Nina maswali mengi juu ya mashetani aliokuwa akipandisha mama yangu mzazi

Nina maswali mengi juu ya mashetani aliokuwa akipandisha mama yangu mzazi

Blaszczykowski

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2022
Posts
339
Reaction score
1,164
Hello wapendwa, kama kichwa cha Habari kinavyo jieleza apo juu. kipindi nilivyokuwa mdogo miaka 7 niliona kwa macho yangu bi mkubwa akipandisha mashetani na kuongea lugha ambayo nilishindwa kuielewa (kiarabu) alieweza kuongea nae alikuwa mama mkubwa na yeye lazima apandishe mashetani ndio waweze kuelewana vizuri.

Kuna siku Moja alipandisha shetani la kizungu na Kwanza kuongea kingereza kabisa pure shida ilikuja akuna aliekuwa anajua anachozungumza kutokana Familia zetu akuna aliekuwa anajua kingereza ili kumtuliza wanampa glass mbili za pombe kali baada ya dk 15 Hali Inatulia na kuendelea na kazi zake za nyumbani (haonekani akinuka pombe wala kulewa) hiyo Hali ilitokea Mara chache sana .
ILA

Nilivyofikisha miaka 30 bi mkubwa akaniltetea mdogo wangu wakike tukawa wawili tu. Tokea kipindi icho bi mkubwa akuwahi pandisha mashetani yoyote Yale

Sasa nishakuwa mkubwa najitambua nataka nijaribu niongee na Hao mashetani walikuwa na siri gani walitaka nini katika Familia yetu sana sana yule shetani aliekuwa anaongea kingereza nijue alitaka nini alitokea wapi na kwanini amekuwa kimya zaidi ya miaka
23

Sijui mama atalichukuliaje hili swala sijui atanijibu Nini nataka apandishe nipate majibu kablasijaondoka apa duniani ..
 
Imagine ulikuwa miezi 9 tumboni mkipishana kwenye mihangahiko wewe na shetani.
Shetani anajua lugha zote, hata mwanadamu anajua lugha zote uki unlock greatness iliyoko ndani yako mpaka kiitaliano utaongea bila kufundishwa na yeyote.
You are bigger than devils
 
Mkuu Blaszczykowski pole sana kwa bi mkubwa wako ila nasikitika kukuambia kuwa bi mkubwa anasumbuliwq na changamoto ya afya ya akili ambayo ni maradhi.

Huenda akawa na Dissociative Identity Disorder(DID) au Multiple Personality Disorder au aina ingine ya changamoto ya afya ya akili inayohusiana na identity yake.

Kama upo Dar hapa hospitali ya Taifa Muhimbili Kuna wataalamu wazuri mpeleke bi mkubwa atasaidiwa.
 
Hayo madude yapo kabisa ila yana ukakasi ,kuna mazingira unayatengenezea ..Nimeongea nayo sana na pia karibia mara zote ni wanawake .
Ukiona yanamfuata mtu basi kayaandalia mazingira ila upo uhusiano kwa mbali na magonjwa ya akili hasa stress.
 
Hello wapendwa .kama kichwa cha Habari kinavyo jieleza apo juu .kipindi nilivyokuwa mdogo miaka 7 niliona kwa macho yangu bi mkubwa akipandisha mashetani na kuongea lugha ambayo nilishindw kuielewa (kiarabu ) alieweza kuongea nae alikuwa mama mkubwa na yeye lazima apandishe mashetani ndio waweze kuelewana vizuri .Kuna siku Moja alipandisha shetani la kizungu na Kwanza kuongea kingereza kabisa pure shida ilikuja akuna aliekuwa anajua anachozungumza kutokana Familia zetu akuna aliekuwa anajua kingereza ili kumtuliza wanampa glass mbili za pombe kali baada ya dk 15 Hali Inatulia na kuendelea na kazi zake za nyumbani (haonekani akinuka pombe wala kulewa ) hiyo Hali ilitokea Mara chache sana .
ILA
Nilivyofikisha miaka 30 bi mkubwa akaniltetea mdogo wangu wakike tukawa wawili tu
Tokea kipindi icho bi mkubwa akuwahi pandisha mashetani yoyote Yale

Sasa nishakuwa mkubwa najitambua nataka nijaribu niongee na Hao mashetani walikuwa na siri gani walitaka nini katika Familia yetu sana sana yule shetani aliekuwa anaongea kingereza nijue alitaka nini alitokea wapi na kwanini amekuwa kimya zaidi ya miaka
23

Sijui mama atalichukuliaje hili swala sijui atanijibu Nini nataka apandishe nipate majibu kablasijaondoka apa duniani ..
Unathibitishaje ni mashetani na si kitu kingine chochote ambacho labda hujakielewa vizuri tu?
 
Mkuu achana na hayo mambo, utaingia ktk imani za kishirikina ukiamua kuyafatilia. Wanaosema mama anasumbuliwa na matatizo ya akili hawajui wanayosema.

So far, mama atakuwa na nguvu kubwa sana za giza endapo kama hakuwahi kuombewa ili kutolewa hayo majini.

Mshukuru Mungu kwa kuwa wewe ni mzima, jikite zaidi ktk kumtumainia Mungu na kumpendeza. Angalia usije ukaidumbukiza familia yako wewe mwenyewe ktk imani za kishetani wakati kuna neema ya Mungu imekufunika wewe kuwa mbali na mambo hayo.
 
Ulikuwa na miaka 7 hakuna aliyekuwa anajua kiingereza kwenu lakini ulijua aliongea kiingereza? Tena umesema kiingereza pure ulijuaje ni kiingereza?
Hata hakuongea kiingereza unahisi tu kilikuwa kiingereza kwasababu ya umri wako wakati huo na hakuna yeyote aliyekuwa anajua chochote kwenu wakati huo.

Huyu mama yako alikuwa mlevi tu, alibuni njia ya kupata pombe za bure, naamini angeomba pesa akiwa mzima ili anunue pombe asingepewa, ila kwasababu aliipata kila alipojitia uchizi, basi akawa kila akipata hamu ya pombe ana jitia uchizi anapewa pombe kali anatulia.
 
Back
Top Bottom