Nina mashaka Luteni Urio anaenda kuharibu ushahidi dhidi ya Mbowe na wenzake 3. Fact hizi hapa
Jana nilikuwepo Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi kuendelea kufuatilia kesi inayomkabili Mbowe na wenzake watatu. Leo sikuweza kwenda kwakuwa ninatarajia kusafiri hivi punde. Nimemsikia na kumuona Luteni Denis Urio akitoa ushahidi wake. Nimemsikiliza kwa makini na kwa kutaka kumuelewa. Ameeleza mengi kumhusu Mbowe na wenzake watatu walio mahakamani na mmoja ambaye hayuko mahakamani: Komando Lijenje.

Luteni Denis Urio, akitajwa na ACP Kingai na wengine, ndiye kiini cha kesi ya Mbowe. Ndiye mtoa-taarifa wa kwanza kuhusu njama za kutenda makosa ya jina: ugaidi na kudhuru viongozi wa kiserikali. Luteni Urio ndiye anayedai kupeleka taarifa za uhalifu wa kijinai kwa DCI na hata mengine kufuata baada ya hapo. Leo anaendelea kutoa ushahidi wake mahakamani. Mimi siusubiri ushahidi wa leo. Wa jana unanitosha na kunitisha.

Luteni Urio amepasua jipu namna alivyowatafuta na kuwapata makomandoo wanne:Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Lijenje. Kila mmoja alikuwa kwenye harakati zake za kimaisha. Harakati halali zisizo na dalali. Alikuwa kipambana kivyake ili kujikimu na kutunza familia yake. Huyu huku, huyu kule. Hii ni baada ya kuwakuta kilichowakuta jeshini (ukweli wanaujua wao wenyewe na Mungu wao).

Wakatafutwa. Wakataarifiwa kuwa kuna kazi ya ulinzi. Wakashawishiwa kuikubali. Wakakubali. Wakapewa na pesa ya kusafiria na kujikimu. Wakaenda mahali pa kupata kazi. Waliambiwa waseme kinachoendelea huko na wakawa wanasema ( mmoja alikuwepo Dar na akasema kinachoendelea). Kama vijana wenye nguvu na maarifa, waliambiwa kuhusu kazi. Wakaitamani na kuikubali kwakuwa kwao ulinzi ni jambo la kawaida. Wakaenda.

Walipokuwa huko walipoambiwa waende, wakavamiwa na kukamatwa kwa kutaka kutenda ugaidi na kudhuru viongozi. La haula! Hayo yalitokea wapi tena? Je, Luteni Denis Urio aliwatengenezea wenzake kesi labda kwa visasi vyao binafsi wakiwa jeshini? Je, iweje waliotafutwa na kuambiwa waende walikokwenda kwa kazi ya ulinzi waende halafu wakakamatwe hukohuko walikoambiwa waende? Hawa makomandoo watatu waliopo mahakamani na ambaye anatafutwa 'hawana kosa lolote'.

Nani angeacha kuifuata ajira ikiwa ana nguvu, maarifa, ujuzi na shida ya ajira husika? Wasibagazwe kwa harakati zao za kimaisha.

Wasiojulikana sasa wamejulikana!?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (safarini kwenda Dodoma)
 
MaCHADEMA jipangeni kisaikolojia mnaenda kulia kama kwa Aqwilina

Marehemu Akwilina alikuwa abiria tu ndani ya daladala, je, alikosa nini!? labda angekuwa dada yako pengine ungekuwa na akili.
 
Sasa mbona umezunguka sana si uende tu kwenye point

Mbowe sio gaidi ilo ndo linakufanya unazunguka ad unatukana watu waliokuzidi uwezo kiakil ata kifikla
 
Ukomandoo ni Kada muhimu Sana katika Jeshi na Ulinzi wa nchi. Ni Kada ambayo katika nchi za wenzetu mafunzo yake ni kitu cha Siri na cha kutukuka. Ni mafunzo ambayo Askari...
Komandoo anatakiwa kuwa na uwezo mkubwa wa kubalance nguvu na akili, lakini Urio ametutjibitishia amekuwa akifundisha matumizi ya nguvu asilimia 85 na akili asilimia 15.

Mbowe ni raia Kwa asilimia [emoji817] Urio kama Komando tena Mwalimu wa Walimu Hakuna mahali popote anapoonesha kuchangia chochote katika kuendesha Mpango hatari wa Mbowe wa kufanya ugaidi
 
Jana nilikuwepo Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi kuendelea kufuatilia kesi inayomkabili Mbowe na wenzake watatu...
Asante na safari njema, lakini ungesaidia kuwapata ndugu wa vijana hawa ili wamuulize Lt Urio kisa hasa cha kuwaharibia maisha ndugu zào huku akijua Wazi anawapeleka kwenye kifo.
 
Siwezi kuzidiwa akili na watumia nguvu kama wewe. Ndo maana unadhani lengo langu ni kumtetea Mbowe hapa. Kama ungekuwa na akili hata kidogo ungejua namaanisha nini? Mbona Wenye akili wameelewa?
 
majeshi yetu yote yajitathmini maana yanatumika vibaya kwa maslah ya wanasiasa.
 
Inawezekana kweli Mbowe kaonewa au hajaonewa, itajulikana mwishoni..."time is the best doctor"

Point zako nyingi ulizoandika hujafikiri kwa usahihi......either umefikiri kishabiki au umeshindwa kufikiri kiundani..
 
Na kwanini Mbowe ahitaji ulinzi wa makomandoo na sio mabaunsa ambao hata yeye anaweza kuwapata maana zamani walikuwa watumishi wake akiwa na Bilicanas...
Wasiojulikana hawakuanza miaka ishirini iliyopita.
 
Back
Top Bottom