Nina 5,000,000 tu. Naweza kununua gari ipi ikiwa na hali nzuri?

Waungwana nimechoka kutembea kwa mguu, Nina ka milioni 5 nilitaka nitafute ka miguu minne nipumzike shida kutembea, ila sina uzoefu na mambo ya magari ni aina zipi za magari naweza kununua ikiwa na hali nzuri kwa hiyo bei?
Hiyo gari ukipata nijulishe

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
 
Tafuta sienta au wish namba c zipo kibao
 
Gari ni bodi mkuu sio engine.
 
Honda ni gari mbovu hata hivyo sio tu ya mnada ila hata wewe ukiagiza leo hii! Sijawahi kuona Honda ambayo haina usumbufu labda ile hondaFit

Agiza honda namie niagize spacio af tuone nani atakuwa analia lia [emoji28][emoji28][emoji28] daily!
Honda ni nyoko Sana sitaki hata kulisikia Hilo jina mamaeee....
 
Steering ni ngumu kuliko fiat mbaula[emoji1787][emoji1787][emoji1787]Bro wewe ni comedian sn asee

Speaking of fiat ,siku moja jamaa kaja na fiat yake kuchukua kontena ofisini kwetu ikabidi nim escort kuingia Nayo bandarini,tumefika Kona ya Malawi cargo tuingie Mofed dereva kila akikata Kona usukani mgumu balaa utafikiri anakata Kona ya meli[emoji1787][emoji1787][emoji1787]..me namtazama Tu anavyohangaika na sterling.Si akanichenjia bn[emoji1787][emoji1787]

"aah mwanangu unazinga bn hunioni ninavyoangaika hapa na kusababisha jam nyuma huko"
..ikabidi tushike wawili usukani ili kukata Kona[emoji1787]..Kona ulienda kukubali karibu na mtaro nusu tuimwage kontena ahahhaah..mwamba anatembea na taulo kubwa Kwa ajili ya kufutia jasho[emoji1787]

Nimecheka sn kuifananisha gari ya mwanao kuwa ngumu km fiat mbaula[emoji1787]

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Honda ni gari mbovu hata hivyo sio tu ya mnada ila hata wewe ukiagiza leo hii! Sijawahi kuona Honda ambayo haina usumbufu labda ile hondaFit

Agiza honda namie niagize spacio af tuone nani atakuwa analia lia [emoji28][emoji28][emoji28] daily!
Unamaanisha hata hii Honda model hii nayo ni mbovu??
 
Baba acha ningumu sana yani usukani unapambana nao kama unavyopambana na umaskini yani😂
 
Nenda Instagram kuna page ya mtu anaitwa JACKTAN SAFARI kwa pesa yako utapata gari nzuri...utaletewa popote kwa gaharama zako.
 
Waungwana nimechoka kutembea kwa mguu, Nina ka milioni 5 nilitaka nitafute ka miguu minne nipumzike shida kutembea, ila sina uzoefu na mambo ya magari ni aina zipi za magari naweza kununua ikiwa na hali nzuri kwa hiyo bei?
Suzuki swift Oldmodel
Unapata kali sana Tena ni gari imara sana
Nimekushauri kwa nia njema...hayo mengine yoote unaweza kupata ila hutapata lenye ubora kama hili nimekushauri japo Uamuzi ni wako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…