Hizi pesa kweli haziji kwenye vichwa vyenye mawazo kibao ya biashara!
Ningekuwa mimi nisingejenga hiyo Guest House, kwa sababu hesabu ya harakaharaka hiyo guest ya 80M ni vyumba kama kumi tu (Guest ya Kawaida sana Mkoani), hapo bado utakuwa unadaiwa pesa ya furniture na mambo mengine! Ukiwa unapangisha 20K kila chumba, say una bahati ya location kila siku vikajaa vyumba saba utakuwa na 140K kwa siku, ondoa 50K ya gharama unabakiza faida ya 90K, mwisho wa mwezi una faida ya 2.7M pekeyake! Itakuchukua miaka kama mitatu kurejesha gharama za ujenzi ndiyo uanze kula faida..hapo nadhani utakuwa unajiandalia mazingira ya kustaafu, obviously baada ya miaka hiyo mitatu guest itakuwa imechoka na kuchuja, Guest nzuri zaidi zitakuwa zimejengwa maeneo hayo na soko lako litashuka!! Sisi wakomaaji wa mjini tukizikamata 50tu basi ntolee, lazima ilale 20M kila mwezi FAIDA! Nina project zangu mbili ziko kwenye vitabu zinahitaji kama 300M na 700M respectively hizo hazina ushindani wowote bongo, ni suala la muda tu, dadeki!
Lakini kwa wewe mkuu ambaye nadhani haujawahi kufanya biashara ya namna yoyote ile ujue unaweza kupoteza kiasi kikubwa cha fedha katika kujifunza biashara, ukija kukomaa mtaji umepungua sana, na kama kazi ndiyo ulishaacha ni lazima ufulie vibaya. NAUNGA MKONO HOJA YAKO YA KUJENGA NYUMBA NA KUREJEA KUAJIRIWA!