Option nzuri ya kuepuka ujira (maana huu sio mshahara) wa hand to mouth ni kutumia ujira huo kuukimbia, sio kuutunza.
Kulazimisha mtu ale majani ya maboga na matembele mwaka mzima haitamfanya afanye savings ya maana kwa 250,000 ya kabla ya matumizi. Ni afadhari
Sakwe uchukue mshahara mmoja mazima mazima uende nao hapo kijijini ununue kuku wa kienyeji na kwenda kuuza mjini.
1. Epuka kudunduliza huo mshahara, hapo utakata roho. Labda utunze mishahara maximum mitatu tu!
2. Epuka ushauri wa sijui ufungue genge mara duka la rejareja. Hiyo akiba haitoshi kuweka chanja za kwenye fremu, kodi na mzigo wa kuuza dukani. Fanya kuhamisha bidhaa tu, mtaji wote uwe ni kununua na kusafirisha isiwe kutunza ndani kusubiri kucheka na wanakijiji ndio wanunue na wakope.
3. Akiba huwa inataka uwe na hela ya matumizi, savings ni extra ya hela unayopata ukitoa matumizi ya lazima. Wewe hata matumizi ya lazima huna, unaenda save nini? Mwishowe ukipata msiba, ugonjwa, simu kuharibika utajikuta any solution inakula 50% to 150% ya savings na madeni juu.
Wewe tafuta biashara kama kuku ambapo unanunua labda kuku wa kienyeji wa 200k watakuwa kama kuku 18 maybe, nenda mjini ongeza kama 3k kwa kila kuku uza jumla kwa wachinjaji au tafuta ufanye supply kwa wapishi wakubwa kama migahawa na hoteli.
Kwa siku ukipata hata net profit 15k ya kwako kumbuka unauza jumla hela ndogo hivyo unamaliza mzigo. Kwa mwezi ukiuza hata mara 15 unapata faida ya 225,000.
Ukifanya reinvestment ya faida kila mwezi na unazidi kupata wateja na bei inapanda kidogo. Baada ya mwaka unakuwa na supply ya kwenda mbali kidogo na faida inaonekana. Hiyo ni njia practical na ya muda mfupi kuliko kuutunza huo mshahara huku unashindia uji.