Nina mashaka Luteni Urio anaenda kuharibu ushahidi dhidi ya Mbowe na wenzake 3. Fact hizi hapa
Hadi sasa nasubiri kusikia ni wakati gani Jeshi la Polisi liliishirikisha Idara ya Ujasusi ya Tanzania baada ya kusikia kuna uhalifu mkubwa unaoratibiwa na unahatarisha amani ya nchi na pengine uRais wa nchi...
Hata kama walishirikishwa lakini haiwezi kusemwa. Vyombo vya kijasusi havizungumziwi hivyo. Na kwa tukio sensitive hivyo ni dhahiri VIlishirikishwa, Si ajabu hata lilianzia huko kabla ya kupelekwa kwa DCI
 
Simtetei Mbowe wala Jamhuri, naongelea content zako..

Makomando wanne sio lazima waende wao front na kutekeleza hayo...bali makomado wanne wanaweza kutoa mbinu, kufundisha na kupanga mipango madhubuti pamoja na kufanya recruitment.

Lazima ujue Komando ni mtu gani then wawe wanne.....uwepo wao kwenye mipango hatarishi tayari ni jambo la hatari.

Nimejaribu kuwaza kwenye hiyo mistari yako na kupingana na fikra zako....Kesi ya Mbowe ibake suala la mahakama, mawakili, majudge nk "Time is the best doctor"
 
technically, Urio kainunu kesi ya mbowe tena kwa bei ya chee kabisaa, kwani amekubali kuwa yeye ndiye 'whistle brower' wa hii kesi na yeye ndiye aliye waingiza hao makomandoo kwenye matatizo bila wao kujua na mengine mengi tuu tutayasikia leo……….
 
1. Wakati akitoa ushahidi wake wote Mara kadhaa wakili aliyemuongoza alisita kuendelea kumuuliza na kuanza kuteta chini kwa chini ikionesha Kuna majibu Alitoa nje ya matarajio yao...
Kesi ikiisha namtafta Urio anitafutie makomandoo wa kuwa mabaunsa wangu binafsi, maana nyumbani kwangu namamsap hakutawaliki!
 
Hivi ndivyo huwa mnadanganywa kwenye vikumbi vyenu vya sinema za kutafsiriwa kwa maneno ya Kiswahili..
Usimdhihaki. Alichokisema ni sahihi kabisa. Tatizo lenu mnafikiri uaskari ni kupigana ngumi ndio maana unawaza how possible for 1 Vs 100!!. Katika hali ya kawaida tu hata Komando mmoja anaweza kuthibitiwa na watu watano.

Alichomaanisha Huyo mdau ni ktk Operation na huyu komando anaweza kuwamaliza hao adui pasipo hata kutumia ngumi au mapigano ya mwili. Ni kwa ujuzi na mbinu tu. Pia anaweza kumaliza watu wengi kwa mikono silently lakini ambao wapo scattered not as organized group.


Sijui umepata Concept.
 
1. Wakati akitoa ushahidi wake wote Mara kadhaa wakili aliyemuongoza alisita kuendelea kumuuliza na kuanza kuteta chini kwa chini ikionesha Kuna majibu Alitoa nje ya matarajio yao...
Na bado hajazungumzia ni jinsi gani aliwashirikisha mabosi wake huko jeshini juu ya jambo kubwa Hilo la ugaidi.
 
Jambazi mkubwa huyu.

alikuwa anataka kulihujumu hadi jeshi letu, dhamira yake ilikuwa ni ovu dhidi ya Serikali, huyu jambazi/gaidi aliachiwa sana....alipaswa adhibitiwe mapema maana alifikia pabaya sana.

anakenua kenua kinafiki.

ashughulikiwe bila huruma ili iwe fundisho kwake na kwa vibaraka wote alio kuwa anawatumia kufanikisha uhalifu.
 
Komando mmoja ni sawa na wanajeshi wa kawaida 100,sasa komandoo wanne sini sawa na wanajeshi 400?.
Komandoo 4 ( sawa na wanajeshi 400) waasi wanaweza kupambana na kuwashinda komandoo 100 (sawa na wanajeshi 10000) walio waaminifu/ watiifu kwa serikali?
 
Swali la msingi kwangu, je baada ya watekelezaji wa mipango yq ugaidi kukamatwa bila ya kumkamata mfadhili...je walikua na uhakika Kama mfadhili atashindwa na mipango.
Na Kwa mujibu wa Urio,hawa makomandoo walipelekwa Kwa mbowe kimtego tu ili baadae Mbowe akamatike,sasa mbona walikamatwa makomandoo kabla hata hawajaanza kuainisha miti ya kukata.
 
