Nina millioni 80 nataka ushauri wa biashara

Nina millioni 80 nataka ushauri wa biashara

Wakuu hebu nipeni ushauri wa biashara nimepata hizo pesa hapo juu millioni 80 lakini kila nikichekecha biashara ya kufanya ilipe nakua sioni sasa nimeiona niweke hapa ili nipate mawazo nijue pa kuanzia.Mimi naishi mkoa wa Dar-es-salaam

Hebu kwanza twende nikakuonyeshe bar yenye mademu wakali
 
Nina kazi ya 140mil ni kazi ya barabara.kwa 80mil, hatukosi 35mil faster.karibu tusongeshe.au nipigie 0712660713
 
hahaaasss wa tz mkiona pesa ndefu mnawaza starehe tuu... bro hii pesa ya ni ndefu sana.... lakini kwa mkoa wa dar kila fursa hapo nadhani imekamatwa.... mikoani kuna nyanja nyingi sana za kuwekeza.. kuna usafiri kama daladala _superroof, coaster..... maduka ya nguao na viatu... ww tu ... kama vipi nkopeshe milioni 20.......
 
Nunua zile screen kubwa za matangazo kama zile za palm beach moja unaweza pata kwa usd 14000 ukiwa nazo tatu moja town nyingine mlimani city nyingine stand au airport

Makampuni yote ya simu unakula vichwa
Benki zote wala vichwa
Makampuni ya bia n.k

Brilliant!
 
fanya biashara ya mbao just 30 milions inatosha na faida yake ni maradufu. me nikipata 10 millions nitakua nimeaga umaskini coz nimefanya utafiti wa hiyo biashara na nimejiridhisha kuwa ni mzuri sana

Hiyo biashara ya mbao imekaaje mkuu, hebu tushirikishe kidogo matokeo ya hiyo tafiti yako.. na kama hutojali tuambie with 10M ni jinsi gani unaweza kuaga kabisa umaskini kupitia hiyo biashara
 
Hiyo kamari ikoje koje mtaji wake kiasi gani na faida yake kiasi gani?

Sina hakika kama una hiyo amount, unless umeokota, maana kila unachoshauriwa hujui pa kuanzia asa uko karibu kulizwa alafu utarudi humu kuomba ushauri tena.
 
Wakuu hebu nipeni ushauri wa biashara nimepata hizo pesa hapo juu millioni 80 lakini kila nikichekecha biashara ya kufanya ilipe nakua sioni sasa nimeiona niweke hapa ili nipate mawazo nijue pa kuanzia.Mimi naishi mkoa wa Dar-es-salaam

Mkuu heshima kwako.
Simple way nakushauri tumia 500,000/= Au 1,000,000/= kuwalipa wataalam wa biashara wakushauri kitaalam kwani inaonekana you have a zero idea about business. Ukiendelea kuomba ushauri wa bure kwa kila mtu utaishia kufanya maamuzi yatakayopelekea hicho kidogo ulicho nacho kupotea!.
 
Wakuu hebu nipeni ushauri wa biashara nimepata hizo pesa hapo juu millioni 80 lakini kila nikichekecha biashara ya kufanya ilipe nakua sioni sasa nimeiona niweke hapa ili nipate mawazo nijue pa kuanzia.Mimi naishi mkoa wa Dar-es-salaam

Fanya survey dubai na china uone. Binafsi ungeingia ktk uagizaji na usambazaji wa karatasi. Usinunue zaidi ya usd 2 per rim
 
Subayi, una haki ya kufikiri unacho fikiria lakini naweza kukuapia mbele ya miungu yote kuwa at the moment crane zenye tani 20 ni nyingi sana, hivyo kazi za kugombania! Na zenye tani 25 sio nyingi sana lakini kazi zipo na hazipumziki! lakini kuanzia tani 30 kwenda juu ni chache na kazi ni nyingi mno mno! Mara iringa, mbeya, dar kwenyewe, tanga, mtwara nk! kazi ni nyingi sana!
Kwa upande fulani nipo kwenye hilo eneo la kibiashara hivyo nafahamu! Kazi zipo nyingi sana, na hata ukitaka kuuza wateja ni wengi mno mno!

Hizi heavy equipment....haziozi, na hata zikiharibika zinatengenezeka na spea zipo! Na kwakuwa ni biashara yako utakuwa unafuatilia kila kitu na hasa service zake!

