Nina miaka 30 na mshahara wangu ni 250k je nitaweza kutoboa?

Punguza matumizi yasiyo ya lazima and save utatoboa. Nakumbuka kazi yangu ya kwa kuajiriwa kwa mhindi mambo ya hadware nilikuwa nalipwa 46k/month nikajifunza kusave na kumuibia kama kawaida nikatoboa kias coz nilmpga tukio la cement 50 mara mbili tukagawana na mimi nikapata cement sitin na tuliyepga na deal akapata 40. Mabati nilikua nahamisha kama takataka hadi wa leo hakujua na alishafilisika.
 
Uko sahihi mkuu malengo na ndoto zangu ni kubwa mnoo ila naona kwa kibarua hiki tena huku kijijini malengo yangu haya makubwa na talanta zilizobarikiwa zitaishia kwenye bomba

Miaka 30 sio Mdogo tena.
Ni kijana ambaye tayari unatakiwa umeshajua na kufanya uamuzi wa maisha kwamba duniani utafanya nini kukupeleka kwenye ndoto zako.
Then miaka 10 mpaka 15 yaani hapo utakuwa na miaka 45 utakuwa umefikia angalau robo tatu ya safari
 
Njoo mjini tufungue mikeka…
Ukiweka odds 25 za kumi kumi unaiongeza inafika millioni…
 
Uko sahihi mkuu
 
Mkuu Sakwe , kwenye mazingira hayo weka mkazo mwenye kilimo angalau kwa miaka miwili kabla hujaingia kwenye biashara.
Kutoboa ni hatua, ukiweka malengo utatoboa tu.
 
Utatoboa lakini lazima uwe na mipango ya muda mfupi na ya muda mrefu.
 
Binafsi naona Laki 2 na nusu sio kubwa ila ukiwa na utulivu wa akili na mwili ni ela unayoweza kukusukuma upige hatua kimaisha.

Kwanza kabisa apo mm nitaweka pembeni matumizi yasiyo ya lazima mfano kunywa, sijui Tv sijui nguo maana sihitaji kununua nguo kila mwaka.

Afu nitaanza kuweka akiba walau laki moja kila mwezi kwa mwaka nitakua na Milion moja na laki 2..

Milion Moja na Laki 2 naacha kazi nafungua Kigenge Duka mtaani... Nitakipanua kigenge duka changu naweka vijipombe n.k ndani ya mwaka unaofata nikiendesha vizur biashara nitatengeneza zaidi ya Milion 3... Nitatafuta Shamba nitalimaa, nitaweka mifugo ya Ngombe, mbuzi, kuku n.k ndani ya Mwaka unaofata naweza tengeneza Milion 5 -10, kufikia miaka 35 nitanunua shamba la Milion 1 nitaanza ujenzi, afu kufikia apo naanza kuwaza makubwa zaidi nitaongeza wigo wa duka na mashamba ya kulima kufikia miaka 40 nitakua natengeneza walau Milion 3 kwa mwezi.

Ukibaki kwenye iyo ajira mshahara ukiongezeka sana hautafika milion.
 
Reactions: Nus
Mkuu Sakwe , kwenye mazingira hayo weka mkazo mwenye kilimo angalau kwa miaka miwili kabla hujaingia kwenye biashara.
Kutoboa ni hatua, ukiweka malengo utatoboa tu.
Nashukuru sana kwa ushauri kamanda
 
Bushmamy kipi kinakusikitisha hapo. Mtu analipwa million tano kwa mwezi na akipata gepu la kuiba mil2 anaiba au ulitaka nijifanye yesu.
 
Bushmamy kipi kinakusikitisha hapo. Mtu analipwa million tano kwa mwezi na akipata gepu la kuiba mil2 anaiba au ulitaka nijifanye yesu.
Ulifanya vibaya, unaona Sasa Hadi muhindi wa watu kafilisika😞.
 
Hutoboi.
 
Jitahidi ufanye biashara

Fanya saving , then fungua biashara hata ya duka la mangi .

Mambo yatakaa sawa.
Ukipewa huo mshahara kila mwezi kwa miaka 10. Tukirudi hapa tutakuta umechanika matakoni hata elfu hamsini huna. Mnaandika vitu haviwezekani.
 
Kwa situation ya sasa is very tough hapo na hizo shule zinavyowabana saa 1 hadi saa 10/11 ila you have a way

Hakikisha una save balance VZR unaanza kufanya biashara ndogo ndogo, Achan na mahusiano hasa ambayo ni tegemezi kiuchumi
Hawezi fanya saving ya maana. Akifanya saving mwaka mzima anajikuta na laki tano na hapo hii simu anayotumia hapa inadondoka kwenye maji.
 
Ngumu mkuu, hapo lazima kichwa chako kidanye kazi 100× ya uwezo wako na ujitume zaidi mkuu.
Kila kitu kinawezekana chini ya jua
 
Ndiyo mkuu nipe elimu
Option nzuri ya kuepuka ujira (maana huu sio mshahara) wa hand to mouth ni kutumia ujira huo kuukimbia, sio kuutunza.

Kulazimisha mtu ale majani ya maboga na matembele mwaka mzima haitamfanya afanye savings ya maana kwa 250,000 ya kabla ya matumizi. Ni afadhari Sakwe uchukue mshahara mmoja mazima mazima uende nao hapo kijijini ununue kuku wa kienyeji na kwenda kuuza mjini.

1. Epuka kudunduliza huo mshahara, hapo utakata roho. Labda utunze mishahara maximum mitatu tu!
2. Epuka ushauri wa sijui ufungue genge mara duka la rejareja. Hiyo akiba haitoshi kuweka chanja za kwenye fremu, kodi na mzigo wa kuuza dukani. Fanya kuhamisha bidhaa tu, mtaji wote uwe ni kununua na kusafirisha isiwe kutunza ndani kusubiri kucheka na wanakijiji ndio wanunue na wakope.
3. Akiba huwa inataka uwe na hela ya matumizi, savings ni extra ya hela unayopata ukitoa matumizi ya lazima. Wewe hata matumizi ya lazima huna, unaenda save nini? Mwishowe ukipata msiba, ugonjwa, simu kuharibika utajikuta any solution inakula 50% to 150% ya savings na madeni juu.

Wewe tafuta biashara kama kuku ambapo unanunua labda kuku wa kienyeji wa 200k watakuwa kama kuku 18 maybe, nenda mjini ongeza kama 3k kwa kila kuku uza jumla kwa wachinjaji au tafuta ufanye supply kwa wapishi wakubwa kama migahawa na hoteli.
Kwa siku ukipata hata net profit 15k ya kwako kumbuka unauza jumla hela ndogo hivyo unamaliza mzigo. Kwa mwezi ukiuza hata mara 15 unapata faida ya 225,000.

Ukifanya reinvestment ya faida kila mwezi na unazidi kupata wateja na bei inapanda kidogo. Baada ya mwaka unakuwa na supply ya kwenda mbali kidogo na faida inaonekana. Hiyo ni njia practical na ya muda mfupi kuliko kuutunza huo mshahara huku unashindia uji.
 
Nenda na ile formula ya spend less save more

Ukiweza kujibana ukapata 1m ukatafuta sehemu nzuri center ukafungua genge (sio duka la mangi) genge kama genge ila classy
Unauhakika wakulaza 10k faida na uwezekano wakuongezeka ni mkubwa sana

Muhimu tu umuone Mshana mapema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…