Nina changamoto ya usikivu hafifu. Natafuta kazi; ikiwa ya kutengeza sofa itanifaa zaidi

Nina changamoto ya usikivu hafifu. Natafuta kazi; ikiwa ya kutengeza sofa itanifaa zaidi

Pole sana Ndugu, Nina TATIZO kama lako, nimedumu nalo Kwa takribani miaka 5, kiukweli ni changamoto Sana Kwani Kuna baadh ya FURSA zinakupita unaziona kabisa kisa tatizo la Usikivu, Kikubwa usikate tamaa MUNGU Yupo Anasikia kilio chako, kuhusu vifaa hivyo huwa wanatoa Bure ila havisaidii Nami nimevijaribu ila havisaidii zaidi ya kuongeza tatizo.
 
Habari zenu wakuu,

Mimi ni kijana wamiaka 24 kwasasa, elimu yangu ni kidato cha nne ambapo nilifaulu vizuri ila nilishindwa kuendelea na masomo kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo kutosikia vizuri.

Baada ya kumaliza shule mwakav2015, kuanzia 2017 nilianza rasmi kujifunza kutengeneza sofa katika ofisi za ndugu zangu ambapo mpaka sasa nilipofika nina ujuzi wa kutosha kutengeza sofa na vitanda vya sofa.

Changamoto ni kwamba hapa nilipo nakosa kazi zangu binafsi kutokana na hali yangu niliyonayo naishia mara moja moja kufanya kazi za mafundi wenzangu kwa malipo kiduchu ambayo kiukweli yanashindwa kunitoa hapa nilipo kwani bado nakaa nyumbani kwa ndungu zangu.

Naandika uzi huu kuwaomba wana jamiiforums wenye uwezo kunisaidia kupata kazi iwe kama hii niliyo na ujuzi nayo ama yoyote nipo tayari kwani nahitaji nijikwamue nijitegemee na mimi.

Mawasiliano yangu 0788362088 itapendeza ukinitumia sms maana hatutoweza kusikilizana vizuri kwa simu, nipo Dar.
Mimi nimechukua namba. If anything happens ntakuchek. Je unaweza jiajiri kama ukipewa mtaji? Hapa naongelea kukadiria gharama za mwanzo pamoja na location
 
Hilo jina nipe yote lina maana gani?
Mkuu nimecheka kwa sauti usiku huu kwa hili swali lako. Ila kuna mdau aliongea point moja kubwa sana, kuwa kama wahitaji msaada basi muhusika ajaribu kutumia majina yenye heshima
 
mimi nina tatizo kama la mtoa post icho kifaa hakisaidii kwani tatizo lake sio masikio bali ni kichwa ukimuongelesha anakisikia ila haluelewi kama tunavyojua sauti hutoka kwa mfumo wa mawimbi na kazi ya ubongo ni kuyachakata mawimbi kuwa kitu kinachoeleweka ila ufanisi wetu ni hafifu mfano mtu anakuita jumaa unamgeukia alafu anakuambia mama kasema fusgajsjksjbska hapo kwenye fusgajsjksjbska ndio kimbembe lazima umuombe arudie na anaweza kurudia na bado ikawa changamoto kingine bila kumuangalia usoni mdomoni huelewi asemacho hata ukiongea kwa sauti nyuma yale haelewi ila anasikia unaongea.
Nimekuelewa sana mkuu, pole sana. Ni changamoto tu zitakwisha
 
Sijajua kwingine Ila Kwa Baadhi ya maeneo niliyofika dar naona inaongoza Kwa changamoto Hii hasa Kwa vijana hasa hawa wanao bet.
Wanao bet online kwenye mikeka au wale wa bonanza na kale ka mlio kao ka kikikikikikikikikiki kikikikikikiki mpaka 50k,lazima masikio yadanji
 
Mimi nimechukua namba. If anything happens ntakuchek. Je unaweza jiajiri kama ukipewa mtaji? Hapa naongelea kukadiria gharama za mwanzo pamoja na location
Nashukuru mkuu, naweza kama nitapata mtaji, naweza kukadiria ghrama na kutafuta location nzuri kwa ajili ya biashara
 
Back
Top Bottom