Nina milioni 45, nifanye biashara ipi kati ya hizi?

Mkuu ninajua real estate imekuwa ngumu na wazo langu hapo limezingatia hali ya sasa.

Pamoja na mazingira ya sasa unadhani wafanyakazi ambao bado familia ndogo au wameanza kazi wa mashirika mabenk,makampuni makubwa, wakuu wa idara au halmashauri za serikali wanakaa wapi?

Au ata watumishi wenye uwezo na umri lakini wanaishi mbali na familia wanaishi wapi?

Kilichotokea wafanyakazi niliowataja wameacha kupangishia vimada na kurudi kwa familia zao na kukwepa majumba ya kulipa laki tano nne sita ndio maana nikasema sio mijumba mikubwa apartment ambazo hazifiki Million 50, ninachokiongea millioni 50 ni aparment tatu.

Pamoja na hali ya sasa wafanyakazi wa sehemu kama TRA,PSSF,CRDB,TANRAOD,NMN,NSSF, wakuu wa idara halmashauri au kwa RAS, Medical Doctors,makampuni makubwa, kwenye hiyo mikoa unadhani wanakaa kwenye nyumba za elfu hamsini? hapana wanaishi kwenye apartment au myumba za laki mbili au zaidi.

Ata wewe kama unapata reasonablle income, umeelimika,una familia ndogo huwezi kukaa nyumba ya 50,000.00 labda kama ulichukua mkopo wa gari ukabakiwa na mshahara wa laki mbili na nusu. [emoji16][emoji16][emoji16] just joking.

Whatever challenge, what matters is your business model and customer target.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
True m50 kusubiria faida ya laki 3 per month plus changamoto za wapangaji kulipa ni bora nijenge frem kumi angalau.Ila real estate ni biashara nzuri kwa kustaafia,na sio mwenye speed ya usakaji
Mkuu ukiwa na kiwanja na good site plan 50 unajenga apartment tatu za vyumba viwili na sitting room utakazopangisha laki mbili au zaidi kila moja.

Nikwambie kitu mkuu mimi najua real estate haina return ya haraka sana lakini my ideas is

i. Jifunze maarifa ya biashara na jinsi ya kufanya kazi

ii. Ukipata nafasi wekeza kwenye biashara na nunua kiwanja kwenye potential area.

iii.Ukipata nafasi tanua biashara na jenga nyumba ndogo kwani nyumba kubwa zinatumia pesa nyingi ambazo hazirudi kwa kodi, lakini ndogo ni nora pia nyumba unapokwama kwenye maisha ndio kitu pekee kwenye maisha kitakacjokustiri fall back, BTW nyumba is long term investmest ambayo inaongezeka value in term of year.

Iv. Ukiwa una nyumba ata moja hasa sehemu unayotarajia kuishi maisha yako wewe focus kwenye biashara tuu ukipenda nunua kiwanja kiache tuu

Usipokuwa makini pesa zote zinaweza kuisha kabisa ukiwa huna pa kulala

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kaka Mmh naomba kuuliza Mpunga wapi elfu 36
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiweka 10m fixed akaunt riba Yake kwa mwezi inakua sh ngap mkuu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
True real estates ni kama life backup maana hatuna garantii ya kesho yetu hasa ukwamapo kimaisha uongo familia haifi njaa hata mtu akili utulia wakati ukisaka miundombinu mingine unamwachia wife aangalie familia kupitia houses
 
Tunis akili yako unatafuta wakumlaumu baadaye
 
Nimekuelewa sana mkuu! Point yangu ni hii . nimekupangisha ww unanipa 1.8m kwa 6mths!...ni bora nifungue kiwanda nisage unga hyo 1.8 naweza ipata kwa tons chache sana za mahindi tena mapema tu!
Haijalishi nampngisha boss gan lakini thaman ya pesa ndo naiona hairidhishi!..
 
Kama huna ajira rasmi, option 2 ndo nzuri zaidi. Ila mpe muhinde 35 baki na 10 then tafuta eneo la heka 10-20 uanze kulima mwenyewe na kulimia watu ili upate hela ya muhindi asap
 
Kama huna ajira rasmi, option 2 ndo nzuri zaidi. Ila mpe muhinde 35 baki na 10 then tafuta eneo la heka 10-20 uanze kulima mwenyewe na kulimia watu ili upate hela ya muhindi asap

Sorry ww umewah kulima?
 
Kama huna ajira rasmi, option 2 ndo nzuri zaidi. Ila mpe muhinde 35 baki na 10 then tafuta eneo la heka 10-20 uanze kulima mwenyewe na kulimia watu ili upate hela ya muhindi asap
Ukute hujawahi kuwa hata na kabustani ka maua ...Kiliko sio easy kama unavyofikiri... Mwaka Juzi nimepata hasara ya maharage huko Morogoro Sina hata hamu .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukute hujawahi kuwa hata na kabustani ka maua ...Kiliko sio easy kama unavyofikiri... Mwaka Juzi nimepata hasara ya maharage huko Morogoro Sina hata hamu .

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndo maana anaddevisfy kipato chake, analima yy na analimia watu. hela ya kulimia watu anamlipa muhind na yy anaendelea kufanya kilimo chake
 
Kama huna ajira rasmi, option 2 ndo nzuri zaidi. Ila mpe muhinde 35 baki na 10 then tafuta eneo la heka 10-20 uanze kulima mwenyewe na kulimia watu ili upate hela ya muhindi asap
Wazo nalo 35 muhindi,10 navuta poweriller hp 10 plus waterpump,mipira,na sprinkler zake 5 hivi zile raingun zitupazo maji upana mita 50 kwa degree 360 nikalima nyanya,vitunguu,kabechi,bamia,viazi napeleka sokoni huku tata nimelikatia bima kubwa linapiga ruti ya nje ya mji yaani asubui nachukua hesabu kabla alijaondoka likiondoka linarudi kesho Mchana navuta tena hesabu naziweka fixed kwa mwaka mzima nachanga za tata na za shamba sitotoboa kweli?
 
Ah ah
duh we mwalimu nini hebu nioneshe hiyo bank yenye riba ya asilimia 120 kwa mwaka nami nikaweke laki yangu.....hiyo asilimia 10 ni kwa mwaka mzee ukiigawa kwa mwezi ni chini ya hapo haizidi hata buku 30 kwa mwezi
 
Ndugu mi naona una idea nzuri sana kikubwa ni implementation any of those idea can work out....na wanauchumi wanasema uaiweke mayai yote kwenye trei moja...kama ukiweza ivunja kama ulivyofanya hapo na kuamua kujitoa mhanga ni wewe tu ...wish you luck
 
Changamoto ni kupata Dereva makin anayejitambua kujua hii ni ofisi maana akifanya kosa tu barabarani tajiri ndo utoboka,mfano kubeba magendo,au vitu haramu,rejea ya wenye malori yao kubebeshewa wahamiaji haramu kisha Dereva kakimbia
 
Hahahaha,kitu Cha kuahidiwa na mbongo Mimi huwa siku zote sikiamini.
Ukitegemea mtego huo huo mmoja utaaibika tu mbeleni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…