Nina milioni 100 naombeni wazo la biashara

Nina milioni 100 naombeni wazo la biashara

nime kuelewa boss wangu. kuna jamaa kaniambia biashara ya bar haina faida
Sijuwi wewe boss wangu una experience na hiyo biashara?
Biashara ya bar ni wachache wanaopata faida na hata hao wanaopata faida inakuwa sio ya kudumu.
Sababu ni kwamba biashara ya bar inakwenda kwa kutegemea umaarufu na promotions za mara kwa mara.
Kwa mfano ukianzisha bar kwa miezi 6 au 12 ya mwanzo ukifanya promotions utawaona wateja wengi wanakuja na utavimba kichwa,lakini ikitokea mwingine kaanzisha bar mpya walevi wote wanakuhama na kwenda chimbo jipya unabaki peke yako
 
Siku hizi nimeishiwa idea za kibiashara kabisa. Kwangu biashara uzaliwa palipo na huitaji. Pasipo huitaji huduma au bidhaa itakubidi utumiw nguvu nyingi kuuza.

Neno langu. Palipo na hatari ndipo palipo na fursa/ uwezekano.

Kwa dar watu wako na capital wako teyari ku compete sokoni so kumbuka kuchagua sahihi.
Dar ni pagumu sana aisee.
Kuna Madon wako na mitaji mirefu imekaa standby kwenye akaunti zao.
Ukianzisha biashara wakaona unauza sana wanakwenda kuchukua mzigo mara 5 ya mzigo wako kisha wanashusha bei lazima uporomoke.
 
Uwakala mkuu wa mitandao ya simu. Airtel Na vodacom. Hii kwa hela yako mnakuwa wawili na pikipiki mbili kazi yenu ni kuweka flot bank na kuwasambazia mawakala mtaani cash na flot. Hii mkiwa serious inalipa sanaaaa na wala haina stress. Na mkishajulikana kwa mawakala mnapiga kazi kilaini sanaaa......

Mnaanza kazi asubuhi saa 1 mpaka saa 12 jioni...... Mda huu bado unakuwa ni muda mzuriiii kwa usalama wenu na pesa zenu.

Ila hii biashara uzuri wake ununui bidhaa kusema biashara ikikushinda basi utakuwa umepoteza pesa zako au utaanza kumtafuta mtu umuuzie bidhaa kwa bei ya hasara HAPANA!! Biashara ikikushinda pesa yako inakuwa ipo palepale. Kama utakuwa hauna cash basi utakuwa nayo kama flot kwenye simu zako za kazi.

Jaribu hii na wala usikimbilie biashara zenye faida kubwaa kwa misimu ambazo hazina uhakika wa kukuingizia faida mfululizo ndani ya miaka miwili mbele......

Ila hii biashara ukishatengeneza soko ndani ya miezi yako mitatu...... Kinachobakia nikufanya kazi kwa uhakika na faida ya uhakika kila mwezi.

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
Hii biashara masharti yao yakoje mkuu,na ni mtaji kiasi gani unahitajika
 
Tenga mil 12 nenda uturuki,Dubai na china huku ukiwa na notebook yako ukirudi utakuwa na idea nyingi unique utachagua mwenyewe.


Ndivyo nilivyopata Idea yangu inayoniingizia faida mil 100+ kwa mwaka.

Safari njema
 
Anzisha ZAHANATI mkuu.,
Kupitia hela yako hyo unaweza kuanzisha ZAHANATI kwa mtaji wa 50ml. Zahanat ya kisasa kabisa.Miezi mitano tu ushazoeleka ambapo utakua na uwezo wa kukusanya 15milion.Ukilipa wafanyakaz unabakiwa zako na 10mil.

Project anzisha kampuni ya clearing...Tafuta connection ujue sehem ya kupeleka mzigo wako.Mathalani Ngozi ya ng'ombe inanunulika sana uarabuni huko...
Hz ni biashara ambazo kwa mtaji ulio nao huchelewi kurudisha hela yako kwa mda mfup
Vifaa vyote vya zahanati vinagharimu kiasi gani mkuu
 
Back
Top Bottom