Nina mashaka Luteni Urio anaenda kuharibu ushahidi dhidi ya Mbowe na wenzake 3. Fact hizi hapa
Anaondoka kwenye mashitaka haya kwa kigezo kimoja tu kwamba ali-riport kwa Kingai mapema kwamba Mbowe ana mpango wa kufanya UGAIDI, kufanya maandamano yasiyo ya ukomo, ukata magogo na kuyatandaza barabara kuu za Mbeya, Arusha, DSM na Dodoma - kwamba anatafuta maaskari makomandoo wa jeshi, pia anatafuta vifaa vilivyofungwa kwa mawasiliano ya Jeshi. Kingai akamwambia haya we endelea kuwasiliana naye na katika kila hatu uwe unanijulisha.

Huyu ndiye Captain Denis Urio - Mkufunzi wa Makomandoo.
Maswali ya Kibatala yatatoa uelekeo leo
 
Naona hawa makomandoo wamefanyiwa entrapment, hawakua na mpango wa kukutana na Mbowe kabla hawajatafutwa na Urio. Na waliambiwa wanaenda kufanya kazi ya ulinzi isipokua Luteni anasema akawaambia wakiona matendo ya uhalifu wamrudie.

Well nafikiri ikifika stage ya kila mtu ashike mbao yake mawakili wa makomando watakua na kazi ya kuthibitisha entrapment.
Kama hao makomandoo hawakumrudia Urio maana yake kulikuwa hakuna uhalifu.. maana bado wapo chini ya kiapo cha utii
 
Shahidi bado yupo mahakamani, ngoja amalize...
 
Habari za asubuhi waungwana,
Niseme wazi kwamba sina chuki na afande Urio lakini inashangaza kuona kesi mama (Kupanga kuua viongozi wa serikali na ugaidi) kwa ushahidi wake kwa nini tusiamini kuwa yeye ndo mratibu mkuu wa kesi husika...
Lt ndiye engineer wa ugaidi
 
Anaondoka kwenye mashitaka haya kwa kigezo kimoja tu kwamba ali-riport kwa Kingai mapema kwamba Mbowe ana mpango wa kufanya UGAIDI, kufanya maandamano yasiyo ya ukomo, ukata magogo na kuyatandaza barabara kuu za Mbeya, Arusha, DSM na Dodoma - kwamba anatafuta maaskari makomandoo wa jeshi, pia anatafuta vifaa vilivyofungwa kwa mawasiliano ya Jeshi. Kingai akamwambia haya we endelea kuwasiliana naye na katika kila hatu uwe unanijulisha.

Huyu ndiye Captain Denis Urio - Mkufunzi wa Makomandoo.
Kapanda cheo leo ama? Maana Jana alijitambilisha kama luten
 
leo ndiyo utamu wenyewe, mbivu na mbichi zitajulikana leo na kesho - tunaomba shahidi asipate tumbo ya kuendesha tu hapo kizimbani ikawa taabu kwa mahamama.
 
A shahidi ambaye alisubiriwa kwa hamu kubwa ili kuujua ukweli ni huyu Lut Denis Urio. Sasa Shahidi wake wote mpaka sasa unathibitisha kuwa hakuna mahali popote Mbowe na walinzi wake walipanga ugaidi...
Umemaliza.. kulikuwa hakuna ugaidi ndo maana hawakumrudia
 
Take note

1. Anasema aliwasiliana na DCI kuwa Kuna watu wanataka kufanya ugaidi.

Yeye ni kiongozi wa platoon, utaratibu unaelekeza kuwa taarifa zote unazotilia shaka usizipeleke URAIANI, zinatakiwa zipelekwe kitengo Cha usalama jeshini ambacho ndicho chenye jukumu la kufanyia kazi taarifa zote.

Je, ilikuwaje yeye apeleke taarifa URAIANI?
Je, viongozi wake wa 92KJ/Mgulani walitaarifiwa?
Je, number ya DCI aliitoa wapi?
Je, kuna kiongozi wa ngazi yake aliyewahi kumshirikisha na hivyo kupata ushauri Ili apeleke suala la kijeshi URAIANI?

2. Anasema watuhumiwa walifukuzwa kwa utovu wa nidham lkn reference zake zote alizipata kwa admin officer

Je, ndio utaratibu wa kijeshi?

Kama sio utaratibu wa kijeshi aseme ni utaratibu Gani wa kupata taarifa jeshini

Mimi sio mwanasheria

Lakini huyo ni mtuhumiwa mwenzao na hao makomando wengine ila yeye amepewa rushwa either ya kuendelea kubaki kazini Ili atoe ushahidi wa UONGO.

Kosa la kukubali kuwaunganisha wenzake na uhalifu ni kosa kubwa sana. Yeye anatakiwa kuzuia uharifu kabla ya kumtokea.

Inawezekanaje yeye ajue uharibifu utatokea then aruhusu akitegemea nini?

Pia kitendo cha yeye kufanya mawasiliano hayo tu tayari ni KUJIHUSISHA NA SIASA kosa ambalo linamuachisha moja kwa moja na jeshi.

Yaani kifupi

Ushahidi wa URIO umefeli sana/ ni zero

Haya ni matokeo ya elimu. Je, ana elimu Gani na akakubali kulishwa utumbo hivyo?

Lieutenant/ luten kafeli sana.
 
Na kwanini Mbowe ahitaji ulinzi wa makomandoo na sio mabaunsa ambao hata yeye anaweza kuwapata maana zamani walikuwa watumishi .wake akiwa na bilicanas...
Kwa stage iliyofikia ya dikteta Magufuli na hasa majaribio ya Mbowe kuuawa ilibidi atafute ulinzi madhubuti zaidi,na Urio ndie aliemshauri achukue makomandoo.

Hao mabaunsa waendelee tu kuwalinda akina Diamond,komandoo ni level tofauti sana
 
Hivi viapo ni siku ya graduation tu. Wakishatoka pale ni work as usual
Hata ikulu wanaapa, kesho ndio vinara wa kuikanyaga katiba. Hakuna utawala wa kisheria, tuna jamhuri ya kambale, mkubwa kumla mdogo, japo wote tuna sharubu.
 
Kweli kabs hawa makomandoo wamechezewa sinema na Luten urio bila kujijua,hv ikatokea wakashinda kesho huyo urio ataachwa salama kweli na hao wanafunzi wake ?
Hata hao makomandoo waliobaki kikosini unafikiri wanamuangaliaaje sasaivi?
 
Kwa stage iliyofikia ya dikteta Magufuli na hasa majaribio ya Mbowe kuuawa ilibidi atafute ulinzi madhubuti zaidi,na Urio ndie aliemshauri achukue makomandoo.

Hao mabaunsa waendelee tu kuwalinda akina Diamond,komandoo ni level tofauti sana
Na inawezekana baada ya kuona akina Bwire ni kikwazo ndipo wakaamua kuwabambikia kesi ya ugaidi.

Niliwahi msikia jamaa mmoja ana laani Bwire kuwa mlinzi wa Mbowe.

Kifupi Bwire alikuwa tishio kwa wote waliokuwa wanataka kumdhuru Mbowe.
 
Back
Top Bottom