Nina mashaka na ujauzito wa mpenzi wangu

Adanganye utrasound ??

Report itoke, Jina la hospitali, Jina la client, Findings & conclusions adanganye? Huyo atakua shetani
 
Ultrasound hutumika kupima umri wa ujauzito kwa kuzingatia ukubwa wa mtoto aliyeko tumboni, na kwa kawaida huwa ni sahihi kwa kiwango kikubwa, hasa katika hatua za mwanzo za ujauzito. Lakini, matokeo ya ultrasound pia yanaweza kutofautiana kidogo kulingana na hali mbalimbali kama vile mzunguko wa hedhi wa mwanamke, na wakati alipotunga mimba.

Kwa kawaida, ultrasound inaweza kuwa na tofauti ya hadi wiki moja au mbili, lakini tofauti ya wiki mbili na zaidi ni nadra. Kwa hiyo, ikiwa ultrasound inaonesha kuwa ujauzito ni wa wiki 5 na siku 2, na ulitarajia uwe wa wiki 3 au chini ya wiki 4, kuna uwezekano mkubwa kuwa wakati wa kutunga mimba ulitokea kabla ya ulivyofikiria.

Ikiwa una shaka juu ya uhalali wa ujauzito huo kuwa wako, unaweza kumshauri mwenzi wako apate kipimo cha DNA cha kubaini uhalali wa baba wa mtoto mara baada ya mtoto kuzaliwa. Hata hivyo, ni muhimu kuzungumza naye kwa uwazi na kwa upole kuhusu hisia zako na wasiwasi ulionao.
 
Inawezekana kitaalam tunaita "cronoenkymosyin" ni aina ya mimba ambayo inapatikana pale tu mbegu ya mchepuko ikiingia siku kadhaa kabla ya mimba ya mume na mara nyingi mume anakuwa kama kachanganyikiwa na kuanza kuuliza maswali kama haya ambayo kitaalamu hayawezani.
 
Nasbukuru sana kwa ushaur wako wa hekima
 
Wewe kakupa cheo cha heshma cha "social father " maisha yaendelee.
 
imekuaje ultrasound isome mimba ni wiki 5 nasku 2?
Ukienda hospital Wana muuliza dada mara ya mwisho kuingia period ni lini?halafu ndo Wana calculate na tarehe ya hiyo siku aliyoenda kupima ndiyo maana unaona mimba inasoma hivyo tofauti nawewe ulivyotarajia,hawahesabu tarehe mliyo-kutana
Sijui umenielewa...😊hujabambikiziwa
 
Thank you nmeelewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…