Nina milioni 20. Nahitaji kufanya biashara ya spare za pikipiki kwa jumla na rejareja


Mkuu wangu... Asante sana mkuu, hapa nimekuelewa kabisa mkuu! Kuhusu huo uzi unaoelezea biashara ya china huwezi ku paste link mkuu? Maana nduo njia rahisi yakuupata.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hiyo ndio moja ya nilichokisema akili ya kujua mambo au kigeni public relation ushirikiano na ushawishi ukimudu hill baishara ushindwi.
Nilisema ukienda na 20m lazimavuweke 10m nyingine mahali kusubiri majanga.
Majanga ya biashara ni bei na ushuru.....contingencies
Pampana mafanikio ni ari, Bidii na kutokata tamaa.
 
Pesa ndogo sana nafanya kazi hiyo mbaka sasa nipo kwenye gemu miaka 15 pesa hiyo uza rejareja tu hata hivo hata reja2 bado pesa haitoshi lakini utaenda mdogo mdogo
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pesa ndogo sana nafanya kazi hiyo mbaka sasa nipo kwenye gemu miaka 15 pesa hiyo uza rejareja tu hata hivo hata reja2 bado pesa haitoshi lakini utaenda mdogo mdogo

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu kwenye kuhusu bajeti kutosha inategemea unataka kuchukua spare aina gani.Kwani kama ukichukua rims bei ni kubwa so mzigo utakuwa mdogo.spare za pikipiki ni nyingi sana labda kama ujikite kwenye baadhi ya spare tu kama utataka kuuza kwa jumla kwa pesa hiyo.

Pia ukichukua mzigo china ujipatie siku 30+ ndo mzigo wako ufike.Kuhusu usafirishaji haina shida makampuni ni mengi sana sasa hivi.ila kwenye bajeti kama umeminya sana maana pana kula,kulala,usafiri,vocha,atleast pigia bajeti yako kwa worst situation ili usije ukajikuta unaishiwa hadi nauli ya kwenda aieport

Halafu ni unatakiwa uwe ukizijua spare geniune ama grade nzuri,otherwise wachina watakupiga sana especially kama wakijua nimgeni ama ndo unaanza.

China spare za pikipiki utazipata guangzhou soko linaitwa baiyun motorcycyle spare parts.kila la heri boss
 
Wazo hili ni wazo bora kwa maoni yangu ambalo ndio nilipanga kulitoa kwake.
Kuna mtu namjua anafanya hii biashara mda mrefu na anaduka kariakoo lakini huwa afati mzigo China pekee yake huwa wanachanga na wafanyabiashara wezake then ndio wanaenda kuchukua mziko mkubwa mixer wa pamoja, Sasa wewe ndio unaaza unataka uundee China.....????

Kama ushawai kufanya bishara ya nguo utakuwa shaidi hapa mfano unataka kununua mzigo wa mashati ,ambao Kwa jumla wanakubali kuuza piece 50 kwa kila Aina ya shirt sasa hapo utalazimika kununua jeupe piece 50,njano 50,blue 50,red 50 ukicheza unaweza kuta pesa yote imekwisha kwa mashirt tu, ambayo ni mengi na ngumu kumaliza mzigo mapema sasa baadae yatageuka uchafu kwasbb utanunua mzigo mkubwa usiokuwa na maana, lakini mfano mkichanga wafanyabiashara watano (5)
Piece 50/5=10

mkanunua mzigo kwa pamoja inamaana kila mmoja wenu atapata piece 10 kwa kila aina ya shirt na rangi kwa gharama ndogo na ni mzigo unaweza kuuzika na kuisha mapema hapo napo utabakiwa na pesa ambayo unaweza kunua bidhaa nyingine.

Sijui sana kuhusu spare za pikipiki lakini ngoja nikupe mfano ukienda China huko usidhani utanunua piece 10/20/30 mfano umenda na list yako lakini unafika kule wanakwambia minimum order ya tyre la pikipiki ni piece 1000 jumla unakuta labda ni milioni 5 , minimum order ya starter ni pice 50 bei 1M ngoja nishie hapa 🤔 lakini natamani unielewe kuwa unaweza kwenda china ukarudi na mzigo mkubwa lakini aina ya spare ni chache..Umebeba mzigo mkubwa lakini ni vitu vinavyojirudia
 
Mkuu,umeeleza jambo zuri sana na la muhimu katika biashara.Kuwa na taarifa sahihi kwa wakati sahihi na kujua namna ya kuzishinda hizo changamoto katika biashara.Hivyo basi kwa mtoa uzi nafikiri sasa ana jua kwamba ni lazima aanzishe uhusiano na watu wa Kariako il apate mtu ambaye wanaweza agiza mzigo pamoja na pia inabidi atafute taarifa za bei ni kiasi cha order pamoja na taarifa nyingine muhimu.Asisahau kwamba INAWEZEKANA ikiwa anayo nia ya kweli ya KUFANIKIWA mradi ajue tu lengo lake kuu ni lipi.
 
