Advanced PCB yamoto Sana ila watu hawawezi wakakupa maelezo ya uhalisia haswa huo ugumu upo wapi mpka uende kwanza ukajaribu hata miezi 4 tu, then uone mwenyew, me ingawa nilifaulu, Ila ni kwa mbinde sana...na ufaulu wenyewe 1.7 niliapply doctor of medicine, vyuo vyote vimenitema mpaka SUZA ya Zanzibar, niliapply vyuo vya serikali vyote vitatu, na vya private vitano, nikaja kupata chuo dirisha la mwisho, chuo chenyewe Kampala, ambapo Ada ya udaktati ni 7.2M kwa mwaka,ndio nipo hapo mpk leo maisha yanaenda hivohivo.. na mkopo wenyewe Sikupata 🙂.....
Nakushauri tu kwa hayo matokeo yako ya form4, na jinsi ulikaa miaka 10 nje ya shule, na unataka upige advanced PCB kwa mwaka mmoja, NENDA DIPLOMA.
Hata ukisoma advance kwa miaka minne bado hutotoboa kupata div1.3-6