Nina laki 9, nahitaji skrepa ya Prado niikarabati

Nilitegemea hili, jiwe la gizani hilo naona walengwa mmeanza kutoa milio.
 
Nilitegemea hili, jiwe la gizani hilo naona walengwa mmeanza kutoa milio.
Mpaka muda huu sielewi kama Wewe ni mbumbumbu au la! Mada ni rahisi na ipo wazi mno, "nahitaji kwa mwenye kujua mahali wanauza skrepa za prado anielekeze" , ila bado unatumbua tu macho na vijembe ivyo vya kipuuzi.

Hivi Watz mmerogwa na nani? Au ulaji wa ugali ni chanzo? Yaani akili zimelala mno, na uchakataji wa taarifa ni 'very poor'.
 
Screpa una maana gani?
Body ya gari lililopata ajali au body nzima.
Kwa taarifa yako body za gari ni ghali sana, laki tisa hata mlango used hupati.
Naomba unipe details chache tu za bei za bodies na frames plus suspension systems(basic).
 
Laki Tisa hii take home ya House girl haupo serious
 
Labda rim zake utapata tena zilizotumika. Alafu wewe ni msomi eti? Huyajui vizuri magari sio!
 
Kwanini usimwambie ukweli tu.
 
Nenda maeneo ya tandale utafanikiwa, maduka ya vifaa vya magari aina zote zipo na hilo unalo hitaji utaelekezwa. Ni wazee wa kukata kata magari na kuuza spaer au chuma chakavu.
 
Ngoja nami nitoe maoni yangu japo naweza nisiwe sahihi.

Mleta uzi huenda anamiliki prado ama kuna mtu wake wa karibu anamiliki prado, hivyo ameanzisha huu uzi kwa lengo moja kati ya yafuatayo.

1. Kufikia huo mwezi wa 10 atakuja hapa na kutuaminisha kwamba amepata na tayari ameipeleka hiyo skrepa gereji. Hapa wapenda mseleleko wataingia king kisha jambo la pili lichukue nafasi.

2. Akishaleta uzi wake humu atawaambia amepata chimbo lenye mazaga ya bei nafuu, watu watajaa PM kisha kupiga kutaanzia hapo kisha atabadili ID na kuiacha hii. Hapo watu wameshalizwa tayari.

Kwa akili ya kawaida hauwezi kutafuta laki tisa kwa zaidi ya miezi 5 kisha utafute kununua gari uende ukaikarabati wakati kuna pikipiki za bei hiyo kwa watu.

Mwisho kabisa, labda ameamua kujifurahisha kwa kusoma maoni yatakayotolewa humu
 
Loh
 
Totally wrong
 
Hiyo itakuwa gari au kituko?! Gharama za kufufua gari kutoka skeleton level hadi kuwa gari ya kutumika kwa hali ya sasa kuanzua ufundi+spare parts, rangi, hadi ikae sawa utakuta umelipa milioni 5 ama zaidi.

Milioni 5 unapata Passo iliyo katika hali nzuri sana, vits nzuri sana, Suzuki swift safi kabisa, Nissan March nzuri kabisa, Carina T. I, Colora 111 na 110, kwa kifupi kwa level hizo utapata list kubwa ya gari ambazo utatumia vizuri tu na utasolve changamoto yako ya kukosa usafiri.

Labda nikwambie kitu gari haununui kwasababu una pesa nyingi ila unanunua kwasababu unahitaji usafiri. So jitoe babu.
 
Wewe unaelewa maana ya scrape au unaongea tu hapa. Umesema unataka scape ya Prado watu wameelewa kuwa wewe unashida ya kutaka utelezi wa kupata mabaki ya gari uunde yako.

Kukusaidia wamekwambia hilo halitawezekana hiyo hela yako laki 9 inaweza ishia katika kuwalipa mafundi kukuwekea parts kwenye hiyo gari. Ila sio kuifanya iwe kamili.
 
Kabisa. Ukiona mtu anaendesha hata Passo hapa mjini asiee mpe heshima yake ni zaidi ya baba mwenye nyumba. Yaani hapo amesacrifice mambo mengi sana kuweka kwenye gari.

Gari ni zaidi ya kuwa na mke na familia. Ukiona mtu ana gari na hana mke na familia jua ni maamuzi yake binafsi sio kwamba ameshindwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…