A shahidi ambaye alisubiriwa kwa hamu kubwa ili kuujua ukweli ni huyu Lut Denis Urio. Sasa Shahidi wake wote mpaka sasa unathibitisha kuwa hakuna mahali popote Mbowe na walinzi wake walipanga ugaidi. Hakuna picha, hakuna video, hakuna voice notes na hakuna hata sms kuthibitisha kuwa kweli walikutana na Mbowe kupanga ugaidi.
Amekiri kwa kinywa chake kuwa aliwatafuta wale makomandoo waliofukuzwa kazi wakafanye kazi ya Ulinzi na siyo uhalifu na kuwaomba kuwa kukiwa na uhalifu wamwambie kitu ambacho hakikutokea, amethibitisha kuwa walitumiwa nauli kwenda kufanya ulinzi na siyo uhalifu, akasema kua angewaambia kua wanaenda kufanya uhalifu wangekataa kwa sababu wana viapo, maana yake walipofika kwa Mbowe wakaacha viapo vyao wakakubali kufanya uhalifu bila kumjuza[emoji1787][emoji1787].
Kwa maana hiyo mpaka sasa kina Adamoo na wenzake ni innocent maana hawakufanya uhalifu na wangekataa ikiwa kungekuwa na uhalifu, maana hata Lut Urio amekiri kwa mdomo wake kuwa wasingekuwa tayari kufanya uhalifu kwa sababu ya viapo vyao. Iweje leo waitwe magaidi? Asante sana Lut Urio imerahisisha kazi.
Hivi kweli DCI na timu yake wameambiwa kuna mipango ya ugaidi badala ya kumtuma Urio amrekodi Mbowe akimpa maelekezo ya kutekeleza ugaidi au ampige hata picha basi, yaani hadi wamtume akawashawishi kina Adamoo waende kwa Mbowe akiwadanganya ni ni kazi ya ulinzi kumbe ni ugaidi? Sasa kwa mantiki hii Polisi walizuia uhalifu au walichochea? Walishindwa nini kumkamata Mbowe kabla hata ya makomandoo hao kwenda Moshi?
Nasema asante sana Lut Urio kwa kuwasafisha Mbowe na wenzake. Sasa tumepata uelekeo wa kesi.
Eti Mama aombwe msamaha Gaidi Mbowe asamehewe, kwa lipi?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Unafki wa ACT Wazalendo wabaki nao majumbani mwao.CHADEMA si wanafki kama wao. Siyo waoga kama ACT.