Nina milioni 25, naweza kuwekeza kwenye nini ili nipate pesa nzuri kwa muda mfupi?

MTV MBONGO

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2016
Posts
1,281
Reaction score
1,251
Nina milioni 25, naweza wekeza kwenye nini ili nipate pesa nzuri kwa muda mfupi?

Wadau mawazo yenu Tafadhali.

Mchango wa mdau

Pia soma: Biashara gani zinazoingiza mamilioni kwa muda mfupi?
 
Chukua 10 zungusha 15 kanunue bond ama fixed account itakulipa. Hiyo kumi fanya biashara ya kuuza nafaka. Ukicheza na 25 ambayo naamini ni ya mirathi ya mzee wako laana itakuwa katika paji la uso wako.

Hiyo pesa mmeuza nyumba mpo wanne mmekula 25 each. Ndugu kama unaweza wekeza kwenye real estate ya Chamazi 15M unajenga nyumba unauza 55M. Zaidi ya hapo italia ni pesa ndogo sana hiyo.
 
Anzisha kampuni ya kujenga makaburi, utatengeneza pesa hadi uchanganyikiwe, hutaamini macho yako; yaani watu kwenye kujengea makaburi huwa hawataki hata kubargain bei, Ukimwambia kaburi milion 6 anakwambia nipe account namba. Mfano waliojenga kaburi la JPM, wale washakuwa matajiri tayari, kwa ile kazi moja tu. Nenda Instagram uone watu wanavyopiga mpunga kimasikhara
 
Wekeza kwenye spare za magari. Anza na zile ndogondogo zinazohitajika wakati wa service za magari....sparkplugs, air and oil filters, oils, coolant....mdogo mdogo utaanza kuongeza heavy spare parts.....oil filter kwa mfano ya toyota maduka ya jumla utanunua kwa bei isiyozidi sh 4000. Rejareja utauza kwa sh 10,000
 
Walipewa tenda suma jkt & jwtz.
 
Bro amka, hakuna nyumba utakayojenga kwa 15m then ukauza 55m labda hapo uuze kiwanja ambapo kipo hot kinoma,,
 
Kwavile huna uzoefu na biashara we nunua bodaboda 5 utakuwa umetumia kama 12m.

Ambazo kila siku zitakuingizia 50k usizitumie uwe unaweka bank tu
Kwa muda wa mwaka mmoja utakuwa na 18, 250,000
Hapo sasa utakuwa na uzoefu wa mambo ya biashara hivyo utaamua ufanye nini kujiendeleza zaidi

Hela zilizobakia chukua kama 3m fungua biashara ya msosi na usimamie mwenyewe

Ila kama utaamua kusimamia kwa simu basi itakula

10m weka akiba utakuja kunishukuru baadae
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…