Pia mkuu, embu fanya risech kidgo...jifanye una kazi ya tani 30, kwa siku tatu na utanataka crane.....ukiipata kwa haraka...mshukuru mungu....vinginevyo utasubir kidgo....na bei yake utakuja kutoa ushuhuda hapa!

Mkuu kwanini hao wenye crane za ton 20 kushuka chini hawanunui za ton 25 kuendelea, ina maana hazilipi au? Kama inalipa kwa kuwa watakuwa na faida kubwa kutokana na crane zao za ton 20 nahisi wangenunua tu...mawazo yangu tu hayo
 
Wakuu hebu nipeni ushauri wa biashara nimepata hizo pesa hapo juu millioni 80 lakini kila nikichekecha biashara ya kufanya ilipe nakua sioni sasa nimeiona niweke hapa ili nipate mawazo nijue pa kuanzia.Mimi naishi mkoa wa Dar-es-salaam

Mkuu tangu uweke huu uzi akna mama wangapi wameku-pm?
 
Nunua zile screen kubwa za matangazo kama zile za palm beach moja unaweza pata kwa usd 14000 ukiwa nazo tatu moja town nyingine mlimani city nyingine stand au airport

Makampuni yote ya simu unakula vichwa
Benki zote wala vichwa
Makampuni ya bia n.k

Issue utapataje nafasi ktk hayo maeneo ili uweke na ww bango/video yako kwakuwa washayawahi....labda uwe mvumbuzi utafute sehemu zingine
 
Mkuu nenda kwa mzungu ukabeti,weka timu moja tu let say chelsea,weka mzigo wote kaka,unaweza kutoboa kama Dr.Leaky wa channel 10 vile,kwa mil 80 hata kama chelsea ikipewa point ndogo unapata mkwanja mrefu sana,ss watoto wa mjini hz ndo biashara zetu,daily twala,twanya,twagonga mademu masuperstar unaowajua wewe bongo yote,tumejenga masaki kwa hela hz hz za kubet,hatuibi wala nn lakini mawaziri wanatuogopa hapa jjijini
 
Hizi pesa kweli haziji kwenye vichwa vyenye mawazo kibao ya biashara!
Ningekuwa mimi nisingejenga hiyo Guest House, kwa sababu hesabu ya harakaharaka hiyo guest ya 80M ni vyumba kama kumi tu (Guest ya Kawaida sana Mkoani), hapo bado utakuwa unadaiwa pesa ya furniture na mambo mengine! Ukiwa unapangisha 20K kila chumba, say una bahati ya location kila siku vikajaa vyumba saba utakuwa na 140K kwa siku, ondoa 50K ya gharama unabakiza faida ya 90K, mwisho wa mwezi una faida ya 2.7M pekeyake! Itakuchukua miaka kama mitatu kurejesha gharama za ujenzi ndiyo uanze kula faida..hapo nadhani utakuwa unajiandalia mazingira ya kustaafu, obviously baada ya miaka hiyo mitatu guest itakuwa imechoka na kuchuja, Guest nzuri zaidi zitakuwa zimejengwa maeneo hayo na soko lako litashuka!! Sisi wakomaaji wa mjini tukizikamata 50tu basi ntolee, lazima ilale 20M kila mwezi FAIDA! Nina project zangu mbili ziko kwenye vitabu zinahitaji kama 300M na 700M respectively hizo hazina ushindani wowote bongo, ni suala la muda tu, dadeki!

Lakini kwa wewe mkuu ambaye nadhani haujawahi kufanya biashara ya namna yoyote ile ujue unaweza kupoteza kiasi kikubwa cha fedha katika kujifunza biashara, ukija kukomaa mtaji umepungua sana, na kama kazi ndiyo ulishaacha ni lazima ufulie vibaya. NAUNGA MKONO HOJA YAKO YA KUJENGA NYUMBA NA KUREJEA KUAJIRIWA!

Hizo project zako ni zipi tishirikishe mkuu...wenda unaweza kupata wawezeshaji humuhumu ndani
 
huyu anazingua tu....yaani upate mln 80 alafu usijue cha kufanya......since 2013 mpaka leo
haiwezwkani
 
@nalo neno

ukiwa na yenye uwezo mdogo wa kubeba tani nyingi...maanake ni kuwa huna soko, maanake huna hela ya kununua yenye tani nyingi! Kiswahili kingine ni kuwa, ukiwa na yenye uwezo wa kubeba tani nyingi.......mfano ya tani 40 na zaidi....ina maana hata ya tani 20 unabeba!
 
Back
Top Bottom