneo letu.

Let them annex it kama wa-Congo wameshindwa kulilinda eneo lao inatosha, watasaidiwa mpaka lini.

Iła M23 lazima nae atiwe adabu kipindi hiki kwa kuuwa askari wa Tanzania, lazima ajue sumu aionjwi.
Matatizo ya vita ya Congo ni jeshi la Congo kuwa very corrupted !
Congo sio wa kuwaamini kushirikiana nao kwenye vita !
Kuna uwezekano baadhi ya wanajeshi wa Congo wako upande wa M23 na upande wa nchi Yao wanacheza kote kote Shauri ya biashara ya dhahabu .
 
Back
Top Bottom