Nina millioni 80 nataka ushauri wa biashara

Kwa anayeogopa/asiyeweza biashara kama mimi, pesa hizo angeweza kuziwekeza mahali pa kupata faida ya10% - 12% kwa mwaka (si pungufu ya milioni 8). Mfano mzuri ni kununua vipande vya mfuko mojawapo wa UTT, kwa mfano Jikimu, ambapo kila miezi mitatu (ukipenda) unapata gawio lako.
 
Nunua mobile crane ya 30tonnes au zaidi! inauzwa zaidi milioni tsh 150/- nje ya nchi na bado kuileta na kulipia ushuru na mengineyo! Jitahidi iwe kwenye hali nzuri!

Demand ipo juu kidgo kwa sasa....na mtu akiikodisha kwa siku anakulipa sio chini ya milioni mbili kwa siku! Na mara nyingi hukodishwa kwa wiki hadi mwezi mzima!

Kwa hela ulionayo...na kama unayo account inayo operate, baadhi ya benk hutoa mikopo ya kununua aina heavy machine ili mradi tu wewe una na 20% ya cost ya hiyo mashine....kadi watabaki nayo hadi umalize mkopo!

Biashara hii haisumbui.....mteja anakupigia (ukiwa unaendelea na shughuli zako, mnaelewana)......operata anaipeleka na kuanza kazi! Kijana mwingine atakaye kuwa na operata ni msimamizi wako na kumsaidia operata vitu vidgo vidgo!

Brand gani ya crane ununue nk, ukiwa interested na hii bishara uliza hapahapa kwa faida ya wengi....nitaeleza!
 
Kwa wazo kama hili huwezi pata maendeleo kabisa! mil80 utegemee faida ya ten percent kwa mwaka hailipi kabisa.
 
Mkuu huo mtaji ni mkubwa sana,tengeneza rebo yako kisha anza kupaki sembe.Funga 5kgs,10kgs,20kgs,25kgs na 50kgs!

Tafuta site nzuri fungua duka kubwa kwa ajiri ya kusupply.pack na unga wa muhogo na dona,uza jumla na rejareja.

Ni ideal nzuri lakini breakdown ya investimate yake na faida yake imekaaje?
 
Kwa anayeogopa/asiyeweza biashara kama mimi, pesa hizo angeweza kuziwekeza mahali pa kupata faida ya10% - 12% kwa mwaka (si pungufu ya milioni 8). Mfano mzuri ni kununua vipande vya mfuko mojawapo wa UTT, kwa mfano Jikimu, ambapo kila miezi mitatu (ukipenda) unapata gawio lako.

Hapana hii nilishafanyaga kwenye nico ikaniumiza sana sithubutu tena
 
Massage shop inalipa kweli, tafuta nyumba sinza na warembo wa maana kama 5 hvi. Utapiga hela kuliko bakhreasa
 
Nunua mobile crane ya 30tonnes au zaidi! inauzwa zaidi milioni tsh 150/- nje ya nchi na bado kuileta na kulipia ushuru na mengineyo! Jitahidi iwe kwenye hali nzuri!

Demand ipo juu kidgo kwa sasa....na mtu akiikodisha kwa siku anakulipa sio chini ya milioni mbili kwa siku! Na mara nyingi hukodishwa kwa wiki hadi mwezi mzima!

Kwa hela ulionayo...na kama unayo account inayo operate, baadhi ya benk hutoa mikopo ya kununua aina heavy machine ili mradi tu wewe una na 20% ya cost ya hiyo mashine....kadi watabaki nayo hadi umalize mkopo!

Biashara hii haisumbui.....mteja anakupigia (ukiwa unaendelea na shughuli zako, mnaelewana)......operata anaipeleka na kuanza kazi! Kijana mwingine atakaye kuwa na operata ni msimamizi wako na kumsaidia operata vitu vidgo vidgo!

Brand gani ya crane ununue nk, ukiwa interested na hii bishara uliza hapahapa kwa faida ya wengi....nitaeleza!

Mimi kwa kweli hivi vyombo vya moto naviogopa sana kuinvest huko manake nikilinunua lazima litakua used je ingini yake ikifa na nimeshaivest hela yote na benk nimekopa nitakimbilia wapi si itakua mwanzo wa kuchanganyikiwa?
 
Massage shop inalipa kweli, tafuta nyumba sinza na warembo wa maana kama 5 hvi. Utapiga hela kuliko bakhreasa

Hilo nalo neno hapo nimekupata mkuu,Massage kwa kichwa kimoja inaenda kama kiasi gani?mitambo ya kufanya hiyo kitu inabei gani?
 
Wakuu hebu nipeni ushauri wa biashara nimepata hizo pesa hapo juu millioni 80 lakini kila nikichekecha biashara ya kufanya ilipe nakua sioni sasa nimeiona niweke hapa ili nipate mawazo nijue pa kuanzia.Mimi naishi mkoa wa Dar-es-salaam

Fanya biasha ya real estate uwe unapokea kodi tu mwisho wa mwenzi Na risk yake ndogo. Ila tafuta consultants kwanza watakuelekeza namna ya kufanya.
 
Kwa wazo kama hili huwezi pata maendeleo kabisa! mil80 utegemee faida ya ten percent kwa mwaka hailipi kabisa.

