Nina Millioni 1 nataka kununua vitu vya awali kwa ajili ya kufungua grosari (mini pub)

Nina Millioni 1 nataka kununua vitu vya awali kwa ajili ya kufungua grosari (mini pub)

Glossary na pub za siku hiz unahitaji uwekeze sana,ka-chimbo kawe kazuri, mziki mzuri, screen haya mbili, meza kali, viti vikali, fridge nzuri walau ile ya milango miwili (lengo ni kuvua paonekane decent) ,,,,,

Pia udizain kajiko ka kishkaji, huduma za mwanzo wwlai chips mishkaki, supu viwepo,,,, au mchemsho asbh mchana jion !

Kwa mwanzo tafuta kaunta mzuri anejielewa, na wadada wawili wa nje wenye mvuto haswa !

Mwanzo ni mgumu ila badae utakuja kupiga sana hela,,,,, alafu usijifanye classic uza bei elekezi !


Kwa haraka haraka walau ukodi frem, sehemu yenye kieneo kwa mbele upadizain pawe na muojekano ,,,,

Usisahu uwe na choo kisafi kizuri, maji yasikosekane mda wote !

Kwa haraka haraka 6m, halafu utafure mtaji kama 1.5m_2m !

Nmeongea kwa uzoefu, sijaropoka tu !

Ila kama unaraka pawe Glossary ya kawaida umekodi tu mfrem meza kadhaa ,karedio mshenzi, ka screen ka kuzuga 2.5m inatosha everything
Nataka ya kawaida kabisaa
 
Kwann?

Wale wanauza ndizi zilizo wiva stend ama karanga kwenye sinia unaweza nambia wana mtaji sh ngapi?
Wengine wanauza mihogo ya kutafuna unakatiwa kipande jero au buku yeye huko kanunua kila muhogo jero mzima akikata vipande3 anapata bukujero faida buku.
Na ndio hapo niliposema hapo juu mtaji sio fedha pekee wala faida sio jumla ya mauzo kutoa manunuzi huyo huenda amepiga matembezi siku nzima na kupiga sound mpaka mdomo umekauka na bado kuambulia matusi na watu kumletea story ambazo haziendani na biashara yake....
Wengine hata huwa hawana mtaji ni uaminifu tu anaenda kwa wauza ndizi wa jumla anapewa jioni au mchana anarudisha hela
Kama nilivyomwambia jamaa kwenye post yangu mtaji sio pesa pekee bali nguvu kazi na skills pia (tena hizi ni zaidi ya pesa) ukikosa hizo hata ukipewa trillioni baada ya miaka kadhaa utakuwa umekata mtaji
 
Hujawahi kurembea Dar ukaona wale wanaouza bia, konyagi mezani? Wale wana leseni?
Wanafanya kosa, kuuza vileo popote pale inabidi uwe na leseni ya vileo achana na hii tu ya kawaida ya biashara bali na ya vileo pia; Hao unaowaona ni kwamba wanavunja sheria..., Bora ingekuwa biashara ya kawaida ungesema wewe ni machinga na una mtaji chini ya 4M hence una kibali cha Machinga pekee (kama bado vipo)
 
Wanafanya kosa, kuuza vileo popote pale inabidi uwe na leseni ya vileo achana na hii tu ya kawaida ya biashara bali na ya vileo pia; Hao unaowaona ni kwamba wanavunja sheria..., Bora ingekuwa biashara ya kawaida ungesema wewe ni machinga na una mtaji chini ya 4M hence una kibali cha Machinga pekee (kama bado vipo)
Hata machinga wanatakiwa wawe na leseni na TiN ila hawana,ndiyo bongo ilivyo
 
We nawe kumbe kichwani maji. Amesema anunue aweke ndani ili aendelee kujikusanya, sio kwamba hiyo M ndo anafungua biashara. Unakimblia wapi kwani?
Hata kwa kuanza hapana hiyo bado haitoshi mkuu ni ndogo kabisa an
 
Back
Top Bottom