Nina mimba na mtoto ana miezi minne, naomba ushauri wenu nifanyeje?

Nina mimba na mtoto ana miezi minne, naomba ushauri wenu nifanyeje?

Usimnyonyeshe Tena yule mwenzake mpe vyakula pain kama uji wa kishe ya mtoto ndizi za kusonga mtori na nk
 
Mwachishe maziwa yako mpe maziwa ya ng'ombe, alafu usilale nae kitanda kimoja. Mumeo mbona hana huruma.
 
Habar zenu wana jf!! Samahani sana kwa usumbufu, naombeni msaada wenu nifanyeje mwenzenu yamenikuta nipo njia panda sina cha kufanya.

Mwanangu bado mdogo miezi minne tu sasa na tayari nina ujauzito. Mtoto kashaanza kuhara kila siku na anazidi kunyong'onyea tuu. Hospitali walimpima hana tatizo, je nifanyeje? Nawaombeni sana mnisaidie ili niokoe afya ya mwanangu.

Najua kuna watu watanitukana ila yote sawa nastahili, ushari wako ni muhimu.

Asanteni.
zaa hamna shida yoyote
 
Jitahidi kumtengenezea balanced diet, protein ni muhimu sana katika umri huo kwani ndio anajenga mwili na kinga ya mwili vyakula vya wanga na mboga mboga na matunda, ikiwezekana blend matunda mpe puree au smooth anywe.
Mtoto wa miezi minne ampe hivyo?mi naona angeendelea tu kunyonyesha akifikisha miezi sita ndo amwanzishie hivyo vitu.
 
Nanyonyesha, na hadi hivi leo sijawahi kumpa mtoto chochote kile tofauti na maziwa yangu mwenyewe, tatizo saivi naona anaharisha
Kuharisha si tatizo.. nende spitali kampe kinga.. jamii ya chanjo.. mtto anakua kuharisha jumla ya uzima. mtto mdgo mavi yake yankua kama ayo.. hana mavi magumu.
Samahanini wadau kutumia maneno makali
 
Mimi naona hamna tatizo tena. Ila una stress tu kwamba umezaa ghafla bila kutarajia kwaio hata muda, waku muhudumia mtoto wako huta upata. Ataendelea kudhoofika kwa sababu na mama nae ana mawazo. Mbaya zaidi kama huna kipato na ndugu hawana muda na wewe,

Ushauri wangu, kubali lilopo na lililo tokea songa mbele.
 
Tafadhali acha kumnyonyesha mtoto kwani ni hatari,na atakuwa akitapika na kuhara ila mtafutie maziwa mbadara na pia mnunulie dawa inaitwa pedzinc na ors,atakuwa mzima kabisa ujifanya hivyo lasiivyo utampoteza mtoto kwani umembemenda.

Sent from my TECNO-Y3+ using JamiiForums mobile app
 
Amuachishe kunyonya fast maana apo maziwa yashatibuka naapate clinical nzuri wa mshuri juu ya mtoto na yy mwenyewe
 
Habar zenu wana jf!! Samahani sana kwa usumbufu, naombeni msaada wenu nifanyeje mwenzenu yamenikuta nipo njia panda sina cha kufanya.

Mwanangu bado mdogo miezi minne tu sasa na tayari nina ujauzito. Mtoto kashaanza kuhara kila siku na anazidi kunyong'onyea tuu. Hospitali walimpima hana tatizo, je nifanyeje? Nawaombeni sana mnisaidie ili niokoe afya ya mwanangu.

Najua kuna watu watanitukana ila yote sawa nastahili, ushari wako ni muhimu.

Asanteni.
Kitu muhimu hapo ni kumuachisha nyonyo, alafu zingatia mlo kamili kwa mtoto. Mtoto akisha nyonya miezi 3 huyo kasha vuka vikwazo we relax [emoji1] [emoji1]

Sent from my Y4 using JamiiForums mobile app
 
Usishtuke kwani sio wwnpeke yako. hayo ni mambo ya kawaida tu na hutokea kwa.bahati mbaya. Ila nakushauri uende clinic utapata ushauri mzuri na ulio bora kabisa. Kwani wao ni wazoefu wa shughuli hizo. Sisi wa mitaani wengi wetu hatuna uzoefu.
 
Back
Top Bottom