Usimdhihaki. Alichokisema ni sahihi kabisa. Tatizo lenu mnafikiri uaskari ni kupigana ngumi ndio maana unawaza how possible for 1 Vs 100!!. Katika hali ya kawaida tu hata Komando mmoja anaweza kuthibitiwa na watu watano...
Uzi wako uko sahihi lakini una uhalisia? Unaloandika ni sahihi tu kwa Komando mwenye Intelligence Quotient na Emotional Quotient kubwa. Umebaini kitu hapo? Tuna Watanzania wangapi wa aina hiyo?

Hata kama wapo, nani hapa Bongo mwenye uelewa na dhamira ya kuwahitaji? Inahitaji mipango endelevu kuanzia kwenye aina ya elimu na uzito staki kwenye msingi huo!
 
Shahidi wa 12, Luteni Urio, au kwa kukusudia au kwa kulazimika, leo amewathibitishia wote kuwa Mbowe alikuwa anahitaji walinzi. Tena kwenye mawasiliano ya Telegram, Mbowe alitamka wazi kuwa kati ya hao watatu, wawili watakuwa full time na yeye:

Wakili wa Serikali: Shahidi Soma Meseji inayofuata

Shahidi: Hao wawili Kwa kuanzia Siyo Mbaya, Hawawezi Kutekelezwa, Wanakuwa na Mimi Full time, Wamekwambia Wanataka nini.?

Wakili wa Serikali: Meseji hii ilikuwa Imetoka Kwa nani

Shahidi: Imetoka Kwa Freeman Aikael Mbowe

Wakili wa Serikali: Neno hawa Wawili Kuanzia Siyo Mbaya ni akina nani hao

Shahidi: Ni Khalfani Bwire na Moses Lijenje

Kwa vyovyote vile, hao wawili kama wangekuwa full time na Mbowe, huo ugaidi wangekuwa wanamfanyia Mbowe? Hiyo miti ya kukata na kuziba barabara ipo kwenye mgongo wa Mbowe? Hivyo visima vya mafuta vya kilipua vitakuwa vipo tumboni mwa Mbowe?

Au tuseme, wakati hawa wanamlinda Mbowe, huyo mmoja aliyebakia ndiye angekuwa anakata na kupanga magogo kwenye barabara zote za Tanzania? Huyo mmoja angekuwa anaruka kwa jet kwenda kulipua vituo vya mafuta kwenye mikoa saba iloyotajwa?

Katiba ni muhimu. Katiba itatusaidia kuwapata viongozi wenye uwezo, dhamira njema, wakweli wa nafsi, na ambao wakikengeuka, tutaweza kuwafurumsha bila mizengwe. Katiba mpya itaangalia ni namna gani tutaweza kuwa na jeshi la polisi lenye weledi, idara ya ujasusi yenye weledi, mahakama iliyo huru na yenye majaji wenye weledi.

Kwa sasa, nchi ipo kwenye giza nene.
 
Shahidi wa 12, Luteni Urio, au kwa kukusudia au kwa kulazimika, leo amewathibitishia wote kuwa Mbowe alikuwa anahitaji walinzi. Tena kwenye mawasiliano ya Telegram, Mbowe alitamka wazi kuwa kati ya hao watatu, wawili watakuwa full time na yeye...
Timu gaidi tulieni dawa iwaigie
 
Na kwanini Mbowe ahitaji ulinzi wa makomandoo na sio mabaunsa ambao hata yeye anaweza kuwapata maana zamani walikuwa watumishi wake akiwa na Bilicanas?

Je, hao makomandoo wangefanya kazi zipi kwake ambazo zingekuwa mpya tofauti na maisha yake ya siasa zaidi ya miaka ishirini?

Je, wajua komandoo mmoja anaweza kuwa na athali kubwa kwa nchi ambayo raia wengi hawana uelewa wowote wa kivita?
Kumbuka urio alisema kati ya hao makomandoo wawili wangekaa na mbowe full time, yaani wako na mbowe muda wote sasa ugaidi wangefanyaje au mbowe angegeuka komandoo wasaidiane kukata miti na kulipua vituo vya mafuta kwa amri ya kikosi command , mbowe.
 
Back
Top Bottom