Nina laki 9, nahitaji skrepa ya Prado niikarabati

Habari za majukumu, nina fedha isiyo taslimu shilingi laki tisa(900000 TZS), ambayo itakamilika kufikia mwezi wa 10 mwaka huu. Nimewiwa kununua usafiri wangu ila nimeamua kutumia njia tofauti kidogo.

Yaani kama ni hesabu za kugawanya, basi tungesema nimetumia njia fupi. Kwa jiji hili la DSM usafiri ni changamoto kubwa mno, hasa local transportation of passengers(usafiri wa hapa hapa Dar).

Naomba kama kuna mtu atakuwa na skrepa au anamfahamu mtu au taasisi yenye skrepa hizo, basi tuwasiliane na atoe details hapa. Ili kila mmoja aone na afahamu hivi vitu.

NB: nahitaji new model, au hata ya mwaka 2020 kulingana na series za matoleo yake.

Karibuni sana!
Hata body ya vits hupati
 
Engine ya tu ya prado mfano 1kz ni 4-4.5m, chasis tuu hupati kwa hiyo hela labda ununue carrier ya prado na hiyo hela
Wapi huko wanauza 1KZ 4.5m ? Maana zipo za aina mbili Intercooled na isio na intercooler...
 
Mpaka muda huu sielewi kama Watanzania wengi ni mbumbumbu au la! Mada ni rahisi na ipo wazi mno, "nahitaji kwa mwenye kujua mahali wanauza skrepa za prado anielekeze" , ila bado watu wanatumbua tu macho na maswali ya kipuuzi.

Hivi WaTZ wamerogwa na nani? Au ulaji wa ugali ni chanzo? Yaani akili zimelala mno, na uchakataji wa taarifa ni 'very poor'.
Kesho nenda Tandale wanapokata magari ma prado yapo kibao..mkuu
 
Mpaka muda huu sielewi kama Watanzania wengi ni mbumbumbu au la! Mada ni rahisi na ipo wazi mno, "nahitaji kwa mwenye kujua mahali wanauza skrepa za prado anielekeze" , ila bado watu wanatumbua tu macho na maswali ya kipuuzi.

Hivi WaTZ wamerogwa na nani? Au ulaji wa ugali ni chanzo? Yaani akili zimelala mno, na uchakataji wa taarifa ni 'very poor'.
Mpaka muda huu sielewi kama wewe ni mbumbumbu au la! Mada ni rahisi na ipo wazi mno, "nahitaji kwa mwenye kujua mahali wanauza skrepa za prado anielekeze" , ila bado wewe unatumbua tu macho na maelezo yako hayo ya kipuuzi.

Hivi WaTZ mmerogwa na nani? Au ulaji wa ugali ni chanzo? Yaani akili imelala mno, na uchakataji wako wa taarifa ni 'very poor'.
 
Habari za majukumu, nina fedha isiyo taslimu shilingi laki tisa(900000 TZS), ambayo itakamilika kufikia mwezi wa 10 mwaka huu. Nimewiwa kununua usafiri wangu ila nimeamua kutumia njia tofauti kidogo.

Yaani kama ni hesabu za kugawanya, basi tungesema nimetumia njia fupi. Kwa jiji hili la DSM usafiri ni changamoto kubwa mno, hasa local transportation of passengers(usafiri wa hapa hapa Dar).

Naomba kama kuna mtu atakuwa na skrepa au anamfahamu mtu au taasisi yenye skrepa hizo, basi tuwasiliane na atoe details hapa. Ili kila mmoja aone na afahamu hivi vitu.

NB: nahitaji new model, au hata ya mwaka 2020 kulingana na series za matoleo yake.

Karibuni sana!
Screpa una maana gani?
Body ya gari lililopata ajali au body nzima.
Kwa taarifa yako body za gari ni ghali sana, laki tisa hata mlango used hupati.
 
Msimkatishe tamaa hivyo mwenzenu, mwacheni atafute mwenye nao watafikia bei hata akianza na steering iko poa
 
Back
Top Bottom