Nina milioni 100 naombeni wazo la biashara

nime kuelewa boss wangu. kuna jamaa kaniambia biashara ya bar haina faida
Sijuwi wewe boss wangu una experience na hiyo biashara?
Biashara ya bar ni wachache wanaopata faida na hata hao wanaopata faida inakuwa sio ya kudumu.
Sababu ni kwamba biashara ya bar inakwenda kwa kutegemea umaarufu na promotions za mara kwa mara.
Kwa mfano ukianzisha bar kwa miezi 6 au 12 ya mwanzo ukifanya promotions utawaona wateja wengi wanakuja na utavimba kichwa,lakini ikitokea mwingine kaanzisha bar mpya walevi wote wanakuhama na kwenda chimbo jipya unabaki peke yako
 
Dar ni pagumu sana aisee.
Kuna Madon wako na mitaji mirefu imekaa standby kwenye akaunti zao.
Ukianzisha biashara wakaona unauza sana wanakwenda kuchukua mzigo mara 5 ya mzigo wako kisha wanashusha bei lazima uporomoke.
 
Hii biashara masharti yao yakoje mkuu,na ni mtaji kiasi gani unahitajika
 
Tenga mil 12 nenda uturuki,Dubai na china huku ukiwa na notebook yako ukirudi utakuwa na idea nyingi unique utachagua mwenyewe.


Ndivyo nilivyopata Idea yangu inayoniingizia faida mil 100+ kwa mwaka.

Safari njema
 
Vifaa vyote vya zahanati vinagharimu kiasi gani mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…