Nina jasho lenye harufu kali sana. Je, kuna dawa ya kutibu tatizo hili?

Chanzo cha harufu ya kwapa mara nyingi inatokana na bacteria, njia za asili zinazoweza kupambana na tatizo hilo jaribu kutumia limao kama wadau walivyochangia, pia bicarbonate(baking soda) inasaidia, apple cider vinegar pia inasaidia.

Unafanya kusugua kwapa kila baada ya kuoga.
 
Tafuta shabu maduka ya dawa ya asili isage iwe unga koga jidugue na scrub gloves kisha jikaushe ule unga wa shabu utie maji pakaa kwapani pia tafuta deodorant zipo nzuri 25,000 kurndelea usisahau kunyoa vuzi la kwapani mara Kwa mara
 
DR Mambo Jambo
Baba Swalehe
Dr Lizzy
Carlos The Jackal
Herbalist Dr MziziMkavu

Hebu msaidieni ndugu yetu huyo aepukane na fedheha hiyo
Huyu Jamaa Anaweza Kuwa na Tatizo la hyperhidrosis..
Ila kuna uwezekano Akawa na Ugonjwa wa Ngozi ajaribu Kumuona Daktari wa Ngozi..

Maana Harufu Huletwa na Fungi au Bacteria kwenye Ngozi...Japo inaweza kusababishwa na Mabadiliko ya Hormones pia..

Cha kumshauri Atumie Deodorant Hizi Dry skin Deodorant sana sana atumie antiperspirant Deodorant Sana sana zilizo na bei nzuri kwa Tz atumie NIVEA antiperspirant Deodorant..

akitumia Hiyo Tatizo litaisha au litapungua kabisa..

Cc: Staphylococcus Aureus
 
Tafuta ukoko wa ugali tia kwenye dishi au ndoo kaoge hatasahizi kesho sa 6 lazima utume kiasi takrima
 
Una nyota mtoajashoooo
 
Check figo zako kwanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…