Nina milion 10 nahitaji kujenga nyumba Mwanza

Wiring nimebananishadogo nansomesha veta umeme aliifanya bure.
 
Kuna mtu humu aliwahi kushare hii picha natafuta sipati uzi wake na mhusika mwenyewe
 
Huu uzi unaniletea simanzi sana niko site nimeshachoma kama 23m mpaka kupaua tu. Na hapo nimesimamia kila kitu asubuhi mpaka usiku na hardware nakwenda mwenyewe.
Mkuu mambo ya Ujenzi acha,mtu kama hajajenga ndio ataongea Vitu asivyojua. Mimi nilimuomba Mtu wa Mchoro anichoree Ramani ya nyumba ya milion 30,kuanza ujenzi mpaka nyumba inaisha nimetumia milioni 70+. Nimefanya ule ujenzi nikiwa mbali,watu wanasema nimeibiwa lakini siri naijua mie.
 
kama ulikuwa mbali usikatae huko kuibiwa.
 
Kama uko mbali na site kuibiwa kupo mkuu.

Yawezekana 20+ imepigwa au zaidi hali ni mbaya sana mafundi na hata watu wengine siyo waaminifu hapo unakuta wameiba material na hela.
 
Kama uko mbali na site kuibiwa kupo mkuu.

Yawezekana 20+ imepigwa au zaidi hali ni mbaya sana mafundi na hata watu wengine siyo waaminifu hapo unakuta wameiba material na hela.
Inawezekana,lakini hela sio rahisi kuiba,nilifanya manunuzi mwenyewe ya kila kitu. Dunia imekuwa kijiji,fundi alikuwa akinipa mahitaji ya Rangi nawasiliana na mafundi wengine wanipe makadirio yao,mara nyingi yalikuwa yanacheza mule mule,nikijiridhisha naweka oda kiwandani mzigo ukiwa tayari unaenda Site. Nimefanya hivyo kwa kila kitu,kuanzia Bati,tiles,Vifaa vya umeme,vifaa vya mabomba, Aluminium n.k...
Nilitaka kuleta uzi humu kuwaambia watu Dunia imekuwa kijiji sa hivi,mfano tiles fundi alinipa vipimo vyake,nikatuma kwa jamaa yangu Engineer akasema viko sawa,Ishu ilikuwa kwenye bei,nilitafuta namba za Twyford kwenye website,nikawapigia wakanipa namba za wakala wao aliye jirani na site,nikaweka oda kisha nikamwambia fundi akakague,akasema ziko sawa,mzigo ukaenda Site. Nimefanya hivyo kwa kila kitu.Kitu pekee ambacho nahisi kupigwa ni cement na Tofali...maana walikuwa wanatoka nje ya hesabu wanazonipa wanaomba nyongeza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…