Nina mashaka Luteni Urio anaenda kuharibu ushahidi dhidi ya Mbowe na wenzake 3. Fact hizi hapa
Natabiri bila Shaka kwamba baada ya ushahidi wake, hii kesi inakwisha. Kuna watu wanatwishwa lawama ili serikali ichomoke.

Serikali haiwezi kuendelea kudhalilika namna hii. Urio ni mbuzi tu wa kafara tu. Hii ni aibu ya taifa
Isiishe tunamsubiri Sirro,Sabaya na Boaz
 
Natabiri bila Shaka kwamba baada ya ushahidi wake, hii kesi inakwisha. Kuna watu wanatwishwa lawama ili serikali ichomoke.

Serikali haiwezi kuendelea kudhalilika namna hii. Urio ni mbuzi tu wa kafara tu. Hii ni aibu ya taifa
Gaidi hawezi kuchomoka pale atakula mvua za kutosha

USSR
 
Bado mashahidi zaidi ya 12 wanakuja,subiri kidogo.

Bado wahudumu wa mahoteli mipango ilipokuwa ikipangwa.

Hiyo ya urio ni Primarily evidence....

Bado exhibition.....
 
Bado mashahidi zaidi ya 12 wanakuja,subiri kidogo.

Bado wahudumu wa mahoteli mipango ilipokuwa ikipangwa.

Hiyo ya urio ni Primarily evidence....

Bado exhibition.....
Kuthibitisha kula njama ni kazi sana, mpo wawili mnajadili yenu mhudumu wa hoteli atasema kweli mlikaa pamoja lakini hakusikia mlichokuwa mnajadili maana Urio anasema walikuwa wawili tu kwenye mazungumzo yao
 
Nyie mrukeruke ila kwa ushahidi wa upandewa mashtaka na weledi wa mawakili wa Mbowe- Mbowe ni mfungwa mtarajiwa
Hata magufulj alikua mfungwa mtarajiwa ndio maana akatunga sheria ya kutoshtakiwa akistaafu.
 
Hahaahaaa!Mahakama za mitandaoni kazi kweli kweli!
Una uhakika gani au unajua siri zipi za Liteni Urio hadi unakuwa na wasi wasi na mchecheto wote huo? Kwani wewe shida yako ni nini katika hiyo kesi?
 
Na kwanini Mbowe ahitaji ulinzi wa makomandoo na sio mabaunsa ambao hata yeye anaweza kuwapata maana zamani walikuwa watumishi wake akiwa na Bilicanas...
Katika hali ambapo nia ya Magufuli ilikuwa ni kuuangamiza upinzani na ikiwezekana kuwaua viongozi wake njia pekee ya akina Mbowe kujilinda ilikuwa ni hiyo ya kuajiri makomandoo kwani hawakuwa na namna. Magufuli akishakuwa "A Rabid Dog 🐶🐕" anang'ata hata mti.
 
Du kazi ipo, kudhibitisha ugaidi sikujua ni ngumu hivi. Ladba serikali iamue iwafunge tu hata kama hakuna ushahidi dhabiti utakao dhibitisha ugaidi.
 
Dennis Urio

Ni mwanajeshi,ni shahidi mwenye maslahi pande zote aliyetolewa kafara na waliomuamini baada ya kujikuta hawana kesi yenye mshiko.

Dennis Urio kama kweli aliota taarifa kwa DCI basi alistahili kwanza kuwekwa katika WITNESS PROTECTION YAANI alindwe kama shahidi.Denis URIO hakupaswa kuwa shahidi katika kesi kama hakuwa analindwa na kama alikuwa ni chambo.

Kwa mtazamo wangu ningewaona POLISI wana akili kama wangempa MBOWE Kanya BOYA mmoja ambaye angekuwa kwenye DEEP COVER kwa ajili ya kutafuta ushahidi na sio kumtumia DENIS na makomandoo wengine ambao hawakuwa na HATIA.

Dennis URIO ameonekana msaliti kwa MBOWE,Kwa Wanajeshi wenzake ambao walikuwa na maisha yao akawafanya chambo,Kwa marafiki zake, kwa watanzania na kwa CHADEMA. Kwa nini? Kwa sababu ya UZEMBE wa JESHI LA POLISI. UZEMBE wa KINGAI, UZEMBE wa DCI BOAZ.n.k.

Swali la kujiuliza ni JE DENIS URIO alifanya kosa kwenda kuripoti au waliokosea ni DCI na KINGAI kwa namna walivyoshughulikia jambo hili?Jambo kla UGAIDI sio PETTY CRIME lilihitajika kushughulikiwa na TAASISI zinazohusiana na USALAMA na kwa umakini mkubwa.

SASA Tunamuona Dennis kama msaliti na shujaa ambaye ametolewa kafara na upande wa Jamhuri.

Usitamani kuwa DENNIS ndio maana wakati mwingine watu wanakataa kuisaidia POLISI kwa sababu wanachojua POLISI ni kubambikia watu kesi, KUIBIA watu, KUUA watu na kukusanya rushwa.

Mungu Ibariki Tanzania
 
Polisi yetu hii ikienda kutipoti tukio zito usishangae wewe ndo ukawa mtuhumiwa namba moja wa hiyo kesi
 
Na kwanini Mbowe ahitaji ulinzi wa makomandoo na sio mabaunsa ambao hata yeye anaweza kuwapata maana zamani walikuwa watumishi wake akiwa na Bilicanas...
Rekebisha kwanza neno la Athali uliloliandika Kimakosa hapa na andika Neno sahihi la Athari sawa?
 
Back
Top Bottom