Nina changamoto ya usikivu hafifu. Natafuta kazi; ikiwa ya kutengeza sofa itanifaa zaidi

Hilo jina nipe yote lina maana gani?
Mkuu hili jina lilikuja tu wakati nafungua id hii kwani id yangu ya mwanzo nilifungua mda wakati nipo shule ina jina majina yangu mawili halisi inakuwa rahisi mtu kunifahamu. Sasa ikawa kila nikiotea jina bandia likakataa mwisho nikabahatisha hili ndo likakubali. Kwangu halina maana yoyote mkuu
 
Sahihi sana mkuu, pole pia changamoto ni nyingi
 
Haina noma mkuu nikajua lina maana
 
Si ununue kifaa cha kukusaidia kukusikia earing aid...hata cha kichina tu
 
Ila samahani kidogo hii ishu imekuwa serious sana .Nyuzi kibao zimerindima kuhusu huu ulemavu wa kupoteza kusikia sijui tatizo ni nn!?
Wengi hawakuzaliwa na tatizo hilo , changamoto mbalimbali wanapata katika kuendea fursa mbalimbali .

Cc Mheshimiwa Dkt. Gwajima D
 
Si ununue kifaa cha kukusaidia kukusikia earing aid...hata cha kichina tu
Mkuu asante kwa ushauri, swali kama hili nilishajibu 👇
Asante mkuu, vile vifaa vinaitwa hearing aid nimeshatumia hasa wakati nipo shule, bahati mbaya havijawahi kunisaidia wala sidhani kama vimeshamsaidia mtu mwenye tatizo kama langu kwani kazi yake ni kuongeza tu sauti
Pia na hii👇
 
Ni kweli tatizo sio la kuzaliwa binafsi limenianza nikiwa shule ya msingi sikumbuki ni mwaka gani na kadri siku zinavyokwenda ndo linazidi kuongezeka kwani uwezo wangu wa kusikia sasa sio kama wa miaka miwili au mitatu nyuma, na hospitali zetu kila nikienda solution yao ni hiyo hearing aid
 
Pole sana mkuu, usikate tamaa mimi ni mwenzako pia, japo sijui kiwango chako cha usikivu.

Ushauri wangu ni endelea kupambana na hiyohiyo kazi ulio na ujuzi nayo,kwetu wenye shida za hearing inshu za kuajiriwa tofauti na serikalini ni shida sana.

Kama uwezo upo kasome ualimu, waalimu wanasjiriwa sana serikalini.
 
Vile vifaa havisaidii, na vikisaidia msaada wake mi mdogo sana.
 
binafsi sijazaliwa nalo na lilianza baada ya kumaliza darasa la 7
 
Pole Sana .
Naimani MUNGU atakuvusha katika hii changamoto nothing impossible. Keep GOD first.
 
Kuwa strong na Hali iyo Ni maisha yetu wanadamu,hapa duaniani tunapita tu.
Ila nilivyokuona ujuzi wako nikawaza kuwa mtu anaweza akafungua ofisi wewe ukawa fundi mkuu. Mnaelewana malipo mnalipanaje kwa kila kazi inavyopatiakana
Sema saivi mfuko hauko vizuri mie nimekuwazia ivyo
 
Asante sana, binafsi nahitaji sana kitu kama hicho ila namna ya kumpata mtu awekeze kwako nayo mtihani
 
I feel you brother pole sana. Daaah. Naelewa ushajaribu mengi kuwa sawa. Sema kipande cha kazi. Nikuombe pambana online. Tena ukiweza una simu nzuri fungua insta account tangaza biashara yako. Jiamini tena waambie watu wewe mtu wa aiina gani, tunahuruma sana watanzania.tutakusaidia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…