Dennis Urio
Ni mwanajeshi,ni shahidi mwenye maslahi pande zote aliyetolewa kafara na waliomuamini baada ya kujikuta hawana kesi yenye mshiko.
Dennis Urio kama kweli aliota taarifa kwa DCI basi alistahili kwanza kuwekwa katika WITNESS PROTECTION YAANI alindwe kama shahidi.Denis URIO hakupaswa kuwa shahidi katika kesi kama hakuwa analindwa na kama alikuwa ni chambo.
Kwa mtazamo wangu ningewaona POLISI wana akili kama wangempa MBOWE Kanya BOYA mmoja ambaye angekuwa kwenye DEEP COVER kwa ajili ya kutafuta ushahidi na sio kumtumia DENIS na makomandoo wengine ambao hawakuwa na HATIA.
Dennis URIO ameonekana msaliti kwa MBOWE,Kwa Wanajeshi wenzake ambao walikuwa na maisha yao akawafanya chambo,Kwa marafiki zake, kwa watanzania na kwa CHADEMA. Kwa nini? Kwa sababu ya UZEMBE wa JESHI LA POLISI. UZEMBE wa KINGAI, UZEMBE wa DCI BOAZ.n.k.
Swali la kujiuliza ni JE DENIS URIO alifanya kosa kwenda kuripoti au waliokosea ni DCI na KINGAI kwa namna walivyoshughulikia jambo hili?Jambo kla UGAIDI sio PETTY CRIME lilihitajika kushughulikiwa na TAASISI zinazohusiana na USALAMA na kwa umakini mkubwa.
SASA Tunamuona Dennis kama msaliti na shujaa ambaye ametolewa kafara na upande wa Jamhuri.
Usitamani kuwa DENNIS ndio maana wakati mwingine watu wanakataa kuisaidia POLISI kwa sababu wanachojua POLISI ni kubambikia watu kesi, KUIBIA watu, KUUA watu na kukusanya rushwa.
Mungu Ibariki Tanzania