Nina miaka 30 na mshahara wangu ni 250k je nitaweza kutoboa?

Mpe mtaji mh mbunge hata mil 5 tu..nyie ni watu wakubwa hapa nchini.
mtaji anao tayari huyo gentleman.

mtaji wa kwanza ni dhamira, lakini pia ana lengo na ana mipango.

hapa jukwaani,
amekuja kuomba wadau wa JF wamsaidie mbinu za kutoboa maisha kulingana na kipato chake cha msingi na kulingana na mazingira aliyopo.

huyo muungwana yupo makini sana kichwani na anahitaji muongozo tu wa kutoboa maisha na sio pesa za kupewa na mtu bali kazi za mikono yake 🐒
 
Wakuu na wasilimu sana !
Bila ya kupoteza muda mimi ni mwalimu wa shule moja ya private huku kijijini ndani ndani na muhitimu wa shahada ya ualimu masomo ya arts(Sanaa).

Lengo la uzi huu kwa wanajamvi ni kuwa uliza hivi kweli kwa kipato hiki cha laki 250,000 ntaweza kutoboa kimaisha kweli? ikumbukwe mimi ni wa kiume sina kiwanja wala nyumba.

Kama ijulikanavyo fainali uzeeni naona kabisa fainali yangu sasa imefika naombeni ushauri wa kina kabisa.

Wenu katika ujenzi wa taifa
Sakwe
Mkuu, una miaka 30 na degree ya chuo kikuu, lakini unalipwa mshahara unaolingana na hela ya mboga ya wiki moja ya houseboy wa mjini.

Halafu bado unajiita mwanaume unayetafuta 'fainali'?

Ukweli ni kwamba kwa hiyo laki 2.5, utazeeka hapo kijijini ukiwa huna hata tofali moja la kwako la urithi.

Hapo hufundishi ili utoboe, unajitolea kuwa mtumwa ili ufe maskini wa kutupwa.
Hama hapo haraka la sivyo hiyo degree yako itakufunika sanda ukiwa hai.
funganya virago vyako ondoka, la sivyo jiandae kuwa masikini wa kupigiwa mfano
 
Naam nimekuelewa vizuri mkuu,japo natamani kubadilisha fani ila nawaza ni fani gani hiyo itanifaa japo najua pia biashara sio kwa ajili ya kila mtu

Jikite katika business hiyo mindset yako itakuchelewesha sana.

Kwa Sasa hakuna fani inalipa acha kusikiliza motivation speakers.

Huo ualimu unatosha jikite kujifunza soft skills na ku-run business .

Maana hata ukijifunza fani ya kupaka rangi , mpaka uje uaminiwe na kupata kazi za maana ujue itakuchukua muda pia sio overnight game.

So kama hauna patient na strategies ni hatari.
 
Mkuu, una miaka 30 na degree ya chuo kikuu, lakini unalipwa mshahara unaolingana na hela ya mboga ya wiki moja ya houseboy wa mjini.

Halafu bado unajiita mwanaume unayetafuta 'fainali'?

Ukweli ni kwamba kwa hiyo laki 2.5, utazeeka hapo kijijini ukiwa huna hata tofali moja la kwako la urithi.

Hapo hufundishi ili utoboe, unajitolea kuwa mtumwa ili ufe maskini wa kutupwa.
Hama hapo haraka la sivyo hiyo degree yako itakufunika sanda ukiwa hai.
funganya virago vyako ondoka, la sivyo jiandae kuwa masikini wa kupigiwa mfano
Duuh hii dawa ni yenyewe mkuu japo chungu ila ime ningia mkuu narudia japo ni chungu ila imeningia vizuri
 
Jitahidi ufanye biashara

Fanya saving , then fungua biashara hata ya duka la mangi .

Mambo yatakaa sawa.
Huo ushauri wa kitoto unakupoteza. Hiyo hela haitoshi hata kununua mifuko miwili ya sukari, wewe usevu duka? Kataa ujinga huo, hiyo hela ni ya kukutoa hapo kijijini, siyo ya kufungua biashara za kufikirika.
 
Jikite katika business hiyo mindset yako itakuchelewesha sana.

Kwa Sasa hakuna fani inalipa acha kusikiliza motivation speakers.

Huo ualimu unatosha jikite kujifunza soft skills na ku-run business .

Maana hata ukijifunza fani ya kupaka rangi , mpaka uje uaminiwe na kupata kazi za maana ujue itakuchukua muda pia sio overnight game.