(a) Lakini ujue hata wafanya biashara wakubwa wenye uelewa sana pia huweka mapesa mengi kwenye unit trusts mkuu. Hii ni kwa sababu wanaona ni vema kuweka sehemu ya fedha zao mahali penye risk ndogo, japo faida pia ni kidogo (b) Ujue kwamba sio kila mtu anaweza kufanya biashara za faida kubwa na zenye risk kubwa. Wengi wanaojaribu bila ujuzi, uzoefu na mipango yakinifu huishia kupoteza kabisa mitaji yao.
 
Ni kweli lakini ndio hivyo nimeshazipata tayari na siwezi kuzitupa lazima nifikirie biashara ya kufanya ziongezeke badala ya kuweka benk tuuu
weka Akiba inayokuwa, Ktk hizo hela, nunua eka 20 za kuotesha miti ya Mbao iringa kwa sh 1.3m, miche sh 1.2m, labour 1.0m, matunzo ya shamba kwa miaka kumi Yaani firebreak ni 2.0m, pruning kwa miaka kumi 1.0m. Jumla ni Tsh 6.0M. Halafu zinazobaki ndio uingie Ktk biashara utakayochagua. Baada ya miaka kumi hii Tsh 6.0m itakuwa inakaribia kufika Tsh 200M
 
  1. Biashara ya kuvyatua matofali na kuziuza kama utapata site nzuri ya biashara hiyo kwani ni biashara nzuri sana na inaliipa watu wengi wametoka kwa hiyo biashara na sasa wapo mbali hivyo unaweza kufanya hiyo biashara
  2. Duka la vipodozi nayo ni biashara nzuri sana kwa sasa kama utakuwa na sehemu ambazo kuna movement ya watu hivo ni moja ya biashara ambayo watu wengi wametoka kwa hiii biashara
  3. Duka la pembejeo za kilimo kama upo mkoani nayo ni muhimu sana kwani ni moja ya mahitaji muhimu sana hasa katika kipindindi hiki katika swala la kilimo kwanza na hapa uwe makini na maeneo mazuri ya kufungua hii biashara
  4. Duka la spare za pikipiki aina ya mbalimbali na duka likichanganya unaweza kuweka na hudumu za upepo wa kujaza magurudumu ya bodaboda.
 
Try this at your own risk - mtafute Mwigulu Nchemba muhonge milion 50 akusaidie kupata ubunge 30 zilizobaki tumia kwa kampeni then ukiingia mjengoni we kazi yako ni kuitikia tu ndiooooo na kugonga meza unaingiza 17m kwa mwezi

hahahahahaha....
 
Hapana hii nilishafanyaga kwenye nico ikaniumiza sana sithubutu tena
(a) Pole sana kwa bahati mbaya hiyo. Lakini bila shaka umesikia kwamba walionunua hisa za badhi ya makampuni megine (kama TCC, TBL, nk) wanafurahia. Mkosi wa Nico usikukatishe tamaa. (b) Hata hivi vipande vya UTT ni tofauti kidogo na hisa za kampuni kama TBL, TOL, twiga, TCC, nk. Wao husambaza sana risk kwa vile wanawekeza sehemu mbalimbali kama katika hisa za kampuni, amana za benki, bond za serikali n.k. Uwezekano wa UTT kupata hasara na kushindwa kugawa faida au kuongeza thamani ya mitaji ni finyu sana.
 
Wakuu hebu nipeni ushauri wa biashara nimepata hizo pesa hapo juu millioni 80 lakini kila nikichekecha biashara ya kufanya ilipe nakua sioni sasa nimeiona niweke hapa ili nipate mawazo nijue pa kuanzia.Mimi naishi mkoa wa Dar-es-salaam
Kwani ni za pensheni kwa maana hicho kiasi lazima kukipata kwa kufanya mambo flani sasa si ujiongeze na hayo yaliyokupatia hiyo Mil 80
 
Nunua mobile crane ya 30tonnes au zaidi! inauzwa zaidi milioni tsh 150/- nje ya nchi na bado kuileta na kulipia ushuru na mengineyo! Jitahidi iwe kwenye hali nzuri!

Demand ipo juu kidgo kwa sasa....na mtu akiikodisha kwa siku anakulipa sio chini ya milioni mbili kwa siku! Na mara nyingi hukodishwa kwa wiki hadi mwezi mzima!

Kwa hela ulionayo...na kama unayo account inayo operate, baadhi ya benk hutoa mikopo ya kununua aina heavy machine ili mradi tu wewe una na 20% ya cost ya hiyo mashine....kadi watabaki nayo hadi umalize mkopo!

Biashara hii haisumbui.....mteja anakupigia (ukiwa unaendelea na shughuli zako, mnaelewana)......operata anaipeleka na kuanza kazi! Kijana mwingine atakaye kuwa na operata ni msimamizi wako na kumsaidia operata vitu vidgo vidgo!

Brand gani ya crane ununue nk, ukiwa interested na hii bishara uliza hapahapa kwa faida ya wengi....nitaeleza!

Mkuu ni vp ukinunua hiyo kitu then ukakosa wateja? 150m inakua imelala how are you sure utapata wateja?
 
Mkuu tafuta shanba walau 50 acres unazoweza pata kwa around 5m chimba kisima kwa around 15m set irrigation system anza kufanya hortculture itakulipa tu
 
Back
Top Bottom