Nina kinyongo na chuki kali sana. Je, hili ni tatizo?

Nina kinyongo na chuki kali sana. Je, hili ni tatizo?

Mwizukulu mgikuru

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2021
Posts
5,715
Reaction score
13,739
Mimi ni mtu mwenye kinyongo kikali na mtu akinitendea ubaya nina tatizo la kumuweka moyoni miaka hata ipite miaka kumi.

Baba yangu ni mtu mwenye imani sana ya dini na huwa ananishauri sana kuwa niwe mtu wa kusamehe lakini mimi huwa nashindwa kusamehe yaani mpaka nihakikishe nimelipa kisasi au nisikie adui yangu katoweka duniani ndipo roho yangu hutulia.

Kwa mfano juzi nilienda kutoa pesa kwa wakala kiasi kidogo tu baada ya kutoa ile pesa yule wakala aligoma kabisa kunipa pesa yangu kwa kigezo kwamba hajaiona meseji. Aisee mpaka sasa roho yangu inanihimiza nimfanyie kitu kibaya yule wakala japokuwa watu wananishauri niachane nae tu.
 
Yawezekana ni roho chafu ya ancestors wako imekuvaa wewe. Since kila kitu huanzia katika ulimwengu wa roho basi tatizo lako lipp kiroho zaidi. Hivyo waone viongozi wako wa kiroho watakupa msaada
 
Mwambie Yesu atulize dhoruba za moyo wako nayo hali itakoma.
 
Mimi ni mtu mwenye kinyongo kikali na mtu akinitendea ubaya nina tatizo la kumuweka moyoni miaka hata ipite miaka kumi.

Baba yangu ni mtu mwenye imani sana ya dini na huwa ananishauri sana kuwa niwe mtu wa kusamehe lakini mimi huwa nashindwa kusamehe yaani mpaka nihakikishe nimelipa kisasi au nisikie adui yangu katoweka duniani ndipo roho yangu hutulia.

Kwa mfano juzi nilienda kutoa pesa kwa wakala kiasi kidogo tu baada ya kutoa ile pesa yule wakala aligoma kabisa kunipa pesa yangu kwa kigezo kwamba hajaiona meseji. Aisee mpaka sasa roho yangu inanihimiza nimfanyie kitu kibaya yule wakala japokuwa watu wananishauri niachane nae tu.
Kuhusu hiyo ishu ya wakala, ulimuonesha meseji iliyorudi kwenye simu yako? Kwa sababu ni ukweli uliowazi, wakala hawezi kukupa tu hela iwapo, hajapata ujumbe mfupi.

Na hata huo ujumbe umechelewa, anatakiwa ajiongeze kwa kuangalia salio lake! Maana hakatwi chochote anapoangalia salio. Option ya mwisho kabisa, ilikuwa ni wewe mwenyewe kuwapigia huduma kwa wateja, na kuwaambia hiyo shida yako. Ikiwezekana wakurejeshee huo muamala wako.

Sasa huoni hayo mambo ya kutaka kumfanyia kitu mbaya huyo wakala, yako kinyume kabisa na ustaarabu wetu kama wanadamu?
 
Back
Top Bottom