So kama hauna patient na strategies ni hatari.
Naam nami nazidi kujifunza mengi kutoka kwako mkuu
 
Mshahara wangu kwa mwaka mzima bila kugusa hata senti moja ni milioni 3, hapo tunazungumzia muda wote uko shule ni asubuhi mpka jioni na malipo ni tarehe 30 na baadhi ya miezi huvuka bila kupewa chochote
Ndiyo maana nimekwambia kwa kazi hiyo na mshahara huo hata ufanye nini huwezi kutoboaaaa

Jaribu kurudi nyuma ubadilishe njiaa
 
Duuh hii dawa ni yenyewe mkuu japo chungu ila ime ningia mkuu narudia japo ni chungu ila imeningia vizuri
Mkuu, kama dawa imekuingia na kuamsha akili yako, hatua ya kwanza kabisa ni kufunganya virago na kuondoka hapo kijijini. Ukibaki hapo kusubiri miujiza, unajidanganya; hakuna fursa mpya inayoota kwenye ardhi ileile iliyokufubaza.

Matajiri wengi walianza kwa riski ya kuhama mazingira magumu. Toka hapo kijijini, nenda mkoani au mji mkubwa (kama Morogoro, Dar, au kwingineko) ambako elimu yako ya Degree ina thamani.
Hata kama utaanza kwa kupanga chumba kimoja, heshima ya akili yako itakuwa kubwa na milango ya fursa, tuition za maana, na connection mpya itafunguka.

Usiogope kuanza upya mjini ogopa kuzeekea kijijini ukiwa mtumwa wa laki 2.5. Chapa lapa sasa hivi, nenda kachakarike kiume
 
Kipato huendana na matumizi. Hicho kipato unachokiona kidogo kuna watu wanatamani wangekuwa wao. Jijenge kidogokidogo, wekeza, nunua kuku peleka kijijini,nunua mbuzi baada ya muda utakuwa na mbuzi na kuku wengi wauze anza biashara yako binafsi.
 
Mkuu, kama dawa imekuingia na kuamsha akili yako, hatua ya kwanza kabisa ni kufunganya virago na kuondoka hapo kijijini. Ukibaki hapo kusubiri miujiza, unajidanganya; hakuna fursa mpya inayoota kwenye ardhi ileile iliyokufubaza.

Matajiri wengi walianza kwa riski ya kuhama mazingira magumu. Toka hapo kijijini, nenda mkoani au mji mkubwa (kama Morogoro, Dar, au kwingineko) ambako elimu yako ya Degree ina thamani.
Hata kama utaanza kwa kupanga chumba kimoja, heshima ya akili yako itakuwa kubwa na milango ya fursa, tuition za maana, na connection mpya itafunguka.

Usiogope kuanza upya mjini ogopa kuzeekea kijijini ukiwa mtumwa wa laki 2.5. Chapa lapa sasa hivi, nenda kachakarike kiume
Huu ni mkakati wa kuhakikisha ki vyovyote singii kwenye Kanzidata ya TASAF
 
Mkuu, kama dawa imekuingia na kuamsha akili yako, hatua ya kwanza kabisa ni kufunganya virago na kuondoka hapo kijijini. Ukibaki hapo kusubiri miujiza, unajidanganya; hakuna fursa mpya inayoota kwenye ardhi ileile iliyokufubaza.

Matajiri wengi walianza kwa riski ya kuhama mazingira magumu. Toka hapo kijijini, nenda mkoani au mji mkubwa (kama Morogoro, Dar, au kwingineko) ambako elimu yako ya Degree ina thamani.
Hata kama utaanza kwa kupanga chumba kimoja, heshima ya akili yako itakuwa kubwa na milango ya fursa, tuition za maana, na connection mpya itafunguka.

Usiogope kuanza upya mjini ogopa kuzeekea kijijini ukiwa mtumwa wa laki 2.5. Chapa lapa sasa hivi, nenda kachakarike kiume
wewe si umeandika uzi jana unatafuta mganga? Unampa ushauri gani sasa wakati wewe ni mshirikina baharia 1
 
Mganga anatafutwa na watu wenye pesa zao wanaotaka kulinda 'mambo makubwa'. Kwenye laki 2.5 hata mganga mwenyewe anajua hapo kuna njaa, hawezi kupoteza muda wake. Shusha mistari ya maana, kupekua maisha yangu hakubadili ukweli kwamba laki 2.5 ni hela ya mboga.
 
Back
Top Bottom