Tahadhima kwenu kizazi Cha Covido-19!
Leo akihutubia kijijini kwake Chato katika uzinduzi wa shamba la miti (Silayo Forest) Rais Magufuli alitumia jukwaa hilo kutoa msimamo wa Serikali kuhusu vita kuu dhidi ya janga la Corona.
Pamoja na mambo mengine, Magufuli ameonya Watanzania kujihadhari na chanjo mbalimbali zinazoletwa na "vipepeo weupe" yaani wazungu akisema, "nchi hii ni tajiri sana" akimaanisha weupe hao hawana nia njema na Afrika.
Rais Magufuli ametolea mfano,"kuna nchi moja ililetewa chanjo kwa mabinti wa miaka 14 ili kujikinga na kansa ya kizazi lakini ikaja kugundulika chanjo hiyo iliwafanya wasichana hao wasizae kabisa", wawe wagumba.
Sijui Magufuli amesahau, hakuwepo nchini, au amedanganywa na wasaidizi wangu. Kwa mujibu wa kumbu-kumbu zangu ni kwamba chanjo hiyo ilitolewa kwa watoto wa Kitanzania kati ya Mwaka 2013/14 ikihamasishwa na Wizara ya Afya chini ya udhamini wa USAID.
Kama ni kweli maneno ya Mr. President, basi nchi hiyo ni Tanzania na tujiandaye kwa wimbi kubwa la kinadada wasiozaa, wagumba.
Hofu kubwa kwa wasichana wetu waliochanjwa.