Shahidi ambaye alisubiriwa kwa hamu kubwa ili kuujua ukweli ni huyu Lut Denis Urio. Sasa Shahidi wake wote mpaka sasa unathibitisha kuwa hakuna mahali popote Mbowe na walinzi wake walipanga ugaidi. Hakuna picha, hakuna video, hakuna voice notes na hakuna hata sms kuthibitisha kuwa kweli walikutana na Mbowe kupanga ugaidi.

Amekiri kwa kinywa chake kuwa aliwatafuta wale makomandoo waliofukuzwa kazi wakafanye kazi ya Ulinzi na siyo uhalifu na kuwaomba kuwa kukiwa na uhalifu wamwambie kitu ambacho hakikutokea, amethibitisha kuwa walitumiwa nauli kwenda kufanya ulinzi na siyo uhalifu, akasema kua angewaambia kua wanaenda kufanya uhalifu wangekataa kwa sababu wana viapo, maana yake walipofika kwa Mbowe wakaacha viapo vyao wakakubali kufanya uhalifu bila kumjuza🤣🤣.

Kwa maana hiyo mpaka sasa kina Adamoo na wenzake ni Innocent maana hawakufanya uhalifu na wangekataa ikiwa kungekuwa na uhalifu, maana hata Lut Urio amekiri kwa mdomo wake kuwa wasingekuwa tayari kufanya uhalifu kwa sababu ya viapo vyao. Iweje leo waitwe magaidi? Asante sana Lut Urio imerahisisha kazi.

Hivi kweli DCI na timu yake wameambiwa kuna mipango ya ugaidi badala ya kumtuma Urio amrekodi Mbowe akimpa maelekezo ya kutekeleza ugaidi au ampige hata picha basi, yaani hadi wamtume akawashawishi kina Adamoo waende kwa Mbowe akiwadanganya ni ni kazi ya ulinzi kumbe ni ugaidi? Sasa kwa mantiki hii Polisi walizuia uhalifu au walichochea? Walishindwa nini kumkamata Mbowe kabla hata ya makomandoo hao kwenda Moshi?

Nasema asante sana Lut Urio kwa kuwasafisha Mbowe na wenzake. Sasa tumepata uelekeo wa kesi.

Eti Mama aombwe msamaha Gaidi Mbowe asamehewe, kwa lipi?
😂😂😂😂
Unafki wa ACT Wazalendo wabaki nao majumbani mwao.CHADEMA si wanafki kama wao. Siyo waoga kama ACT.
 
MaCHADEMA jipangeni kisaikolojia mnaenda kulia kama kwa Aqwilina
 
Me nadhani hii sio kesi ya ugaidi
Ni kesi ya uhalifu wa kawaida tu.
 
Serikali imekosa aibu kabisa!!
Bi Mkora hapa katia aibu mno, kosa la kipumbavu walilofanya ni kumkamata kwanza Mbowe kisha kuanza kutunga kesi...

Sasa jamii ikiona upuuzi huu wa serikali inaona kumbe unaweza kumfanyia unyama mtu yeyote!

Ndio maana tunasikia mauaji kila kona kila kukicha.
 
Umejaribu kufanya analysis, seems there is great reasoning. Katika law ukisema Fulani ameniaibisha kwa kuniambia hivi mbele za watu, mahakama inaangalia je, katika society unaumoishi, je utakuwa umeaibishwa kweli? Kwa wahaya, Uhayani kwenu ukimsema mtu kuwa hujatahiri ni aibu? HAPANA. Lakini mwambao wa pwani na Musoma Ni aibu kubwa na tusi kumwambia mtu hujatahiriwa.
Nije kwenye issue ya andiko lako. Kwa society ya watanzania, na maisha Yao nanyania zao, ukionekana unakata miti, unapanga magogo, kweli watu wataandamana? Watanzania watakuona unatishia Amani na kuwaweka hofu na hivyo kuandamana? A BIG NO!

KAMA Jaji siyo wa MCHANGO,na Samia Mtume Mohamed (SAS) amtelemkie aondoe kutumia màdaraka yake kuinfluence mahakama, hii kesi imeishia na Urio!
 
Na wasipomleta ndio wanaaribu zaidi kuhusiana na uwepo wa hii kesi. Nadhani ameamua kusimamia anachokijua, ngoja tuone.
 
Mahakama zetu zinatenda haki, mmeona kwa Sabaya? Chadema na wasio chadema wote tumeona haki imetendwa na mahakama.
Sasa hiyo hiyo mahakama itatenda haki kwa kesi ya ugaidi. Hakuna haja ya kuingilia wa kuipangia kwamba mbowe ni gaidi au siyo gaidi.
 
Amekuwa harmonies [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mmmh,,Hivi ni Kweli watu wanatii viapo vyao????Dhambi ni Mbaya saaana.Ndio Maana weusi kuendelea tutasubiri Sana Kwa sababu ya dhambi.
Hivi viapo ni siku ya graduation tu. Wakishatoka pale ni work as usual
 
Kubwa. Zaidi ni jinsi home boy alivyowaunga wale makomando wakafanye uhalifu haiingii akilini 😂😂😂😂mana yeye alipewa idea nakudai akatafuta watu wakafanye hiyo kazi sasa hao makomando kosa lao liko wapi? Na Kama asingewatafuta ina maana wasingekuwa na kosa lolote? Maswali ni mengi muda mchache ngoja tuone wataalamu wa sheria waje kufanya kazi yao ila kimsingi inamchafua mama kwenye juhudi zake njema zakukwamua taifa
 
Mi nahisi JWTZ wanaweza kuja kuzuia watu wasiingie mahakamani
 
Kumbe makomando wa watu wanaonewa sana walikuwa wanalima urio ndio akawadalalia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…