Shahidi wa 12, Luteni Urio, au kwa kukusudia au kwa kulazimika, leo amewathibitishia wote kuwa Mbowe alikuwa anahitaji walinzi. Tena kwenye mawasiliano ya Telegram, Mbowe alitamka wazi kuwa kati ya hao watatu, wawili watakuwa full time na yeye:
Wakili wa Serikali: Shahidi Soma Meseji inayofuata
Shahidi: Hao wawili Kwa kuanzia Siyo Mbaya, Hawawezi Kutekelezwa, Wanakuwa na Mimi Full time, Wamekwambia Wanataka nini.?
Wakili wa Serikali: Meseji hii ilikuwa Imetoka Kwa nani
Shahidi: Imetoka Kwa Freeman Aikael Mbowe
Wakili wa Serikali: Neno hawa Wawili Kuanzia Siyo Mbaya ni akina nani hao
Shahidi: Ni Khalfani Bwire na Moses Lijenje
Kwa vyovyote vile, hao wawili kama wangekuwa full time na Mbowe, huo ugaidi wangekuwa wanamfanyia Mbowe? Hiyo miti ya kukata na kuziba barabara ipo kwenye mgongo wa Mbowe? Hivyo visima vya mafuta vya kilipua vitakuwa vipo tumboni mwa Mbowe?
Au tuseme, wakati hawa wanamlinda Mbowe, huyo mmoja aliyebakia ndiye angekuwa anakata na kupanga magogo kwenye barabara zote za Tanzania? Huyo mmoja angekuwa anaruka kwa jet kwenda kulipua vituo vya mafuta kwenye mikoa saba iloyotajwa?
Katiba ni muhimu. Katiba itatusaidia kuwapata viongozi wenye uwezo, dhamira njema, wakweli wa nafsi, na ambao wakikengeuka, tutaweza kuwafurumsha bila mizengwe. Katiba mpya itaangalia ni namna gani tutaweza kuwa na jeshi la polisi lenye weledi, idara ya ujasusi yenye weledi, mahakama iliyo huru na yenye majaji wenye weledi.
Kwa sasa, nchi ipo kwenye giza nene.