Nina Mgogoro kwenye ndoa, kila pesa anayopata Mke wangu anaenda kujenga kwao. Naomba msaada

kilichobaki uspokua makini watu wataskuma kete mbele ile kwako mazima.
 
Kama hamna mtoto wa kiume wazazi wafe? Nyi ndo mnawafanya wazazi wajute kuzaa watoto wa kike
 
Tafuta pesa zako ndugu, acha KUTOLEA MACHO pesa ya mwanamke utakufa kwa magonjwa yasiyoambukiza. Sawa sawa?
 
hii inaweza kuwa sawa kama marejesho hayata adhiri Afya ya familia yako
 
Tafuta hela.
We unaumia na 20M aliyokopa serikalini, si na wewe ukakope benki au kwingineko ili kuwatengezea future watoto wenu?
Kumbuka, pesa zake ni zake. Pesa zako ni zenu.
Wanaume wengi wameaminishwa huu ujinga kwamba pesa ya mwanamke ni ya mwanamke, mwanamke atafute pesa ila mwanaume udhibiti hizo pesa, yeye kutumia pesa aliyoingiza yeye inatakiwa ruhusa aipate kutoka kwako, hiyo ndio ndoa.
 
Anakiuka yale maagano ya ndoa, imeandikwa kuna siku utaachana na wazazi na kuambatana na umpendae ili kuanzisha familia yako. Ni jukumu lako kujenga hiyo familia uliyoanzisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…