Nina mpenzi mpya ila mpaka mimi nimtafute

Tofauti yenu ni umri. Mpenzi wako amekomaa, wewe bado mtoto. Tafuta mwanafunzi mwenzio muwe mnachati.
 
Huyo ana stress na tozo za miamala, huenda madanga wake wanakataa kumtumia pesa kwa sababu wanakatwa mno
 
Hakuna mapenz hapo chapa mwendo utaumia sana moyo wako kwa mtu asie jali hisia zako sikushauri uwekeze kwa lolote lile
 
  • Kwanza acha kuamini unae mpenzi, chukulia kwamba bado unamsomesha binti na yeye bado hajakuelewa.
  • Achana na mambo ya kumuadikia maelezo marefu. Yaelekea huyo binti anapenda chat fupi fupi, hivyo maelezo marefu yanamchosha tu.
  • Elfu 30 hujaipoteza bali umewekeza. Usisite kuwekeza zaidi😀 Ukianza kuwaza hiyo pesa umepoteza ujue na binti utampoteza kweli.
  • Hizo zawadi za kama elfu 30 ni za makopo ya juisi ya ukwaju? Hebu badili aina ya zawadi jombaa.
 

Wewe ni Ke au Me? Kama wewe Ke na ushaliwa sio ajabu, na Me vile vile hauna maajabu na sio ajabu hio pesa wapo wenye shida elfu2 kwa siku anakuona malaika. Reference ya mbwa ya mdau usiipuze paukwa pakawa
 
Tabia za wanawake wazuri hizo, kifupi anakupa wakati wa kukupima, je una fit vizuri kama mwanaume, kikubwa acha papara, kama unapenda kuchat sana tafuta marafiki zako wa kike wengine chat nao hivyo, yeye mpe nafasi, kaa nae kwa mwaka mzima halafu mwambie unataka muishi kama mme na mke, akikubali sawa akisema bado, piga chini!! tafuta mwingine!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…