Ni mwaka wa tatu sasa tangu niamue kabisa kuacha uzinzi na pombe na kuamua kutulia na mke wangu tu.
wakati wote nimejitahidi kuishi kwa kufuata neno la Mungu pamoja na kusali sana.
Nimezingatia kufunga, kutoa sadaka, zaka na michango mbalimbali.
Mwaka jana mwezi Agosti niliweza kununua tena kausafiri kazuri ka kutembelea,
sambamba na kuanzisha mradi wa kilimo cha bustAni kubwa.
mwezi wa pili mwaka huu, Mrs alipata changamoto kazini, iliyopelekea kuhamishwa kituo, hivyo nilijikuta nauza gari ili kulipa madeni ambayo tulikuwa tumejikopesha.
nimeendelea na kilimo lkn hadi sasa mtaji umeisha, sina namna ya kuweza kuendelea na mradi.
hivyo nimepoteza Gari yangu na mtaji wa mradi ambavyo nilifanikiwa kuvipata baada ta maisha ya wokovu wangu,
ikumbukwe huko nyuma nishaanzisha miradi mingi na ikafa,
Mbali na hayo mimi ni mwajiriwa, lkn nimekwama kbs kiutumishi,
nina miaka 14 tangu nihitimu shahada lkn sijafanikiw kupanda cheo kazini.
Kama mwaka na nusu umepita Kuna jamaangu nilimshauri kuhusu madhara ya uzinzi, akazingatia,
juzi nimekutana naye akiwa na furaha kuu kwa mafanikio aliyoyapata baada ya kuzingatia ushauri niliyompatia,
yeye anasema alituma kwa mchungaji mchango wa SH. elfu 20 tu mchungaji,
tangia hapo alifunguliwa na neema zinamfata mpaka sasa,
ikumbukwe wakati namshauri anasema alikuwa amekata kbs tamAa ya maisha,
miradi yake ilikuwa imekufaa, madeni kila kona, mshahara unapitiliza tu bila kununua hata shati,
sawa na hali ambayo naipitia mimi.
pmj na mambo mengi tuliyoongea,
amenishauri nihudhurie kanisani kwao kwa ajili ya maombi ya kufunga na kukesha,
kwamba RC ninakosali hakuna nguvu za kiroho,
npo njia panda sielewi kinachoniangusha na wapi ntApata msaada.
- kumradhi kwa uandishi na mpangilio mbovu,
penye utata uliza ntafafanua vzr
- Matusi na lugha za kejeli naomba sana viepukwe.