Nunua mobile crane ya 30tonnes au zaidi! inauzwa zaidi milioni tsh 150/- nje ya nchi na bado kuileta na kulipia ushuru na mengineyo! Jitahidi iwe kwenye hali nzuri!
Demand ipo juu kidgo kwa sasa....na mtu akiikodisha kwa siku anakulipa sio chini ya milioni mbili kwa siku! Na mara nyingi hukodishwa kwa wiki hadi mwezi mzima!
Kwa hela ulionayo...na kama unayo account inayo operate, baadhi ya benk hutoa mikopo ya kununua aina heavy machine ili mradi tu wewe una na 20% ya cost ya hiyo mashine....kadi watabaki nayo hadi umalize mkopo!
Biashara hii haisumbui.....mteja anakupigia (ukiwa unaendelea na shughuli zako, mnaelewana)......operata anaipeleka na kuanza kazi! Kijana mwingine atakaye kuwa na operata ni msimamizi wako na kumsaidia operata vitu vidgo vidgo!
Brand gani ya crane ununue nk, ukiwa interested na hii bishara uliza hapahapa kwa faida ya wengi....nitaeleza!