Nina hofu kubwa na huyu kuku kaingia ndani kataga kwenye sofa na sijui katokea wapi, sielewi nifanyeje, au ni uchuro?

Kawaida Tu.Mi juzi nimekuta Kataga kwenye kabati la vyombo.
 
Wabongo bana,sasa hapo jipya ni lipi, Kuku kutaga?je angetaga paka?Uwe unafunga milango/mlango wako kila wakati.
 
Hizo nguo zinachefua kuwepo hapo. Hadi kuku kavutiwa alidhani ni kichaka.

Vp mara mgeni anaingia akute minguo imezagaa namna hiyo!
 
Wadau hamjamboni nyote?

Wenye elimu zenu mkiongozwa na ndugu mshana na bujibuji nipeni ushauri

Niwatakie siku njema
kula yai gentleman achana na imani potofu kwenye vitamin..

kwenye ajira yangu ya kwanza,
washirikina waliwahi kunifungia kufuli kwa nje ya nyumba yangu usiku, wakachinja jogoo mkubwa sana mweusi mlangoni wakanyunyiza damu mlangoni kwangu na wakapasua na nazi2, wakaacha na vikaratasi vilivyo andikwa lugha nisiyoelewa..

Majirani walipo nisaidia kuvunja mlango asubuhi ile mbele ya viongozi wa hicho kijiji, nikawaambia huyo kuku nitakula supu na nyama itakayobaki nitapika rosti ya maana sana ya nazi.

Nikawaambia,
msiogope endeleeni na shughili zenu kwa amani, kijiji hicho si hami mpaka nitakapoamua mwenyewe.

Mbona mpaka leo nipo salama nadunda tu?🐒
 
Baba huna hamu ya nyama ya ngoko.kamata tia roba piga kisu kaanga utumbo vichwa na miguu kiwili wili pila supu.
Yai nalo chemsha kula.
 
Chumba kiko rafu namna hiyo kwanini kuku asitage popote, huenda alifananisha na banda lake.
 
Usitie hofu,huyo kuku kapendezwa na hizo nguo hapo,akaona km Ni kiota,Jambo la maana waambie majirani zako ,wape na yai lao.
Jitahidi kufunga mlango laa sivyo kila siku atakuwa anatagia hapohapo
Hilo lundo la nguo kwenye makochi aliona ni kiota cha kutagia.
 
Sasa umeweka lundo la nguo limekaa kama kiota yy afanyeje...
 
Wawekee mazingira mazuri bandani watatagia huko, ila Kwa hizo nguo hata kama ww ungekuwa kuku ungetaga hapo hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…