Nina mpenzi mpya ila mpaka mimi nimtafute

Nina mpenzi mpya ila mpaka mimi nimtafute

  • Kwanza acha kuamini unae mpenzi, chukulia kwamba bado unamsomesha binti na yeye bado hajakuelewa.
  • Achana na mambo ya kumuadikia maelezo marefu. Yaelekea huyo binti anapenda chat fupi fupi, hivyo maelezo marefu yanamchosha tu.
  • Elfu 30 hujaipoteza bali umewekeza. Usisite kuwekeza zaidi😀 Ukianza kuwaza hiyo pesa umepoteza ujue na binti utampoteza kweli.
  • Hizo zawadi za kama elfu 30 ni za makopo ya juisi ya ukwaju? Hebu badili aina ya zawadi jombaa.
Yes mkuu nipeleke zawad zipi labda ataelewa somo
 
tabia za wanawake wazuri hizo, kifupi anakupa wakati wa kukupima, je una fit vizuri kama mwanaume, kikubwa acha papara, kama unapenda kuchat sana tafuta marafiki zako wa kike wengine chat nao hivyo, yeye mpe nafasi, kaa nae kwa mwaka mzima halafu mwambie unataka muishi kama mme na mke, akikubali sawa akisema bado, piga chini!! tafuta mwingine!!
Ndo niwekeze mwaka mzima kwel ujue inakatisha tamaa sana yaaan
Kuna kipind nikazuga naumwa hata kuulizia kuwa naendele aje hakuna
 
Polen na tozo za miamala

Mie nina mpenzi mpya kabisa ila tatizo nisipomtafuta mie baas ujue ndo siku imepita hvyoo...
Nikimwambia ' Nakupenda' anajibu ahsante
Nikimpigia simu anasema ana kazi atanitafuta badae baas hiyoo baadae mpaka mie nimtafute
Nikimtumia msg anajibu inshort sana yaaani naandika maelezo maelefu yeee anajibu sawa au asante
Ila nikimpelekea zawadi anapokea sana nimeisha poteza kama elf 30 hivi.
Huyo hana mapenzi na wewe, anakupa matukio ili ujiongeze mwenyewe uachane naye. Soma alama za nyakati mkuu, usipo angalia ipo siku atakutolea uvivu tu na kukuambia ana matatizo, anataka pango la nyumba la milioni 6 ili tu akukimbize.
 
Back
Top Bottom