Una ushari mzuri kwa muhitaji.
Huwezi kumwambia mtu 20m kwa ajili ya spare za piki piki ni peanuts vifaa vinavyouzwa $0.02 a piece? Engine block $5.0 ambayo ina uzwa hapa laki +? Biashara is determination and skill Huyu amekwisha determine amepata mtaji wa 20m ambao ni mkubwa to scale, wapo watu ukimpa 500,000/= Leo ukimwona baada ya mwaka mmoja unamwita mzee!
 

Mm niko kariakoo nafanya biashara import kutoka china
Ushaur: Husiende china kufanya biashara yoyote kama hujawai fanya iyo biashara hata mwaka moja kwa kuchukua mzingo hapa hapa bongo coz hutakuwa na experience ya iyo biashara utapoteza ela yako kama upepo
Mm naona anza kwa hapa bongo kwa iyo ela yako then ukipata experience ndio uende China

Watu wanaenda na ela nyingi sana china tena izo biashara ya spare za pikipiki ni 40ft ndio wanaoata faida bt loose cargo hakuna ela utapoteza ela yako mkuu cha kabisa
Kuna biashara wapo matajir wengi huwezi fanya na mtaji wa million 100 kwenda chini. Vitenge, spare za pikipiki,viatu nk

Kama utapata ela basi ya soda tu kutoboa huwezi coz wanaobeba 40ft wanaweka bei chini sana ww wa loose cargo huwezi pata faida mkuu lamda kipindi cha kikwete ulikuwa unaweza pata faida coz mzunguko ni mkubwa nw mzunguko ni mdogo utachoma ela yako tu

Kwenda china malazi viza nauli lazima 4m ikate hapo bado uo mzingo hujanunua
Sasa utapata faida kiasi gani hapo mkuu ?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona unamlipia mwanao 5M ya ada? Huoni unamtajirisha mwenye shule?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo ni kweli, unapotaka kuvuka mto ingiza mguu mmoja kwanza ukiona kina kinavukika tumbukiza mguu wa piki uvuke.
Hyu aanze na biashara ya hapa hapa akisikia utamu wa greese basi aende huko Guangzhou akakombe hiyo miko alete awagawie walaji.
Asante kwa ushauri wako mzuri.
 
Wengine ni wafanyabiashara wa bidhaa hiyo wanakutisha ilihali wanaogopa ushindani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimesoma comment nyingi za kukatisha tamaa ml 20 ni kubwa mnoo wastani wa kununua mzigo China ml 10 ukifanya biashara yoyote ya kuleta Tanzania achana na wenye roho za korosho nafaida inakuwaga x 3 ya manunuzi

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23] mkuu unakosea. Nani kakuambia hayo yote? Unataka kufanya boashara kkoo ya spare kwa million 20? Kodi ya frem kkoo waijua? Nauli ya china go and return? Accomodations? Meals? Nani anaenda mzururisha? Mtafsiri? Huo mzigo ananunua kwa hela ipi hapo? Hivi mnachukulia poa mtu kuwa hapa kkoo ama. Ushuru wa bandarini? Leseni za biashara etc? Mil 20 kwa china ni peanut money kwa mtu anayetaka soko la kkoo. Ni hasara kiujumla.
 
yes upo sahii mkuu.Alfu ukiingia sokoni ka stage eyo ya rejareja unaweza kulisoma soko la spare kiundani na kujua changamoto zake vizuri mno.Unajua changamoto unazitatutaje zikija na kwa wakt unauza rejareja unaanza kutengeneza good customer basee ambayo hata ukifunga mzigo wa jumla unaulaaa piaaa.

The key ni kwamba waweza ukawa na Duka la jumla ambalo hio duka unaprint ezo parts kwa jina lako ,au unabrand zile boksi za kufungia spea ikiwa kama njia ya kujitanganzaaaa,na pia unakuwa na duka huku una ka workshop ambacho kataenda sambamba na unachokitoa sokoni......
 

Biashara pekee yenye return ya uakika ni Real Estate upande wa property tu.

I can assure you mwaka jana nimeanza na Tsh M10 nimenunua shamba two accers nimeplan viwanja 36 @ M1.5 kwa hesabu za kawaida tu utaona faida ipo wapi?

Now nipo kwenye process ya kufanya usajili wa kampuni official.

Hili game ni tamu no stress za kuangaika what you need ni advertising tu
Kama unahitaji somo karibu officen

0692275216

 
Mungu akutangulieee kwakila jambooo Hongeraaa
 
Hongera office nzuri... tufafanulie hapa hapa mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…