Aisee, kiukweli ushahidi wa kubumba wa mtu aliyekalishwa chini ili akaseme uongo kum - incriminate ndugu yake asiye na hatia ni rahisi mno kuugundua kwa sababu huwa unakosa uhalisia na siku zote huyu shahidi wa uongo hujisahau na hukosa consistency katika melezo yake....
Kwa mfano, huyu Denis Urio, kuna maelezo ya matendo yake mwenyewe au ya wale anaotaka wahukumiwe akiwemo Freeman Mbowe hayana uhalisia bali ni hisia zake tu na kwa namna yoyote hayathibitiki na mtu mwenye akili timamu hawezi kuàmini wala kufikiri kutendwa na mtu smart kichwani mwenye nia kutenda uovu mkubwà kama wa ugaidi...!
Najua (anaweza) kuendelea kumwaga pumba zake kesho...
Nakubaliana na wewe kuwa, kwa hakika kabisa, pengine huyu Denis Urio ndiye anayeweza kuwa shahidi wa hovyo zaidi wa upande wa mashtaka kuliko mashahidi wengine 11 wote waliotangulia anàyejaribu kuweka wazi (expose) udhaifu wa mashitaka haya...!!!
Ni afadhali hata Kingai au Mahita...!!
To cut it short, hii timu ya kubumba kesi hii ili kum - incriminate Ndg Freeman Mbowe wamefeli kwa kiwango cha juu sana maana hata mjinga kabisa aweza kujua ukweli huu mpaka hapa ilipofika...!!