Nina mashaka Luteni Urio anaenda kuharibu ushahidi dhidi ya Mbowe na wenzake 3. Fact hizi hapa
Naona hawa makomandoo wamefanyiwa entrapment, hawakua na mpango wa kukutana na Mbowe kabla hawajatafutwa na Urio. Na waliambiwa wanaenda kufanya kazi ya ulinzi isipokua Luteni anasema akawaambia wakiona matendo ya uhalifu wamrudie.

Well nafikiri ikifika stage ya kila mtu ashike mbao yake mawakili wa makomando watakua na kazi ya kuthibitisha entrapment.
 
1. Hakurekodi mazungumzo yoyote yeye na Mbowe ili kulifikishia Jeshi la Polisi kama ushahidi waweze kufanya upellelezi

2. Haku screenshot chats na call logs history za WhatsApp na Telegraph kuonesha kweli alikua anazungumza na Mbowe kupitia Apps hizo

3. Hakurekodi mazungumzo yake na vijana alio watafuta kuonesha kweli aliwatuma hizo kazi

4. Hakueleza popote kama alipewa kibali na Jeshi lake JWTZ kwenda kushiriki na Jeshi la Polisi kukamata magaidi

5. Kwakua alikua anajua Mbowe anataka kumsaidia kufanya ugaidi, hakutaka kukusanya ushahidi wa Dereva tax aliyempeleka, kufaham eneo walilokaa, muhudumu aliyewahudumia.

Je,

1. Pengine Lt. Urio na Mbowe walishindwana kwenye malipo baada ya kumtafutia vijana wa Kumlinda ndipo akamdanganya DCI kuwa vijana Wanaenda kufanya Ugaidi?

2. Pengine walikua na Ugomvi binafsi na vijana wake na kuamua kulidanganya jeshi la polisi?

3. Jeshi la polisi linawezaje kuchukua hatua za upelelezi kwa maelezo yalio elea ya LT. Urio bila uthibitisho wowote? Yani DCI analetewa tu umbea na Luten wa Jeshi, hajamwuliza rekodi za mazungumzo waliyo fanya na Mbowe, au chochote kinachoweza kuonesha kweli kuna njama za kufanya ugaidi?
 
Mimi nauliza swali moja tu.

Je bastola za akina Adamoo ni za halali?
...
Kwani hizo bastola ziko ngapi?
Na je mbona hayo madawa ya kulevya eti waliyokutwa nayo kwenye hati ya mashitaka hayapo kabisa, na yamekuja ibuliwa na mashahidi mahakamani?pesa waluzokutwa nazo ziliandikwa wapi?tuanzie hapo kwanza!!
 
Huyo home boy kwa mujibu wa washtakiwa katika utetezi wao wakati wa kesi ndogo ya kwanza nae alikula kichapo hapo TAZARA akawa analia kama nyau.
 
Habari za asubuhi waungwana,

Niseme wazi kwamba sina chuki na afande Urio lakini inashangaza kuona kesi mama (Kupanga kuua viongozi wa serikali na ugaidi) kwa ushahidi wake kwa nini tusiamini kuwa yeye ndo mratibu mkuu wa kesi husika.

Kwa nini alijua kuwa Mbowe anataka hawa vijana kwa ajili ya malengo maovu kwa nchi (kama ni kweli) na yeye alikuwa tayari kutoa mchango wake katika kutekeleza mpango huo haramu kwa nchi yetu.What if deal lingekuwa done na akina Ling'wenya wangefanikiwa kufanya jambo lao (japo nahisi wametengenezewa zengwe) bila kumpa taarifa yoyote kuhusu harakati zao?

Au ndo mchango wako afande umeutumia kutengeneza kesi ya mchongo?
Naomba wataalamu wa sheria mtuambie kwa nini afande Urio asiwe miongoni mwa watuhumiwa katika kesi hii?
 
