MTV MBONGO
JF-Expert Member
- Feb 18, 2016
- 1,281
- 1,251
Nina milioni 25, naweza wekeza kwenye nini ili nipate pesa nzuri kwa muda mfupi?
Wadau mawazo yenu Tafadhali.
Mchango wa mdau
Pia soma: Biashara gani zinazoingiza mamilioni kwa muda mfupi?
Wadau mawazo yenu Tafadhali.
Mchango wa mdau
Kama huna wazo la kufanya Biashara yoyote mpaka umepata hiyo hela tayari umeshafeli.
Biashara Ni wito kutoka moyoni mwako Kuna asilimia chache ya kutusua biashara ambayo umeambiwa au kusikia.
Nakuomba utulie na utafute Jambo unaloweza kufanya wewe hata Kama umeambiwa ila lazima liendane na moyo wako. Usipelekeshwe kuwa umesikia biashara flani inalipa.
Kwa muda huu uko kwenye utafiti nakushauri hiyo hela fungua fixed account bank iweke hiyo hela wakati kichwa kikiwa kina chaji.
Ushauri wangu kwako kwasababu hauna uzoefu wa biashara, fungua biashara yenye moderate risks iwe rahisi kuiendesha.
Nakushauri fungua biashara ya chakula. Tafuta ene lenye mzungo wa watu wengi. Fungua goli asubuhi uza supu , mchana weka nyama choma na ugali na usiku weka chapati na maharage. Hii ni biashara inayolipa sana . Kulaza faida 70,000- 150,000 ni Jambo lA kawaida Sana. Ila zingatia Location.
Nakusisitiza biashara utakayoweza kwasasa kwa level yako ni biashara ya chakula. Mkuu watu huwa wanakula hata kama wako Vitani.
Pia soma: Biashara gani zinazoingiza mamilioni kwa muda mfupi?