Nina mtaji wa laki moja. Je nifanye nini ili niwe napata angalau elfu mbili kwa siku?

Nina mtaji wa laki moja. Je nifanye nini ili niwe napata angalau elfu mbili kwa siku?

Wazo la bure.
Nenda kachonge kale kajiko kadogo hivi ka kuchomea mishkaki.
After that nenda machinjioni, nunua kichwa.
Kicharange vizuri hukoai japo kilo 4 au 5 (sina uhakika hapo).
Nenda sokoni, nunua viungo mbalimbali. Njoo marinade hyo nyama. Kisha nunua zile vimbao vya mshkaki.
Ikifika jioni, tunga hyo nyama kwenye hzo vimidenge, nenda sehem yenye mkusanyiko kama stendi hivi.
Panga vimishkaki vyako. Uza 200 vitatu jero.
Hakikisha una kasufuria kadogo ambako unapikia pilipili humo ndani so kanakua kanachemka kwa pembeni.
Usisahau ka taa ka sola ka kuning'iniza hapo kwa juu. Kama hela imebaki nunua ka redio ka bluetooth af ueke flash inayosema mishkaki mitamu 200 mitatu jero.
I got a feeling utapata zaidi ya 2000 ya faida na huo mtaji utakua bado umebaki.

Biashara ikichangamka ongeza mishkaki ya mapumbu ya ng'ombe, mmoja jero.
What a great idea,fuata Hilo wazo mkuu
 
Habarini wana jf.

Nimepata mtaji laki moja.je nifanyej ili nipate elfu mbili mpk elfu tano per day.

@everyone
Mkaa unalipa tafuta Chaka nunua miti choma mjini hapa Nusu kisado buku kisado kikijaa buku 2 ndoo ndogo buku 5/6 inategemea na ukubwa na ndoo kubwa buku 10

Sasa changamoto ni Chaka lipi? Tafuta mtaani kuna watu wanauza miti yao nunua nenda kachome mkaa

Bei ya mti mtaani haizidi 30 to 40k

Tafuta eneo changanyikeni huko mtaani uswahili huko hawatumik gesi baada ya kupata gunia zako kadhaa za mkaa paki hapo na makopo yako ya kupimia mkaa I'm telling you kwa siku utalaza 50k mpaka 100k
 
Anzisha mikopo kwa riba. Utawakamata sana wamama wa marejesho..
Bila bondi x3 ya mkopo usitoe hela.

Uzuri wa hii biashara huwa wanaitana wenyewe

No need of marketing
Hii haileti faida 2000 kwa siku. Na kufilisika ni nje nje. Purchasing power imeshuka sana. Maana Ili umpe mtu laki anatakiwa aje na mali inayozidi 150k _300k. Sasa mpaka upate mteja lazima utaona rangi zote
 
Hii haileti faida 2000 kwa siku. Na kufilisika ni nje nje. Purchasing power imeshuka sana. Maana Ili umpe mtu laki anatakiwa aje na mali inayozidi 150k _300k. Sasa mpaka upate mteja lazima utaona rangi zote
You are not in the Fìeld Dr. Luis!
Keep calm and Learn from elders
 
Mkuu kama uko dsm cha kwanza ondoa aibu ingia kariakoo kuna biashara nyingi ndogo ndogo unaweza kufanya

Kuna hii mikanda ya wanaume inayouzwa 3000, ambayo wamachinga wengi wanaitembeza sana k.koo ... ukifika ulizia chimbo wanaponunua kwa jumla, coz kwa jumla wananunua mkanda mmoja 1000, ukiweza kuuza hata mikanda mitano kwa siku hapo hapo k.koo hukosi 10000

Kuna nyingine ya kuzungusha maji ya kunywa na hiz soft drinks zingine .. pia unaweza kuifanya pia

Kwa mtazamo wangu hiz ni biashara nyepesi unazoweza kuanza nazo kama utakua dsm ...kama uko mkoani kwakweli ntashindwa kukushauri coz kila mkoa unatofautiana kwenye fursa

Kuna jamaa
Siku hizi anauza maji yapo kwenye dumu la lita 3 I think
Anauza 1,000
Anapitisha kila duka asubuhi
Jioni anapita kukusanya madumu yake na hela ..
Ana uhakika wa maisha
 
Back
Top Bottom