Habari za asubuhi waungwana,
Niseme wazi kwamba sina chuki na afande Urio lakini inashangaza kuona kesi mama (Kupanga kuua viongozi wa serikali na ugaidi) kwa ushahidi wake kwa nini tusiamini kuwa yeye ndo mratibu mkuu wa kesi husika...
Urio ni mchaga hivyo anatumika na watawala iliionekane Mbowe anashitakiwa na wachaga kwa hiyo hakuna uonevu
 
Habari za asubuhi waungwana,
Niseme wazi kwamba sina chuki na afande Urio lakini inashangaza kuona kesi mama (Kupanga kuua viongozi wa serikali na ugaidi) kwa ushahidi wake kwa nini tusiamini kuwa yeye ndo mratibu mkuu wa kesi husika...
Au ndo mchango wako afande umeutumia kutengeneza kesi ya mchongo?

Naomba wataalamu wa sheria mtuambie kwa nini afande Urio asiwe miongoni mwa watuhumiwa katika kesi hii?
 
A shahidi ambaye alisubiriwa kwa hamu kubwa ili kuujua ukweli ni huyu Lut Denis Urio. Sasa Shahidi wake wote mpaka sasa unathibitisha kuwa hakuna mahali popote Mbowe na walinzi wake walipanga ugaidi...
Turudi RAU madukani a.k.a kwa Mama P.
Askari aliyefunzu, akaaminiwa hadi kupandishwa cheo kuwa ACP unakwenda kukamata watuhumiwa 3 unatuma Askari ukiwa umbali mfupi toka walipo anakurudishia jibu wako 3.

Wakati wa ukamataji unapata wawili unaondoka nao Hadi kituoni bila kazi yoyote hapo kituoni maana tungesema alikuwa anakwenda kuhifadhi watuhumiwa wale wawili labda! Lakini unaondoka nao tena kurudi kutafuta mtuhumiwa aliyekimbia saa 1 iliyopita eneo lilelile alipotorokea? Akili au tope?
 
A shahidi ambaye alisubiriwa kwa hamu kubwa ili kuujua ukweli ni huyu Lut Denis Urio. Sasa Shahidi wake wote mpaka sasa unathibitisha kuwa hakuna mahali popote Mbowe na walinzi wake walipanga ugaidi. Hakuna picha, hakuna video, hakuna voice notes na hakuna hata sms kuthibitisha kuwa kweli walikutana na Mbowe kupanga ugaid...
Acp Kingai alibase kwenye Hearsay za Lt Urio.
 
Anaondoka kwenye mashitaka haya kwa kigezo kimoja tu kwamba ali-riport kwa Kingai mapema kwamba Mbowe ana mpango wa kufanya UGAIDI, kufanya maandamano yasiyo ya ukomo, ukata magogo na kuyatandaza barabara kuu za Mbeya, Arusha, DSM na Dodoma - kwamba anatafuta maaskari makomandoo wa jeshi, pia anatafuta vifaa vilivyofungwa kwa mawasiliano ya Jeshi. Kingai akamwambia haya we endelea kuwasiliana naye na katika kila hatu uwe unanijulisha.

Huyu ndiye Captain Denis Urio - Mkufunzi wa Makomandoo.
 
Au ndo mchango wako afande umeutumia kutengeneza kesi ya mchongo?
Naomba wataalamu wa sheria mtuambie kwa nini afande Urio asiwe miongoni mwa watuhumiwa katika kesi hii?
Kaka Mshana, au na wewe ni snitch humu ndani maana kazi yako kubwa ni quoting of paraphrasing statements. Usitufanye tukuogope kaka, unajua watu wameanza kupotea? Wengi Instagram ba Facebook wanakamatishwa sana
 
Mimi nauliza swali moja tu.

Je bastola za akina Adamoo ni za halali...
Forensic Beaural watwambie inamilikiwa na Nani hakuna Silaha isiyo na umiliki.

Hawa jamaa waliwabambikia madawa na bastola wakidhani itakuwa ushahidi.
 
Back
Top Bottom