Premij canoon
JF-Expert Member
- May 27, 2018
- 1,203
- 2,771
- Thread starter
- #41
Mkuu kwanza nikupe hongera kwa kuweza kutengeneza kiasi hicho cha pesa japokuwa hujasema kwa sasa unafanya nini,mim nikushauri tu kwamba kama alivyoshauri hapo juu ni kwamba biashara sio hela tu ni zaidi ya pesa na wataalam wa biashara wanasema ujuzi wa biashara ndio mtaji mkubwa zaid kuliko pesa hivyo anza kwanza kupata ujuzi kabla ya kufikiria kwenda china kwani hii ni kutaka kuanzia juu wakat biashara huwa inaanzia chini.
Ni kweli biashara ya spare za pikipiki zinalipa kwa sasa hivi sema hii corona virus imekuwa ni tatizo na bado hatujui itaisha lini. Kama alivyoshauri mkuu mmoja hapo juu chukua kiasi kidogo kama 5m fungua duka la reja reja fanya kazi kupitia hilo utajua aina za pikipiki na spare zake na zile ambazo mahitaji ya spare zake yapo juu kuliko zingine na utawajua wauzaji wa jumla kwa kariakoo sasa kadri utakavyokuwa unafnya utazidi kupata ujuzi na taarifa muhimu zaidi kuhusu hii biashara na kitafika kipindi utajiona tu sasa unatosha kwenda china na hapo taarifa nyingi utakuwa nazo.
Nasisitiza tena ukianza biashara bila ujuzi yaani "Technical know how " utapoteza pesa yote na hutafikia lengo ndio kuna mkuu moja amekuambia hiyo pesa ni peanut ni kweli ukiwaza kwenda kufunga container na 20m ni peanut lakin ukiwaza kwa upande wa pili ni pesa nyingi. Kuna mkuu mmoja aliwahi kuleta uzi mmoja humu kuhusu biashara ya China na Tanzania ule uzi una vitu vingi sana kuhusu safari, clearing , TRA na vinginevyo vingi tu utafute usome ukiwa umetulia utajifunza mambo mengi kuhusu biashara ya China na Tanzania nafikiri mkuu alotuma huo uzi anaitwa kipilipili utafute usome ukiwa umetulia.
Mwisho nikutakie kila la kheri.
Mkuu wangu... Asante sana mkuu, hapa nimekuelewa kabisa mkuu! Kuhusu huo uzi unaoelezea biashara ya china huwezi ku paste link mkuu? Maana nduo njia rahisi yakuupata.
Sent from my iPhone using JamiiForums